Mzee Jaji Warioba ndani ya Dk 45 ITV

Mzee Jaji Warioba ndani ya Dk 45 ITV

Hivi Warioba ni Chadema???

Mkuu kwa vile uko ughaibuni na Maccm yanawatetemekea nyie mliolowea na kuamua kuwa watumwa nchi za wengine, naomba sana uwashauri ccm na hasa vigogo wafanye kile tunachokiita kibiashara "Market Survey" kwa maana kwamba wafanye random study kwa kuwatumia wale vijana wa idara nyeti wapite sehemu mbalimbali waliko wakaulize wananchi ni wangapi wanakubaliana na "RASIMU YA TUME YA JAJI JOSEPH SINDE WARYOBA" Halafu ndio watwambie matokeo yake, na kama hiyo hawataweza wawatumie kile Kitengo chaocha UDSM chini ya Dr. Bana yaani "REDET" wawafanyie sudy kabla hawajapotezwa kenye ulingo wa siasa nchini. Majivuno kwamba mnashinda Kalenga, Chalinze wakati mmetumia Tume, fedha na vitisho na bila aibu mnajivuna ni dalili za ukosefu wa akili timamamu yaani ni upunguani.

Kama wajumbe wenu wanashindwa kujieleza kwenye midahalo halafu kwenye uchaguzi ndio mshinde ama kweli hili ni ajabu la Tisa la Ulimwengu liandikwe tu kweny Guiness Book of Records
 
ni saa 20:53 mwanza tumekatiwa umeme katika njama za kutokumuonyesha jaji warioba
 
Hivi Warioba ni Chadema???

LUKOSI, kwa Mtanganyika au Mzanzibari yeyote atakaye ita Jiwe kuwa ni JIWE basi kwa CCM huyo ni Mpinzania. HOja na Maamuzi ya CCM hakuna anayonufaika nayo kwa raia wa kawaida ispokuwa inner cycle members. Ukitataka kutumia akili yako ndani ya ccm utaitwa msaliti, mpinzani nk

Muungano wetu uliundwa na kulindwa kwa goodwill ya Mwl Nyerere na Karume, ukifuata sheria unamatatizo lukuki...Sasa ni wakati muafaka kuufanyia marekebisho lakini baadhi ya watu wameamua kuleta propaganda kama zako za kumpachika Mh Warioba umember wa CDM. Ndani ya tume kulikuwa na wanasheria waliobobea, viongozi waliotumika wakati wa awamu ya kwanza na wanaujuwa muungano na mapungufu yao kuliko wewe uliyeko England, kwa wao kutoa mapendekezo ya hivyo sio wa kubezwa hata kidogo bali tunatakiwa kujiuliza jinsi ya kuuboresha muungano bila kufarakana.

Kumbuka huwezi kuuwa uraia wa watu kirahisi....miaka ya 1870 wazungu walibadili majina ya miji ya Azania (now South Africa) ;lakini leo majina mengi yamerejeshwa kumbuka Pretoria now is Tshwane!!! Kwahiyo Tanganyika itarudi tu hata kama sio leo
 
...ameanza kwa kukataa kuzungumzia rushwa...
 
...anazungumzia upotoshaji na uongo wa bulembo...
 
bulembo na wasira washacjezea zauso.....chezea warioba wewe
 
Anasema wanaomtukana wanafanya hivo kwenye mikutano ya Ccm!
 
Wakuu ni wakati huu ninamfuatilia huyu nguli wa sheria na mambo ya katiba mzee wetu j.s. Warioba akipafafanua vipengele mbali mbali tuwe pamoja.
-anaanza kwa kumshangaa bulembo kuwa ni muongo kwa kujifanya anamfahamu wakati yeye hata hamjui.
-anakemea tabia ya kula kiapo cha kuingia msituni na pia ana mlaani na kumlaumu mwenyekiti wa kamati namba moja kwa kuwasilisha taarifa ya hovyo.
 
nipo naangalia hapa.sijui kwann ccm wanataka kupoteza amani iliyopo. Nawashangaa hata vjana wa ccm na akili zao wamepitwa hadi na huyu mzee.
 
Anaonesha masikitiko yake kwa hisia jinsi alivyotukanwa bila sababu, na uongo mwingi ulionenwa juu yake na akina Bulembo et al. Anasema hamjui kabisa Bulembo... Anasema baada ya kikao cha bunge alipigiwa simu na wajumbe waliokuwako BMK kuwa ampuuze tu Bulembo! Anamshangaa kama Bulembo ni mjumbe wa kamati kuu ya chama kinachoongoza dola, anaweza kuwa mzushi vile!
 
Ana ongeza kuwa wao hawajutii kutukanwa maana walifanya kazi nzuri waliotumwa na watanzania.
Anaeleza kuwa kuileta tanganyika hakuvunji muungano na anaendelea kusema kuwa mawaziri wa zanzibar wamegeuka kwani wao ndio walikuwa mstari wa mbele kuidai zanzibar yao.
 
Mawaziri wa ccm Zanzibar waumbuliwa na mzee warioba.!😀
 
Back
Top Bottom