ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
My people,
Unapomuacha mtoto wako aache sahani mezani baada ya kula sio tu kwamba unamfanya awe na tabia mbaya bali unamtengenezea mazingira ya kuwa na future mbaya huko ukubwani.Mtoto anapomaliza kula na kisha mzazi ukamuondolea sahani yake,hii inamjenga mtoto akilini kwake kwamba kuna mtu siku zote atakuwa around kumfanyia mambo yake,kwahiyo hana haja ya kuwa na mashaka na baadhi ya mambo kwani siku zote kuna mtu yupo pale kwa ajili yake
Hii imenikumbusha Prince William baada ya kukabidhiwa rasmi ufalme,akiwa pale mezani ana Saini nyaraka,peni haikuwa mbali na yeye ni swala la kunyoosha kidogo tu mkono na kuichukua lakini aliashiria msaidizi wake amsogezee,wale walio ona hiyo clip watakubaliana na mimi kwamba ule ndio ubaya wa malezi ya kufanyiwa kila kitu.
Haya wale ni familia ya kifalme je vipi watoto wako na wangu tunawatengenezea mazingira gani katika future yao?
Watoto wa namna hii huwa wanashindwa kuwajibika wanapokuwa watu wazima,kwasababu wameshazoea kufanyiwa kila kitu,na pale wanapoingia kwenye mazingira ambayo yanawalazimisha wawajibike na kuchakalika,wanaanza kulaumu kazi kwamba ni ngumu,au kulaumu boss mkali au hata kulaumu system nzima ya mpangalio wa kazi pale kwenye maeneo yao ya kazi
Kwahiyo tangu wakiwa wadogo wafundishe wajue kwamba hapo nyumbani sio hotelini kwamba kuna mtu atawafanyia au kuwahudumia ,bali hapo ni home wana kila sababu ya kuwa na jukumu la kushirikiana kufanya kazi,wakifika umri wa kufua nguo basi wafue nguo zao,hata kama una washing mashine,siku moja moja hakikisha wanafua kwa mikono yao,wafagie hapo nyumbani,hii itawajenga wawe watu wanao jua kuwajibika na watathamini kile ambacho wanakifanyia kazi
Kumbuka vijana wengi ambao leo hii hawawajibiki,hawataki kufanya kazi au hawajitumi,msingi mkubwa wa tabia zao hizi zilianzia nyumbani,kuna nyumba moja ya wapangaji ipo karibu na home,mazingira yake machafu,matakataka yapo hapo,majani hayaja limwa na wao wala hawana habari.
Hapo moja kwa moja unajua tu kwamba wamekutana watu ambao sio responsible, watu ambao ni goi goi na hawajitumi kusafisha mazingira yao,unaweza kabisa kujaji kuwa mazingira ya ukuaji wao haya kuwafunza kuwa responsible adults
Lau mie ningekuwa mmoja wa wapangaji pale,basi ama ningefanya usafi mwenyewe au kuwahamasisha wenzangu nao wajitume kusafisha mazingira yao
Kwahiyo kuwaacha watoto bila kuwajibika hapo home sio kwamba unawapenda bali unawatengeneza kuwa kizazi cha hovyo sana huko mbele ya safari
Kuwapenda watoto ni kuwaelekeza mapema kabisa kwamba wanatakiwa wajifunze kufanya shughuli mbali mbali hapo nyumbani na wakiwa wakubwa watakushukuru sana,nililima bustani,nilichunga ng'ombe na kukamua,nilifanya usafi wa mazingira,leo hii ni mtu wa kujituma sana kwasababu wazazi wallinifundisha toka awali kabisa kuwa a responsible man.
Ni hayo tu