Mzazi mwenzangu hahudumii mtoto; nataka nimpeleke mahakamani

Hio ndio akili ile ile aliotumiaga Hamisa kwa Mondi 😂
Nikuambie tu ukweli huyo dada anajua vizuri kwamba na yeye atafaidika, sio suala la selfish, kwa sababu kitendo Cha mwanaume kumuachia nyumba mwanamke ambaye ndoa Yao imedumu muda mfupi maana yake anajali ustawi wa mtoto wake, na haya yanazungumzwa hapa yamkini yako katika uhalisia huo japo mtoa mada hajataka kufunguka, kama mama anataka mwanae asome shule bora na anaamini Mzazi mwenzie ana Maisha mazuri ampeleke mtoto Kwa baba yake huko Baba ataamua mwanae asome shule gani hakuna Mzazi ambaye hapendi mwanae asome pazuri na uwezo anao, hebu jiulize kwanini huyu dada anakimbilia mahakamani?? Anajuafika kwamba mahakama itakuwa upande wake na itamuamuru baba alipe na Hela ya matunzo hapo mama atapata faida na kama mwanaume huyo anaishi na mwanamke hapo usijefikiri mama mtoto anamkomoa mwanaume no hapo analenga kumkomoa mwanamke mwenzie anayelamba sukari, swali la kujiuliza unafikiri huyo baba huko Hana watoto wengine na je ikithibitika anawatoto wengine ambayo wanamtegemea hiyo mahakama Bado itamlazimisha apeleke mtoto ingilishi midiamu??? Msitafute huruma kupitia watoto, huyo Mtoto hakubakwa alikubali Kwa Moyo mweupe na kumtunza amtunze Kwa Moyo mweupe hivyoo hivyo bila kutafuta sababu na visingizi
 
Ndio maana nawe nikakuambia kuwa wewe akili yako ni chenga.

Kama unajua kabisa watoto wote wanapaswa kupewa haki Sawa. Nini kinakufanya usimpeleke Mtoto Kwa Baba yake ili apewe Huduma na ndugu zake Kwa pamoja?

Kama unataka haki tenda Haki.
Ukiwa Mbali utapata Haki za Mbali
Ukiwa karibu utapata Haki za ukaribu.

Mtoto akiwa mbali ni Kama Mwanampotevu aliypotezea na Mama yake.

Ushaambiwa fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

Pia kiuchumi sio rahisi kuhudumia mtu ambaye yupo nje ya Mfumo. Na nigharama. Sijui wapi huelewi.
Mtoto anayelelewa na Mama yake yupo nje ya Mfumo wa Baba yake.
Ndio maana haya baadaye akikua ata-base na Kwa mama tuu

Mtoto unataka apate Haki zote Kwa Baba yake, mpeleke Kwa Baba yake.
Hutaki basi Acha kulalamika kuwa Baba hamjali mtoto ilhali wewe ndio humjali mtoto kwani hutaki kumpeleka Kwa Baba yake.

Unataka atumiwe Ada ili ujisifu Kwa watu huko unasomesha wewe kumbe anayesomesha ni Baba yake
Ukitaka sifa inabidi uzigharamikie.
Mkuu nakukumbusha tu kuwa mtoa mada ndio huyu Anita kaja na ID mpya kujitetea ndio maana humuoni mtoa mada, achana nae
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.
Si kakuaachia nyumba,Hela ya ada mwenzio kahamishia kwenye kodi.Cha msingi we dogo mpeleke Kayumba tu.Kama nyumba inawapangaji chukua kodi mtoto apate chakula.Hakuna kesi hapo.
 
Sasa mtoto kumlisha utalinganisha na ada? Ada kwa mwaka kwa shule za wapenda show off inaweza fika hata 4M kwa mwaka 😅 yeye kajichagulia kipengele cha kumlisha ambacho mtoto anakula kile kile anachokula yeye which is inexpensive compared na malundo ya school fees, unapigiwa simu inatakiwa laki 8 ya ada fasta.
Acha Upumbavu!! Nimesoma Private Indian Schools kuanzia Nursery Mpaka Secondary!! Eti unapigiwa simu inatakiwa laki 8 ya Ada Fasta!! Unafikiri hizo Ada unatoa Daily au kwa Kukurupushwa na Shule?Kwa taarifa yako Shule za Private unalipa in Installments… ni juu yako na uwezo wako wa Kifedha either ulipe kwa awamu 1,2 au 3.
 
Wanawake huwa wapuuzi sana hapo,
Ni kutaka kumkomoa tu mshkaji baada ya kuona wameachana na yuko vizuri bado.
Ukiona anaanza kukimbilia mahakamani ujue diplomasia imeshindikana.
Haya yalinikuta niliyamaliza kibabe ila usumbufu miaka mingi tulisumbuana saana toka mtoto akiwa na miezi 6-10 mpk nimemkomboa akiwa na miaka 13.
Kwahiyo asaivi una ishi nae.
 
Nyakati hizi tuna vijana wa kiume wanaokuwa miili tu lakini akili zinabakia pale pale.......ukifuatilia hii michango utalifahamu hilo.....na ndio chimbuko la mabinti wanaoitwa single moms.......
Ni huzuni kwakweli! Nchi zilizoendelea Serikali inahudumia Single Moms pamoja na watoto wao na kuwapa Nyumba ya Kuishi.
 
Sasa hapo ndugu una mfunza in hard way ni mama au mtoto wako mwenyewe.....??

Kwani madai ya mama ni kumhudumia yeye au mtoto wako.....??

Sasa kuacha kutoa huduma za mtoto wako kunamkomoaje mama mtoto wako....na kwanini ufikirie kumkomoa mtu ambaye anamtunza mtoto wako.....??

Kwanini unakwepa uwajibikaji kwa jambo ambalo umelisababisha mwenyewe.....??

Kwanini umpe adhabu kiumbe ambaye hakukuomba umlete duniani kwa kosa ambalo pengine hata halifahamu au ahusiki nalo......??
Utaratibu ni mtoto arudi kwa baba fullstop!
 
Loh pole sana

Usikwazike na majibu ya wanazengo wa humu

Kama upo Dar nenda pale Chang'ombe Mahakama kituo Junuishi ya Ndoa na mirathi. Kuna ofisi za WILDAF wanatoa ushauri mzuri kisheria kuhusu masuala aina hii.

Sheria inamtaka baba kugharimia matunzo ya mtoto hata kama mmeachana kisheria. Tatizo ninaloliona ni wamama wengi wamekuwa na moyo wa KUMUACHIA MUNGJ pale wanapokosa matunzo ya watoto.
Mdanganye mwenzako
 
Naomba msaada wa namna bora au mwanasheria atakayenisaidia kumpeleka mahakaman baba mtoto wangu ili angalau awe analipa ada tu.

Mtoto ana miaka 9 yuko darasa la nne siku zote nimekua nikimlipia ada na matumizi yote lakini safari hii hali imekua ngumu nimeshindwa na nimemuambia kiungwana tu kakataa kasema hana hela niuze nyumba nimlipie ada mtoto.

Alikua ni mtoto wa kwenye ndoa ila tuliachana kabla mtoto hajaanza shule.
Hivi hawa watu wanaofurahiaga shida za wengine shida huwa nini ??
Semeni tu mtu anatoa post za masikitiko limtu lenye ma'xxxmbu yaliozeeka yanacheka cheka kama ni raha mwenzenu kuteseka hivi moderator wapashe hawa makenge au wablock hii inakera au unakuta ni mwanamama anayejieshimu anafurahia shida za mtu mo nakerekaga sana
 
Wanawake wanamatatizo Sana Mimi wangu alinipokonya mtoto na kashfa kibao kwamba Mimi maskini siwezi mtunza mwanae na nikimuhitaji masharti kibao lakini Leo hii ananitafuta nitoe maela kwa mtoto na Mimi namkazia tuone yeye si alisema yupo vizuri atamtunza mwenyewe na anauwezo minipozangu tu namtazama kama nacheki derby ya kariakooo
Kesi yako imefanana na yangu moja kwa moja

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom