Mzazi mwenzangu ananitukana sana

Mzazi mwenzangu ananitukana sana

ANDERSON YM

Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
76
Reaction score
32
Habarini;

Nina tatizo moja kuna mdada nilizaa nae mtoto mmoja wa kiume kutokana na maisha nilimpangia pa kuishi na nikaa namhudumia mpaka sasa. Cha ajabu ukimpa pesa ya matumizi mfano elfu hamsini haipiti siku tatu imeisha, nikimwambia huanza kunitukana matusi na kudharau kazi yangu inayomtunza.

Siku hizi amemwita ndugu yake wa kike mmoja anakaa nae hapo nilipompangia, wana umri sawa ni matusi kila mda na amesema mtoto si wangu nisimjue na kule nisikanyage na wala nisimpigie simu na hahitaji chochote kutoka kwangu.

SASA TATIZO; niliwahi kumsitishia huduma kutokana na tabia zake za kunitukana na kusema nisimjue mtoto na nyinginezo, lakini cha ajabu akaja ofisini mpaka kwa bosi wangu eti mimi simtunzi tangu mimba jambo ambalo ni uongo, alishawawahi kwenda mpaka ustawi wa jamii nikiitwa yeye anatokomea mitini, yaani imekuwa ni usumbufu.

JE NIFANYEJE MAANA NIMESHAMCHOKA SANA!

Mchango wenu tafadhali.
 
Mkuu usije ukawa ndo wale wale wa kuwakimbia panya road,kulamba mdomo,na kumwogopa scorpion, ooohh angalia,mwanamke atakutukanaje aisee na huku umezaa nae?
 
Umri wa mtoto?,tafuta Sababu za maana Ili umchukue mtoto wako!,....unakumbuka MR SUGU alivyomchukua mwanawe kutoka kwa yule kicheche?,amka usiendelee kuwa mtumwa mkuu..
 
Anakwambia mtoto si wakwako kwanini usijaribu kupima DNA? Au huyo mtu wako hatokubali? Kama huna shaka mtoto ni wako basi endelea kumhudumia tu pamoja na vituko vyote kwasababu wakati "mnakutana" kabla ya huyo mtu wako kupata pregnancy ulikuwa una-enjoy sasa ni zamu yako kuona hekaheka.

Unajua haya mambo wanaume na sisi hatufikirii sawasawa, kwanini uzae tu na mtu unafahamu kabisa huyu SIMPENDI......bado hutumii contraceptives unatarajia nini? Au unataka kusema aaaah bahati mbaya tu?

Mkuu hapo inabidi uendelee kuhudumia tu hadi mtoto afikiashe 18 au 21. Mwenzako ameshakuwa single mother.....na unajua kasheshe wanazokutana nazo.....au vipi muoe kabisa muishi wote.
 
Habarini;

Nina tatizo moja kuna mdada nilizaa nae mtoto mmoja wa kiume kutokana na maisha nilimpangia pa kuishi na nikaa namhudumia mpaka sasa. Cha ajabu ukimpa pesa ya matumizi mfano elfu hamsini haipiti siku tatu imeisha, nikimwambia huanza kunitukana matusi na kudharau kazi yangu inayomtunza.

Siku hizi amemwita ndugu yake wa kike mmoja anakaa nae hapo nilipompangia, wana umri sawa ni matusi kila mda na amesema mtoto si wangu nisimjue na kule nisikanyage na wala nisimpigie simu na hahitaji chochote kutoka kwangu.

SASA TATIZO; niliwahi kumsitishia huduma kutokana na tabia zake za kunitukana na kusema nisimjue mtoto na nyinginezo, lakini cha ajabu akaja ofisini mpaka kwa bosi wangu eti mimi simtunzi tangu mimba jambo ambalo ni uongo, alishawawahi kwenda mpaka ustawi wa jamii nikiitwa yeye anatokomea mitini, yaani imekuwa ni usumbufu.

JE NIFANYEJE MAANA NIMESHAMCHOKA SANA!

Mchango wenu tafadhali.
Badili namba ya simu ili asiweze kukutukana. Akija ofisini waambie walinzi wamzuie kuingia... Ili mtoto wako asife njaa kutokana na kiburi chake, endelea kumtumia hizo elfu hamsini hamsini kupitia kibanda cha simu ili asijue namba yako mpya...
 
huyo binti kwanza atakuwa ana mtu mwingine anaye mpa kiburi na pia sio wa kuishi nae koz anataka akunyee kichwani na ushauri we kaa kimya na uachane nae na kama una huakika mtoto ni wa kwako basi hamna jinsi mchukue mtoto ukae nae umuache yeye kivyake
 
Pole sana mzee.
Kuwa na akili ni kitu kimoja, kuna na ufahamu ni kitu kingine, kuwa mjanja ni kitu kingine pia.
Uwezo ya kuviunganisha au kuvitumia hivyo ni kitu cha kipekee zaidi.

''Wisdom is the principal thing, therefore get wisdom; and with all thy getting get understanding'' Proverbs 4:7
 
Habarini;

Nina tatizo moja kuna mdada nilizaa nae mtoto mmoja wa kiume kutokana na maisha nilimpangia pa kuishi na nikaa namhudumia mpaka sasa. Cha ajabu ukimpa pesa ya matumizi mfano elfu hamsini haipiti siku tatu imeisha, nikimwambia huanza kunitukana matusi na kudharau kazi yangu inayomtunza.

Siku hizi amemwita ndugu yake wa kike mmoja anakaa nae hapo nilipompangia, wana umri sawa ni matusi kila mda na amesema mtoto si wangu nisimjue na kule nisikanyage na wala nisimpigie simu na hahitaji chochote kutoka kwangu.

SASA TATIZO; niliwahi kumsitishia huduma kutokana na tabia zake za kunitukana na kusema nisimjue mtoto na nyinginezo, lakini cha ajabu akaja ofisini mpaka kwa bosi wangu eti mimi simtunzi tangu mimba jambo ambalo ni uongo, alishawawahi kwenda mpaka ustawi wa jamii nikiitwa yeye anatokomea mitini, yaani imekuwa ni usumbufu.

JE NIFANYEJE MAANA NIMESHAMCHOKA SANA!

Mchango wenu tafadhali.
Huyo mwanamke mwehu,na atakupelekesha sana usipo jipanga,kama mtoto sio wako unamlea wa nini? nenda na wewe ustawi wa jamii ukaseme alivyokwambia kua mtoto sio wako na usonge mbele na maisha asikuchefue roho mda wote..
 
Kumbe tayari alishakupeleka ustawi wa jamii... Kesi yako rahisi sana, nawewe nenda huko huko..., ila uwe na proof ya kuonesha unamlipia pango na kumtumia hizo fedha pia ushahidi usio na shaka kuhusu yeye kukutusi
 
Back
Top Bottom