Mzalendo Pombe Magufuli asingempa VISA Mzambia kuwa CEO Yanga

Kusimamia sera, kuingia mikataba na wadhamini, kusimamia mapato kumemshinda Mtanzania ?

Huwezi kukuta Mchina wa Gwanzuu kaletwa na Visa UK kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Man U na Kiingereza hajui.

Au Mhindi wa Bombay awe imported kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa New York Yankees wakati kuna Wamarekani milioni 100 wanaweza kazi hiyo.

Never, ever!
Acheni hizo wabongo,think bigger,mwamvita Makamba ni boss mkubwa wa Vodacom south afrika.
Hizi ni biashara sio mali ya serikali,sio kwamba huyo mzambia amekuja kuwa waziri au mkurugenzi wa ttcl,kwa taarifa yenu nchi hii ioiishawahi kuwa na mwanasheria mkuu raia wa Ghana!!
Kinachotskiwa ni cv sio kulia Lia,hao ambao wangetaka hii nafasi alioxhukua mzambia,wekeni cv zenu hapa,
Hapa bongo,Kuna kampuni ya wazawa kabisa ina tender kubwa huko Kenya,na hakuna kampuni ya Kenya yenye uwezo huo,hii ya bongo ni sole provider,ikitokea kazi lazima wabongo waende hata kama ni kubadilisha mapazia tu,ndivyo zilivyo biashara.
Itokee ajira ya UN kutanisha wasomi wetu na wakenya,nani atashinda,jibu liko wazi!!kama Raisi wenu anakimbia UN anaenda kujificha Msumbiji kwenye halmashauri!!wakati Ruto anagonga interview tu,aljwzeera,ujerumani
 
hiyo kambale nyeusi ndiyo ilikua inatoa Visa kwa wageni??
Rais wa nchi ni bosi wa kila mtumishi wa umma na kila taasisi ya umma, alikuwa na mamlaka kisheria kusimamia Sera ya Uhamiaji.

Mtanzania asingeweza kupewa Ukurugenzi Mtendaji Mufurira Wonderers au Safaricom au Gor Mahia. Ndio akasema tutembee kifua mbele, tuache kujinyenyekeza kwa wageni.
 
Hiyo kambale isingeweza kuzuiya visa.

Alifuta visa za maafisa wa European Union, wafadhili wa bajeti ya nchi, akiwataka waondoke na ndege ya jioni hiyo hiyo sembuse Mkurugenzi Mzambia wa Yanga.

South Africa hawakubali Mtanzania kuishi kwa kukusanya makopo ya plastiki njiani sembuse uwe Mkurugenzi Mtendaji wa Orlando Pirates.

Lakini sisi tunakubali kila kitu na kila mtu.
 
Tanzania tunahitaji expatriate wa ki Zambia kuwa Mkurugenzi Mtendaji Yanga ?

Kama ambavyo alinyimwa Visa yule Mama wa Kikenya mwenye degree ya cookery kuja kuongoza VODACOM ndivyo hivyo ilibidi huyu Mzambia apigwe chini.

Haya, kaja kwenye mkutano wa utambulisho hajui Kiswahili, Maulidi Kitenge anampa maneno ya kuongea ya Kiswahili. Kwa hiyo mijadala ndani ya Yanga itakuwa inampita, kwa sababu Jangwani hakunaga mjadala wa Kingereza. Hakukuwa na haja.

Pombe Magufuli aliyewaambia Watanzania tembeeni kifua mbele anabiringika kaburini.
Kumbe kuna tofauti Kati ya Mada na Murder?
 
Back
Top Bottom