Unapoachia namba yako ya simu kwa jinis hii, fikiria sana madhara yake, Tunaamini kwa nchi kama Bongo ambayo japo Serikali kupitia Tume ya Mawasiliano (TACRA) inaratibu na kusimamia mawasiliano ikiwemo simu na hivi karibuni zoezi la kusajili simu na namba limekuwa likiendelea, ukiachia nia kuu ya kuzuia uhalifu (crime control) bado tunawasiwasi kubwa juu ya uwezo wa Serikali na vyombo vyake kulinda haki za wenye namba (right to privancy) hususan pale ambapo zoezi hili limekuwa likiendelea pasipo kuwa na na Sheria ya kulinda taarifa za wateja (Data Protection Law) kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea. Tutaamini vip Serikali itawajibika pale taarifa au mawasilino yatakapovyujishwa na watendaji wake au vyombo vya serikali vitakapohusika kufuatilia taarifa binafsi za watu muhimu kwa nia ya kuwabana nyendo zao. Kwa mfano, kwa nchi zenye Sheria ya kulinda taarifa (Data Protection) ni marufuku kwa watunza taarifa kutoa siri za mtu na pia sheria inatoa haki kwa mtu anaeathirika kwa taarifa zake binafsi (personal information) kuvujishwa kudai fidia. Kwa sasa wakati makampuni ya simu yanalazimika kusajili namba zetu, hatuna pia uhakika iwapo watendaji kwenye makampuni ya simu hawatatumia vibaya taarifa zetu binafsi.