My opinion: Je serikali ya CCM iko serious kweli au ni kiini macho tu

Wlly,
Mkuu nadhani huifahamu vizuri CCM ya sasa hivi na jinsi watu walivyobadilika. Ondoa kabisa mawazo ya kwamba kina Lowassa, Chenge na Rostam wataondolewa hata kamam utakuwa na mawasiliano moja kwa moja na JK. Hili haliwezekani na CC hawawezi kukiweka chama ktk vita ya ndani. Kumbuka tu kwamba EL alijiuzuru Uwaziri mkuu kukinusuru chama na hakika wahusika wote ni pamoja na Rostam, Chenge na JK mwenyewe.

Sisi wote tulifurahia sana pindi JK alipoingia madarakani kutokana na ahadi zake, lakini kumbuka pia ni wewe mwenyewe uliyetutahadhalisha na mtandao jinsi walivyotumia nguvu ya fedha kuingia madarakani. Binafsi sikuamini na ilinichukua muda sana kuamini maelezo ya mkuu wangu wa ukweli ikiwa ni pamoja na yule Mzee Es...

Hakuna kilichobadilika na hakuna matumaini tena ndani ya CCM na ndio maana nilijiunga Upinzani sii kwa sababu nyingine zaidi ya kuelewa kwamba Utawala wowote unaoingia kwa nguvu ya fedha hasa za wafadhili iwe wa ndani au nje matokeo yake ni kuwafanya wananchi ambao ndio serikali kuwa watumwa wa wafadhili hao..Hii ndio CCM ambayo unatafuta kiongozi bora atokee wakati ushindi haupatikanai isipokuwa kwa kutumia fedha.

NNauye mshikaji, bwana mdogo ambaye kapachikwa wadhifa huu makusudi baada ya kupigwa vita kule vijana wa CCM na ni ktk kujaribu kukijenga chama upya kutokana na migogoro ndani kwa ulipatanisho wa Mzee Ruksa na Kinana. Hivyo chama bado kabisa hakijaweza kupona donda la uhasama ndani kinahitaji recovery period. Kusimika kisu ktk donda la Ufisadi ati kwa kujivua magamba ni hadithi za Abunuasi..

Upatanisho wa kamati ya Mzee Mwinyi haukuwa na mshindi, hivyo kuwaondoa Mapacha ni kuwapa ushindi kundi pinzani jambo ambalo haliwezekana kabisa kutokana na kuwa JK mwenyewe ni kundi la mtandao. Na kama Lowassa alivyosema Urafiki wao haukuanza jana, Sasa wewe nambie boyza to Men walianza lini ilihali Mwalimu alimwita Lowassa fisadi na JK hajakomaa kisiasa...

Ifike wakati tukubali matokeo mkuu wangu, huwezi kuibadilisha CCM kwa siasa za kiitikadi ikiwa watu wamepania kutajirika. Utajiri hauna mfumo wala Elimu bali ni tamaa ambayo haiwezi pukutika isipokuwa kwa sheria kuwabana na bahati mbaya sheria wameikalia wenyewe.
 
- Nilitegeema utawataja kwa majina hao wagomeba wenye uwezo wa kuishinda CCM, kutoka huko Chadema, badala yake naona zile zile ngonjera za bila Facts, unasema ni wazungu gani hao ambao hawakuamini kwamba Obama hawezi kua Rais, wakati ni hao hao Wazungu waliomsaidia kua Rais? Unasema Teddy Kennedy alimsaidia Obama huku akiwa haaamini kwamba anaweza kushinda? Tafuta kitabu mkuu kinaitwa Game Change, uelewe jinsi wazungu walivyokuwa wanamsaidia Obama!

- Hoja zingine bwana! Duh! halafu unasema haya yako ndio mawazo ya kisasa! ha! ha! ha!

William @ NYC, USA.

Dr. W. Slaa alitajwa miezi michache tu kabla ya uchaguzi. hakuna aliyetegemea kwamba angeweza kuitoa kamasi CCM. na kwa kweli taarifa kadhaa independent zina wasiwasi na matokeo ya uchaguzi wa 2010. kwa hiyo vyama vingine havilazimiki kufuata model hiyo ya kumtaja mgombea mapema. hata CCM kwenyewe historia inaonesha tofauti. wengi wanaamini Salim A. Salim ndio alikuwa ameandaliwa kumrithi Nyerere 1985 lakini mambo yakawa tofauti. wengi walimtarajia mzee Malecela 1995 lakini mambo yakawa tofauti. JK naye alijiandaa na kutumia nguvu nyingi sana na hatimaye ameingia madarakani akiwa na makundi yake ambayo yanaendelea kumsumbua mpaka sasa second term. hakuna aliyemtarajia Mkapa, lakini ndio akaja kuwa Rais.

Huko CCM wananyukana vilivyo. wale wanaojitokeza wanagongwa nyundo kichwani. anyway, kitakachodetermine rais ajaye wa nchi hii wala sio umaarufu wake. kumbuka Kikwete alikuwa maarufu sana 2005, lakini amekuwa rejected 2010 (ama kwa lower votes ama kwa cooked votes) Determinant ya kwanza ni hasira ya watanzania kwa CCM. kama CCM itaendelea kula mtaji wake kama inavyofanya sasa hivi, watanzania watatafuta mtu mwingine wa kuwaongoza na sio CCM. na kumbuka watanzania wa leo sio wale wa enzi zile. hawa wanafanya kweli. Pili ni kama CCM itakuwa muungwana wa kutosha kukubali kushindwa. hii ni determinant kubwa sana. so far inaonesha CCM iko tayari kutumia ma F-16 yake, ma-Tomahawk yake, ma-cruise missile yake - the full arsenal, kumsambaratisha yeyote atakayejitokeza kuitishia "mkate wake". lakini kauli ya wananchi ndio ya mwisho na kama CCM watatuepusha na vurugu kwa kukubali kushindwa
 
- Serikali ya Tanzania kwa sasa inaongozwa na kutengenezwa na CCM, kama vile Serikali ya Democrats kule US ilivyomuuua Osama ndivyo wanavyojinadi kwenye kutafuta kura za uongozi na ndio ukweli wenyewe, unajua JF tuna kaazi sana ya kuelemisha jamii!, I mean hata haya mambo madogo hivi!

William @ NYC, USA.

Robert Gates (Secretary of Defence) is a GOP and not a Democrat!
 
William unajua unachokisema hakina ukweli wowote CCM haina dhati yeyote ya kupambana na uhalifu halafu wala kuwaletea maendeleo Watanzania kuwa muangalifu Watanzania sio wajinga kiasi unacho fikiri sitaki kwenda into details kukujibu sababu nafikiri you can read between the lines jiepushe na uzuzu ulitufikisha hapa tulipo tuangalie namna ya kuanza kujenga Tanzania mpya tumia akili na uwelewa wako vizuri kuleta mchango chanya vichwani mwa Watanzania na sio kupandikiza fikra za kitwana kwa Watanzania.

@ Facebook: by William Malecela on Tuesday, June 7, 2011 at 8:36pm

@ NEW YORK CITY-US: Hongera sana Serikali ya CCM kwamba kwa mara ya Tatu toka tupate Uhuru, imeonyesha kuwa ikiamua inaweza kusimamia Sheria bila kujali inamgusa mwananchi au kiongozi wa taifa. Ninasema kwa mara ya Tatu kwa sababu mara ya kwanza ilianza na Balozi Mahalu, halafu Mawaziri Wake Yona na Mramba, na safari hii Mwenyekiti wa Chadema. Kama kawaida siku zote the end of hizi National Legal dramas huwa ni open for debate, na hasa iwapo the end justifies the means, lakini angalau hata kidogo kuliko kutokuwepo kabisaa! Ninasema hivi, kusimamia Sheria za Jamhuri ni lazima kuwepo na gharama na sisi wananchi walipa kodi lazima tuwe tayari kulipia gharama za Serikali yetu kusimamia Katiba ya Jamhuri, ambayo Viongozi wetu wa taifa hukubali kwa kiapo cha vitabu vyetu vitakatifu kwamba bora wafe, kuliko kuona Sheria za Jamhuri zinavunjwa!

- HOWEVER: Serikali ya CCM ifike mahali sasa isituchukulie sisi wananchi kama ni wendawazimu au walevi walevi flani hivi, ambao tunaweza kudanganyika kirahisi sana na viini macho. I mean huu mwendo wa kasi sana uliotumika katika kusimamia Sheria kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwa nini isitumike na kwenye kesi zingine ambazo ushahidi wake wa maovu against sisi wananchi, na kwa Sheria za Jamhuri yetu upo wazi kabisa! I mean upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Ufisadi wa Radar na BAE, tunajua kwamba upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Richmonduli, tunajua sana kwamba upo ushahidi wa wazi kuhusu Dowans na Kagoda, sasa kwa nini huku upande wa pili unaowahusu Viongozi wa CCM Serikali inasua sua na kuwa na makengeza? Hivi ni kweli Serikali ya CCM inaweza kwa macho makavu sana na uso kwa uso kutuambia wananchi kwamba Farijala na Maranda tu ndio waliochota hela za EPA? Yaani kazi yote ile na gharama za kamati ya Mwakyembe na Richimonduli mpaka leo kwa nini hakuna kiongozi hata mmoja aliyefikishwa kwenye Sheria? Kumbe Serikali ya CCM ikitaka kusimamia Sheria inaweza kutumia hata midege ya Jeshi ambayo tafsiri yake inaweza kuwa Amiri Mkuu Wa Majeshi yetu ndiye Chief Of Our Law Enforcement, kwa hiyo mkono wa kushoto kuusaidia wa kulia sio dhambi, Bravo for that lakini vipi wahalifu sugu huko ndani ya CCM?

- I mean we are taking Serikali ya CCM at its words kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwamba iko serious na kusimamia Sheria za Jamhuri, So! tunasema hivi Charity begins at home sasa ni wakati wa Serikali ya CCM kutuhakikishia wananchi kwamba katika kusimamia Sheria za Jamhuri, hakuna aliye juu yake kwa kuwafikisha kwenye Sheria Viongozi wake wengi wanaotuhumiwa kuvunja Sheria ile ile iliyovunjwa na Mwenyekiti wa Chadema, mpaka kumbeba na Midege ya Jeshi letu ili akaridhie Sheria Arusha, sasa hii Midege iwabebe na wanaohusika na Radar & BAE, Richmonduli, IPTL, Dowans, Kagoda, EPA, Deep Green, Meremeta, Anabem, Kiwira, ATC na wao tuone wakibebwa na midege ya Jeshi kwenda kwenye Sheria za Jamhuri!: Tunasema hivi sisi wananchi wa Tanzania sio mabwege tena!

Well, People Good Night!

William Malecela @ New York City, USA.
 
William, Mdogo wangu mimi ninaswali "Hivi ni lini mara ya mwisho ulikuwa hapa bongo?" inaelekea ni long time. Na hata ukija basi maongezi yako ni Sea Criff, Holiday Inn, Mlimani City n.k. Maongezi yako na akina kasesela, Nape, na makada wenzio. Nenda vijiweni bwana ndio utapima jta halisi la siasa TZ mzee, Nakuthibitishia kuwa hujui hali ya kisiasa imekaaje hasa kwa upande wa MAGAMBA. Sio siri safari hii kama haitapatikana katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa ya kisiasa na kijamii basi CCM itashinda lakini hawatatawala. Lakini katiba mpya ikipatikana, inayo kidhi mahitaji ya sasa ya kisiasa na kijamii basi ujue CCM ndio kwaheri.

Usijipe moyo sana ndugu yangu haijawahi tokea chama cha kisiasa cha upinzani kikawa maarufu katika rika zote za watanzania kama CHADEMA labda TANU during sixies. Mimi shughuli zangu zinanifanya nitembee sana mikoani CHADEMA iko juu, Uchaguzi wa 2015 issue haitakuwa mgombe, bali chama cha mafisadi na CHADEMA. Najua utakataa lakini hii ndio hali halisi. Kwasababu ndio kawaida yako kukataa hata kama kweli, jana nilikuambia kitendo cha kumkamata Mbowe kimemuongezea umaarufu ulinibishia. Sasa sijui umeona jinsi alivyo shangiliwa wakati anaingia bungeni, mkuu bunge lilizizima na makofi na kushangiliwa akiitwa Mandela, Mandela!!! mpaka wabunge wa magamba wamemshangilia. Kalaga baho!!!!
 
Zumbemkuu....

Si kweli kwamba CCM wamelinda sheria mara tatu tu, ni ile ufupi wa kumbukumbu na uelewa wa William, na sometimes ni mtu wa kudandia mada nakuleta kama inititator, so expects lots of similar "shody" analyses from William

Nevertheless, CCM ya JK is the weakest CCM in history and unfortunately wanavuana nguo wenyewe kwa wenyewe kama wake wenza!!

Mkuu MTM, hapo kwenye red ingesomeka fortunately siku yangu ingekuwa poa zaidi....
 
@ Facebook: by William Malecela on Tuesday, June 7, 2011 at 8:36pm

".......................................

- HOWEVER: Serikali ya CCM ifike mahali sasa isituchukulie sisi wananchi kama ni wendawazimu au walevi walevi flani hivi, ambao tunaweza kudanganyika kirahisi sana na viini macho. I mean huu mwendo wa kasi sana uliotumika katika kusimamia Sheria kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwa nini isitumike na kwenye kesi zingine ambazo ushahidi wake wa maovu against sisi wananchi, na kwa Sheria za Jamhuri yetu upo wazi kabisa! I mean upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Ufisadi wa Radar na BAE, tunajua kwamba upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Richmonduli, tunajua sana kwamba upo ushahidi wa wazi kuhusu Dowans na Kagoda, sasa kwa nini huku upande wa pili unaowahusu Viongozi wa CCM Serikali inasua sua na kuwa na makengeza? Hivi ni kweli Serikali ya CCM inaweza kwa macho makavu sana na uso kwa uso kutuambia wananchi kwamba Farijala na Maranda tu ndio waliochota hela za EPA? Yaani kazi yote ile na gharama za kamati ya Mwakyembe na Richimonduli mpaka leo kwa nini hakuna kiongozi hata mmoja aliyefikishwa kwenye Sheria? Kumbe Serikali ya CCM ikitaka kusimamia Sheria inaweza kutumia hata midege ya Jeshi ambayo tafsiri yake inaweza kuwa Amiri Mkuu Wa Majeshi yetu ndiye Chief Of Our Law Enforcement, kwa hiyo mkono wa kushoto kuusaidia wa kulia sio dhambi, Bravo for that lakini vipi wahalifu sugu huko ndani ya CCM?

- I mean we are taking Serikali ya CCM at its words kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwamba iko serious na kusimamia Sheria za Jamhuri, So! tunasema hivi Charity begins at home sasa ni wakati wa Serikali ya CCM kutuhakikishia wananchi kwamba katika kusimamia Sheria za Jamhuri, hakuna aliye juu yake kwa kuwafikisha kwenye Sheria Viongozi wake wengi wanaotuhumiwa kuvunja Sheria ile ile iliyovunjwa na Mwenyekiti wa Chadema, mpaka kumbeba na Midege ya Jeshi letu ili akaridhie Sheria Arusha, sasa hii Midege iwabebe na wanaohusika na Radar & BAE, Richmonduli, IPTL, Dowans, Kagoda, EPA, Deep Green, Meremeta, Anabem, Kiwira, ATC na wao tuone wakibebwa na midege ya Jeshi kwenda kwenye Sheria za Jamhuri!: Tunasema hivi sisi wananchi wa Tanzania sio mabwege tena!

..........................................

William Malecela @ New York City, USA.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

William, kwa hizo paragraphs mbili hapo juu niko nawe kwa asilimia 100. Mwenye macho na aone, na mwenye masikio asikie.

Na tatizo ni kuwa hata tukisema na kuwaambia hao wakulu, basi inaonekana ama unatetea upinzani au unatetea kundi mojawapo ndani ya makundi ya CCM. Wao kuangalia kwa msingi wa sheria za nchi, hawalioni kabisa hilo.
 
Haaaa ha ha Mzee wa US naona CCM mnajitahidi kuwatafutia CDM mgombea urais.haa ha ha je CDM wataingia kwenye mtego wenu? na kwenu ccm chaguo lenu ni zito ha ha mnachekesha sana na karibu CCM wote humu jf kwao zito ndiyo chaguo lao? naogopa isije ikawa adui yako muombee njaa.
Kazi kwenu CDM mkimteua zito ccm watampigia kura!
 
duh! W.J Malecela anapangilia hoja kama FaizaFoxy!! Huu ndio ujasiri wa mwendawazimu aliokuwa anasema Ndimara!!
 
@ Facebook: by William Malecela on Tuesday, June 7, 2011 at 8:36pm

@ NEW YORK CITY-US: Hongera sana Serikali ya CCM kwamba kwa mara ya Tatu toka tupate Uhuru, imeonyesha kuwa ikiamua inaweza kusimamia Sheria bila kujali inamgusa mwananchi au kiongozi wa taifa. Ninasema kwa mara ya Tatu kwa sababu mara ya kwanza ilianza na Balozi Mahalu, halafu Mawaziri Wake Yona na Mramba, na safari hii Mwenyekiti wa Chadema. Kama kawaida siku zote the end of hizi National Legal dramas huwa ni open for debate, na hasa iwapo the end justifies the means, lakini angalau hata kidogo kuliko kutokuwepo kabisaa! Ninasema hivi, kusimamia Sheria za Jamhuri ni lazima kuwepo na gharama na sisi wananchi walipa kodi lazima tuwe tayari kulipia gharama za Serikali yetu kusimamia Katiba ya Jamhuri, ambayo Viongozi wetu wa taifa hukubali kwa kiapo cha vitabu vyetu vitakatifu kwamba bora wafe, kuliko kuona Sheria za Jamhuri zinavunjwa!

- HOWEVER: Serikali ya CCM ifike mahali sasa isituchukulie sisi wananchi kama ni wendawazimu au walevi walevi flani hivi, ambao tunaweza kudanganyika kirahisi sana na viini macho. I mean huu mwendo wa kasi sana uliotumika katika kusimamia Sheria kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwa nini isitumike na kwenye kesi zingine ambazo ushahidi wake wa maovu against sisi wananchi, na kwa Sheria za Jamhuri yetu upo wazi kabisa! I mean upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Ufisadi wa Radar na BAE, tunajua kwamba upo ushahidi wa kutosha sana kuhusu Richmonduli, tunajua sana kwamba upo ushahidi wa wazi kuhusu Dowans na Kagoda, sasa kwa nini huku upande wa pili unaowahusu Viongozi wa CCM Serikali inasua sua na kuwa na makengeza? Hivi ni kweli Serikali ya CCM inaweza kwa macho makavu sana na uso kwa uso kutuambia wananchi kwamba Farijala na Maranda tu ndio waliochota hela za EPA? Yaani kazi yote ile na gharama za kamati ya Mwakyembe na Richimonduli mpaka leo kwa nini hakuna kiongozi hata mmoja aliyefikishwa kwenye Sheria? Kumbe Serikali ya CCM ikitaka kusimamia Sheria inaweza kutumia hata midege ya Jeshi ambayo tafsiri yake inaweza kuwa Amiri Mkuu Wa Majeshi yetu ndiye Chief Of Our Law Enforcement, kwa hiyo mkono wa kushoto kuusaidia wa kulia sio dhambi, Bravo for that lakini vipi wahalifu sugu huko ndani ya CCM?

- I mean we are taking Serikali ya CCM at its words kwenye ishu ya Mwenyekiti wa Chadema, kwamba iko serious na kusimamia Sheria za Jamhuri, So! tunasema hivi Charity begins at home sasa ni wakati wa Serikali ya CCM kutuhakikishia wananchi kwamba katika kusimamia Sheria za Jamhuri, hakuna aliye juu yake kwa kuwafikisha kwenye Sheria Viongozi wake wengi wanaotuhumiwa kuvunja Sheria ile ile iliyovunjwa na Mwenyekiti wa Chadema, mpaka kumbeba na Midege ya Jeshi letu ili akaridhie Sheria Arusha, sasa hii Midege iwabebe na wanaohusika na Radar & BAE, Richmonduli, IPTL, Dowans, Kagoda, EPA, Deep Green, Meremeta, Anabem, Kiwira, ATC na wao tuone wakibebwa na midege ya Jeshi kwenda kwenye Sheria za Jamhuri!: Tunasema hivi sisi wananchi wa Tanzania sio mabwege tena!

Well, People Good Night!

William Malecela @ New York City, USA.

Well said Mkulu.....once again.........heshima mbele.......

Inatia shaka sana kuona baadhi ya watu tunaoamini kuwa.......pengine watakuja kuwa viongozi wa nchi hii.......wanakuwa not only hawafuati sheria...........but also........wanasupport sheria mbovu mbovu............Nilitegemea mtu mwenye nia ya kuwa kiongozi anatakiwa awe mfano mzuri kwakila hali.....ikiwa na pamoja na kufuata sheria..............Yes kunaweza kuwa na shortfall kwneye utekelezaji wa sheria katika sehemu mbali mbali lakini hali haitupi free pass kufanya mambo the way we feel like..........NO WAY

Siasa zingine ni za kijinga sana.........na hii inaonyesha ni jinsi gani....potentially watu wanaweza kuja ku-undermine sheria na ku-insinuate watu/wananchi wafanye/lete ushabiki..........ili wawe popular.............Nilisema na ninarudia.......misingi ya sheria yeyote ni KULINDA na wala si vinginevyo.............kama kuna sheria ambayo haiko katika mtizamo huo......basi ina kasoro...........

Right on Time Billy!!............Fimbo hii hii waliyoitumia CCM yenu.......inabidi tuwakome nao Giladi mchana kweupe kwenye scandals walizonazo (kama ulivyoainisha).....well done!
 
- Mbowe na Chadema bado hawajafikia kuwa tishio kwa CCM kuwa kwenye power, na it has nothing to do na Mbowe kushindwa kufika mahakamani alikowekewa dhamana, kama kweli CCM inataka kumu-eliminate Mbowe sidhani kama inahitaji kusubiri ashidnwe kwenda kwenye kesi yake Arusha halafu ikamuachia,

- Mbowe hawezi kugombea Urais tena, na Chadema wana tatizo kubwa sana hapo 2015, unless atokee a strong candidate from CCM, Zitto anaweeza kututikisa sana, lakini that is all unless CCM tujimalize wenyewe kama kawaida yetu!

William @ NYC, USA.
Hivi CCM mtajimaliza mara ngapi? Na hii dhana kwamba Mbowe hawezi kugombea urais inatokana na kanuni gani? Just wondering!
 
- Mkuu hivi nilisema Tarehe mbona inakusumbua sana vipi si unaweza kuanzisha tawi la Chadema! ha! ha! mkuu this wekend tunakutana tena kuanzisha tawi majuu sio mchezo so soon linakuja usiwe na wasi wasi, na karibu sana!

William @ NYC, USA.

Sipo huko majuu jamaa yangu, nipo huku Mchichira nakula ming'oko kwa kwenda mbele, huku kwetu CHADEMA ni wachache sana. Huku CUF ndio wenyewe. Mie nilidhani ulikusudia kufungua tawi majuu kwakuwa CCM wanajivua gamba na kuleta matumaini mapya na kwakuwa sasa umegundua kwamba walisahau kuvua gamba la matumizi mabaya ya dola ungefikiria upya mpango wako. Lakini kwakuwa kila anayekuuliza swali kuhusu adhima yako unamdhania ni mwanaCHADEMA mie naufyata sitachangia thread yako tena.
 
- CCM ina alternatives nyingi sana za wagombea wa Urais, kuliko huko upande wa pili Magufuli, Mwandosya, Membe, Sitta, Mwakyembe, hawana wapinzani!

William @ NYC, USA.

Are u serious mkuu? Jaribuni kuweka mmojawapo utaona matokeo. Tatizo ni kwamba uko mbali sana na hujaziona Siasa za Tanzania zilivyobadilika.
 
hao waliokufuata walikuwa influenced na post za hapa ndani, swali ni je hizi post ziko influence na chadema?
jibu liko wazi ni no?
hao wana akili za kimagamba kama walitaka kujua umiliki wa jamii forum walitakiwa kupata ushahidi wa umiliki? nimesikia una share kiasi hapa lakini sio kufikia hatua wewe kuongea pumba zako hapa kwenye forum, hacha mambo ya kitwana una ishusha hadhi forum yakwamba wewe ndiye unaweza kusema nini kina endelea hapa ndani na nani mmiliki wa hii forum?
ina maana wewe ulinunua share kwa ajili ya kufanya umagamba hapa ndani watu wakunyamazie kisa utawambia kwamba utawambia waandishi wa habari inamilikiwa na chadema.
zama za kutishana zimepitwa na wakati kama umefanya kitu kizuri katika jamii isiwe blackmail katika jamii.
sometime u need to shut up man

- Mkuu nimekusoma naona una tatizo kubwa sana kuliko unayoyasema! ha! ha! lakini naomba kukukaribisha sana, karibu ninakuosma sana between the lines kwamba una tatizo kubwa sana, ni vyema ukalisema kuliko kuzunguka zunguka! ha! ha! ha!, Umenivunja mbaavu sana na majungu majungu! ha! ha! ha!

William @ NYC, USA.
 
William mbona kana kwamba uraia wako wa Tanzania uliupata kwa kuomba? Majibu ya maswali yote unayo na unayajua, sheria tunazo zipo vitabuni labda jaribu kuwakumbusha wawe wanazisoma kidogo, kama tungekuwa na utawala wa kisheria kashfa zote hizi zinazojitokeza zingekuwapo. CCM haina cha kujinadi kwa wananchi wanachotakiwa ni kujaribu kuondoa kero zinazowakabili watanzania. UTAJINADI VIPI WAKATI MWILI MZIMA UMEJIPAKA MAVI? Mwenyekiti analijua hili fika ndio maana hawezi kufanya mkutano wa hadhara, kimsingi alipaswa kufanya angalau mkutano mmoja wa hadhara si kushinda bali kuwashukuru wanaccm waliompigia kura. Kilichobaki ni kumtuma mtu punguani kama NAPE kufanya mikutano ya hadhara mwenye akili timamu hawezi kusimama mbele ya watanzania kuinadi CCM katika kipindi kama hiki. Kazi ni kubwa kinachotakiwa ni viongozi wetu kuwa wakwel ili kurudisha imani.

Chama
Gongo la Mboto DSM.

- Nonsense!

William @ NYC, USA.
 
wacha bwana! ivi unajua kuwa Osama aliyekuwa kwenye sera ya Obama wakati anagombania urais? Pili, unajua ugaidi ni vita...aka 'war on terror'? Kwenye vita ni nani anachukua credit ya ushindi? Si jemedari mkuu. Kwenye ishu ya Osama, who gave the go ahead on the mission? Si jemedari mkuu aka Obama. Why should he not take credit? Tofautisha Jeshi katika vita na polisi katika kutunza sheria za nchi. Wewe umesoma shule gani mkuu? Mbona unaonekana kama vile huko shule ulikuwa unapitishwa tu? Jeshi na polisi ni vitu tofauti na havifanyi kazi moja. Jifunze hilo kwanza!!! Ndio maana mafunzo yao ni tofauti kabisa. Wewe leo Polisi Marekani wakimkamata Bush kwa wizi tuseme kwenye supermarket, Obama atasifiwa? embu fikiria hilo kwanza. Polisi ni CIVIL SERVANTS. They have/should not have political interest. Kauli yako inaonyesha jinsi gani nyie ccm mlivyoharibu hii nchi. Na inafanya kauli za viongozi wa Chadema waliosema kuwa Polisi wanaupendeleo wa chama kuwa kweli. Huoni kuwa hilo sio sahihi? Jifunze URAIA aise ndugu yangu. Unatia aibu sana!

- Mkuu wa Polisi wa Tanzania, anachukua amri toka kwa Waziri wa Ndani, ambaye ni Mbunge wa CCM aliyechaguliwa na Rais wa ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, Mwenyekiti wa Chadema hawezi kukamatwa bila hao wawili kujua in advance na pia hata kutoa their input, kama ulikuwa hujui haya basi ndio maana hapa JF hatuelewani, ni very simply National Politics ambazo hata mtoto wa Shule ya Vidudu anatakiwa kujua, kwamba sio bongo ni siasa za Dunia nzima! UNDERSTAND!

wIlliam @ NYC, USA.
 
Zumbemkuu....

Si kweli kwamba CCM wamelinda sheria mara tatu tu, ni ile ufupi wa kumbukumbu na uelewa wa William, na sometimes ni mtu wa kudandia mada nakuleta kama inititator, so expects lots of similar "shody" analyses from William

Nevertheless, CCM ya JK is the weakest CCM in history and unfortunately wanavuana nguo wenyewe kwa wenyewe kama wake wenza!!

- Serikali ya CCM imesimamia only Three National high profile cases toka awamu ya nne ishike power, huhitaji kuwa na PhD kuelewa nilichokisema kwenye article yangu, ndio maana mara nyingi sana hapa tunasema hivi mpumbavu siku zote hwua ni rahisi sana kujisema upumbavu wake tena bila kujijua, huku akidai wengine ndio, kumbe ni yeye mwenyewe akijivua nguo kwa maneno yake! ha! ha! ah! ha!

William @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom