My Man is a workaholic

My Man is a workaholic

badiebey

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Posts
5,875
Reaction score
3,117
Za jioni wakuu

Naomba ushauri, kichwa cha habari chahusika, What can I do to interest him outside work, he works like everyday, morning to late evenings, Napenda sana bidii yake kama mwanaume mana kwa kiasi kikubwa inampa heshima .

Na ananiweka mjini, lakini namuonea huruma pia anavyochoka jamani with work in his mind kila saa, nampenda sana maana everything between us works well in good and bad times, sitaki kumbadilisha my partner ila napenda aenjoy pia activities out of work zaidi.

Karibu kwa ushauri
 
BintiiiWee anakujengea Mustakabal SunRiser !! Hongera..... watu wanatafuta wa hivyo!!
 
First, find new ways of titivating yourself.

Second, once he notices the differences he will be titillated.

Third, after he's titillated the job of getting him to pick up other interests becomes easier.

Fourth, tell him that he should be working to live and not live to work.

Fifth, adopt the motto 'work hard and play even harder'.
 
Usije lalamika tu hizo activities za nje zikimkolea
 
Jifunze kidogo kuhusu kazi yake
na wajue watu anao fanya nao kazi
ili uweze kumsaidia kwenye decision making....

ili muweze kuwa na kuongea ..ataweza kukushirikisha
mfano annaweza kukupa story ya watu wa ofisin
ukiwa unawajua japo sura utaweza say something kwa jinsi ulivyowasoma sura zao tu

au kama kuna decision inamsumbua kichwa unaweza ongea kitu

that way akiona unajua something utaweza kumshawishi kupunguza masuala ya kazi

sio sifa kuwa workaholic Tanzania hasa kama umeajiriwa...
workaholic nzuri ni ya kujiajiri
 
First, find new ways of titivating yourself.

Second, once he notices the difference he will be titillated.

Third, after he's titillated the job of getting him to pick other interests becomes easier.
Nini hio misamiatii sasaa sijaelewa titivate/late
 
NN hio misamiatii sasaa cjaelewa titivate/late

Yes, you titivate yourself in order to titillate him.

Once he's titillated, it's much easier to get him to go for a drink at a martini bar or some other place like that.
 
Jifunze kidogo kuhusu kazi yake
na wajue watu anao fanya nao kazi
ili uweze kumsaidia kwenye decision making....

ili muweze kuwa na kuongea ..ataweza kukushirikisha
mfano annaweza kukupa story ya watu wa ofisin
ukiwa unawajua japo sura utaweza say something kwa jinsi ulivyowasoma sura zao tu

au kama kuna decision inamsumbua kichwa unaweza ongea kitu

that way akiona unajua something utaweza kumshawishi kupunguza masuala ya kazi

sio sifa kuwa workaholic Tanzania hasa kama umeajiriwa...
workaholic nzuri ni ya kujiajiri

Thanks Bossman,nimepata kitu indeed
 
Yes, you titivate yourself in order to titillate him.

Once he's titillated, it's much easier to get him to go for a drink at a martini bar or some other place like that.

Okay dictionary imehusika,will do all kinds of titivation possible to titillate him
 
najua and am happy kwa kweli,lakini naamini ni muhimu kubalance
Nakusihii karne hii usichokoze mwendo huo...bora wewe uchukuwe Love,Dovie zako hadi kazini kwake maana usisubiri aje yeye!!
take the war to thr land" au peleka Bustani kwake !!uwiiii....
 
Invisible na Moderator michezo ya kubadilisha maneno kwenye uzi wangu sitakiiiii,mngetaka personalized topics msingeweka Jf as a public forum
Sijapendaaa ,muurudishe ulivokua na muuacheee
 
Last edited by a moderator:
Kama vipi achana nae maisha yenyewe mafupi yeye yupo busy hata kufaidi hafaidi
 
Pamoja na kuwa interested na kazi zake, jaribu kumuiba mara kwa mara. Mfano msapraizi na kidate cha dinner. Mfuate ofcn muambie twende mahali kuna bendi ama dinner, ama hata star gazing. Get a together hobby kama swimming ama gym once a week.
 
My own story

I once was a workaholic....Awali kabla ya kuoa nilikuwa natoka kazini kati ya saa 1:30 mpaka saa 3:00usiku wakati wafanyakazi wenzangu wote saa 11:00jioni huwa wameshaondoka kazini. Kwangu haikuwa shida and I was happy na hasa watu walipokuwa wakiniita "Jembe" kwa kule kujituma Saana kazini

Baada ya kuoa some first few months niliweza kujimudu kuwahi kurudi mapema lakini after some six months nikarejea ada yangu.

Hii ilienda kwa muda mrefu na wakati fulani nilikuwa naonyesha kuchapa kazi na mke ajivune kuwa na mume responsible ambae anachapa kazi na anamudu kuendesha family

Hali hii ilipozidi mke wangu ikamshinda na siku moja akaniambia angependa nimpeleke Korogwe Tanga akamsalibie Bibi Mzaa mama yangu. Japo ilikuwa ngumu kwangu lakini sikuataka kumuangusha nikachukua 2 off days na zilikuwa Alhamisi na Ijumaa na Jumatatu yake ilikuwa sikukuu ya Mwalimu Nyerere (October 2013) hivyo tukawa na muda wa kutosha

Tulitoka Moro tukafikia HighWay Hotel (Dar Express) na jioni hiyo wife akaniambia ni kweli amekuja Korogwe kusalimia lakini kuna jambo la muhimu angependa tuzungumze.

Hapo ndipo alipoonesha hisia zake. Alinisaidia kufahamu namna ambavyo anafurahia kuwa na mume responsible na ambae anatunza family yake vizuri....wanapata kila wanachohitaji

Lakini pia akanisaidia kujua anavyoumia kuniona nikijiumiza saana kwa kufanya kazi kunakozidi. Alinisaidia kujua anavyoumia kihisia kuwa mpweke lakini wasiwasi wake kuwa Binti yetu Mdogo hapati wasaa wa kutosha na baba yake.

Baada ya hay a na mengine mengi ambayo siwezi Sema yote, wife akaniuliza juu ya kazi yangu na mapana yake. Kisha akauliza juu ya wafanyakazi wangu (waliochini yangu kiusimamizi) na wafanyakazi wenzangu (waliojuu yangu kiusimamizi au nilionao level/grade moja) na nani kati yao anaweza nisaidia lipi na lipi (Mke wangu ni mwalimu by profession so hapa kalamu na notebook vilikuwa karibu). Aliniuliza nani namwamini nani simwamini?. Je sio kweli najiumiza kwa kuwa siwaamini watu wanaweza fanya kazi nizifanyazo kwa ubora uleule? Kama wapo niwaaminio basi niwape kazi na kama hakuna niwaaminio basi je hakuna yeyote naweza m-coach akaweza kufanya yale nipaswayo kwa viwango vile vile Kama reports, weekly/monthly plans e.t.c.?

Baada ya yote akanisaidia kushirikisha majukumu na wenzangu (japo nilisoma delegation chuoni lakini sikuikumbuka) na akanisaidia kuweka ratiba na taratibu zangu za kazi ili zisiniumize wala zisiwe sababu Kuwa mbali na family yangu.

Kwa kweli that was a turning point. Maana baada ya yote haya tulikubaliana kuwa nitoke kazini muda wa mwajiri (mkataba) saa 11:00jioni otherwise kuwe na jambo ambalo linahitaji nichelewe kulimaliza (hali ya udharura) lakini pia nijifunze kujinidhamisha katika yote. Kisha tukaomba pamoja.

Toka wakati huo Lazima saa 12 niwe nimeshatoka ofisini isipokuwa katika mazingra machache ya siku zinazohesabika ambazo hujikuta nalazimika chelewa

My Advice
Mara nyingi hutukuta wengi hasa ambao by nature tunapenda kuonekana tunachapa kazi na tuko serious katika ku-deliver even beyond employer's expectetations tukisahau tuna jukumu LA ku-deliver pia expectations za wenza na familia zetu. Cha muhimu kusaidiana na kukumbushana....usimchukulie katika namna itakayomfanya aka-react vibaya...nenda nae slowly na kwa mpango mzuri (sio lazim Kama mbinu aliyotumia mke wangu) then msaidie Kama nilivyosaidiwa

Ahsante
 
Back
Top Bottom