JF kuna visa jamani, khaaa!!! Nilifikiri niko peke yangu.
Sasa wewe
gugu wataka kujidhuru wakati Wanaume tupo kibao kabisa hapa Sikonge tumejaa kama Chungu cha
Masangu au Makande, tena yale Makande ya Njugu mawe au Bambara Groundnuts.
Kama huyo hakutaki, wee njoo hapa Sikonge uunge tela na uwe Mke mwenza. Uzuri wangu ni kuwa najua kupenda sana tu na kujali familia nzima (Family Man).
Najua kwa wanawake au binadamu wanaokuwa Brainwashed inakuwa shida sana kubadili. Wanaume wakishaanza kutumia vitisho na Mwanamke akakubali kuwa manipulated, basi kwisha kazi yake kabisa. Jamaa anaweza kuwambia kanisubiri kwenye kiti pale ufukoni baharini na usiondoke, basi Mwanamke atakaa pale hata inyeshe mvua ya mawe.
Kuna dada mmoja nilishawahi kukutana naye, ana msuli mgumu kama wa Bondia. Kumbe kisa ni kuwa anacheza Martial Art. Sasa na yeye alikuwa kawekwa ndani na mumewe kwa miaka mingi pamoja na ukakamavu wake kwenye michezo. Tena dada mzuri kweli aisee na kajijazia mzigo mzuri tu kule Wanyamwezi tunapenda na Mtindi wa haja kwa ajili wa Wanaume wa Kidhungu. Ila bado aliwekwa kwenye kona hadi akawa Kondoo.
Siku moja akashindwa kuvumilia, akamuweka jamaa vitu vya uhakika kwa kutumia ujuzi wake. Sijui ilikuwa Karate au Kung-fu? Jamaa akaishia hospital kavunjwa vunjwa mifupa kadhaa. Dada wa watu akaishia kufungwa kifungo cha nje kwa kumpa kibano Binadamu mwenzake kupita kiasi ingawa na yeye alikuwa akibondwa sana tu ila hawezi kushtaki.
Muangalia Tina Turner na yeye alipata sana kipigo. Ila ikafika mwisho akajiondoa kwa mumewe na kuja kuwa Mwimbaji maarufu sana duniani. Nakumbuka concert yake ya mwisho, watu walisafiri kutoka kila kona ya dunia kuja kumuaga.
Kama uliweza kuhangaika na kuwa na Mabasi, basi anza upya na hangaika na utapata mengine mengi tu na mwisho Mwanaume atakayekupenda kwa dhati. Heri hata upate aliyeowa kama mie hapa kwani walau utajua umesimama wapi kuliko kudhani upo peke yako wakati mpo wengi. Sisi wanaume NDIVYO TULIVYO kwa bahati mbaya.
Nimemwambia
snowhite awe wifi yake wa tatu dada
FirstLady1 na
Kaunga ila bado anaringaringa anataka hawa vijana wanaovaa mitepesho. Mambo ni Wazee vijana bana kama Sikonge hapa. By the way, hivi huyu
FP kuna nini kinaendela juu yake maana huwa namuonaona hapa ila sijawahi kuongea naye hata siku moja.
Salaam Aleikum dada FP? Hahahaa nimejifunza kutoka kwa Lil Wayne......