Ukisoma comments za baadhi ya watu huko juu utaona kwamba walitegemea kabisa majibu ya ELISA yatolewe positive,hebu jiongeze kidogo kwenda mbali zaidi ya hapo,ingawa umejiuliza maswali mazuri sana ambayo pia unatakiwa ujue majibu yake...ATTENTION PLEASE: Majibu ya ELISA test yametoka, yanaonesha mpenzi wangu bado ni HIV+, see the attached crop screenshot.
Bahati mbaya tulienda jioni kidogo hatukuweza kuonana na daktari japo tuliomba majibu yetu na kupewa. Bado nina maswali mengi sana yasiyokuwa na majibu, ELISA inaonesha Reactive result (HIV+) while SD Bioline & Unigold vyote vinaonesha Non-Reactive results (HIV-).
Wataalamu wetu humuanzishia mtu yeyote dozi za ARV's pale tu Bioline test ikiwa reactive then wakathibitisha na Unigold test. Leo hii ukitaka kufunga ndoa na mkatakiwa kwenda kucheck afya....wataanza na SD Bioline test na kama majibu yakitoka non-reactive basi vyeti vyenu vitaandikwa nyie wote ni HIV-. Maana yangu ni kuwa kama ningekuwa sijui status ya mpenzi wangu na leo tumeenda kupima basi majibu yangetoka sote tu HIV-.
Kama SD bioline ikitoa reactive result basi watathibitisha kwa kutumia Unigold test na endapo majibu yakitoka non-reactive utaambiwa urudi tena baada ya miezi 3.
Ipo haja ya kudadisi zaidi hii kitu ili kujua mbivu/mbichi ni ipi!!! Bado nitaendelea kuwa na mpenzi wangu mbali na majibu ya ELISA kutu-disappoint kiaina.
Mjadala huu bado upo wazi mpaka mwisho wa dahari.View attachment 1144808
Huko nyuma kuliwahi kuwa na kesi kama hizi mahakamani watu wakidai haki zao kwa kudanganywa...kesi hizi zina madhara makubwa sana kwao kibiashara kama mfunguaji kesi atakua anajua sheria na haki zake...angalia hiyo video ya dada wa Uganda hapo juu...
Pia nimejaribu kufanya udadisi pengine kuna figisu imefanyika,...hebu fikiria kama majibu ya ELISA yangekuwa negative unadhani wangekuwa katika wakati gani kujibu au kulishughulikia suala la mkeo wakati tayari wameshampa ARVs kwa miaka 4?...
Hebu jiulize,Tanzania hakuna ELISA test?...ingawa najua figisu hata hapa yaweza kufanyika,ila waweza kufanya kwa siri pasipo kumwambia mtu yeyote...
All in all,haya yote nilishayazungumza huko nyuma,mtu amepimwa negative mara 3 lakini bado anaendelea kula ARVs,for what?...yaani hapa wanaona bora kupingana na miongozo yao ili wafiche ukweli kwenye suala la mkeo...