Haya nimeskia kilio chenu, bado nipo kwenye Team happiness wengine mnataka kuwasiliana na mie
Me napatikana whatsapp tu namba yangu +255688411043 usipige hiyo ni namba ya whatsapp tuu!
A.TEAM HAPPINESS
Hidaya amekaa zake barazani anakunywa chai saa 3 asubuhi anasikiliza redio wee baadae akanaliza chai ukapigwa mziki wa Pepekalee Hidayaaa! Akaanza kucheza huku amekaa anafurahi mwenyewe! Jina lake linaimbwa!
Mara akaingia ismail anamkuta Hidaya ameshasimama anacheza, wakaanza kucheza nae mpaka mziki umeisha wakakaa chini wanahema, mara Ismail akaona gari imepaki nje ya ofisi yake akakimbia mbio kumbe ni Patric!
Hidaya nae akaingia ndani akafunga milango yote na dirisha kubwa akaingia chumbani kwake ananasa king'amuzi.
Patric: nimekuja kuongea kuhusu ile evidence nataka niondoke nayo maana usiku nimeora kiza kinene kipo mbele yangu!
Ismail: mh! Mheshimiwa, ungeacha kwanza tuje tuivuruge huku huku usije enda nayo ukapatwa na matatizo bure!
Patric: hapana mzee acha me najua oa kuificha
Ismail: basi uje alhamisi tuichome hapo msitu wa kati, nimeificha huko
Patric: sawa hamna neno! Wakawa wanaongea mambo mengine Ismail akapewa mil 5 na Patric akaondoka
Hidaya kadaka maongezi yoote akawapigia mjini kuwa mishe imewekwa alhamisi ila sio confirmed kamili ila nitahitaji team ije inipe support huku. Mara akasikia hodii! Akazima simu haraka akaja sebulen, kufungua mlango ni Ismail, vipi kazi zimeisha?!
Ismail: ah we fungua tu bwana mlango nimepigiwa simu mjini kuna dhoruba nimechanganyikiwa
Hidaya: nini tena jaman
Ismail: mke wa Masoud ana ukimwi na inasemekana na Manoa alikuwa anatembea nae ameukwaa huku anaheeema kama kakimbizwa na simba!
Hidaya: ok kama anao ukimwi we unatetemeka nini au ulikuwa unatembea na kungwi?!
Ismail: akaona kawahiwa akadanganya, hapana mke wangu ametembea na Manoa sasa naogopa
Hidaya akapanik kwani wewe, yani, eh! Inamaana na wewe unao?!
Ismail: hata sijui kwakweli sijapima ila sijaonana na mke wangu huu mwezi wa 8
Hidaya kichwani akajipa moyo lakini bado ana wasiwasi, sasa mpenz me nawewe itabidi twende kwa dokta tukapime ukimwi unaonaje?!
Ismail akawa mduuuchuu! Akakubali shingo upande basi tutaenda jumamosi ijayo,
Hidaya akaaga anaenda kumwona mjomba wake mjini atarudi j4!
Ismail akawa amekaa tu hajaskia anachoongea akaomba apumzike kwanza ataongea baadae, Hidaya akamlaza chumbani kwake yeye akaendelea na kazi
Ismail kakaa siku nzima hajatoka ndani, anaishia seblen anakula anarudi kulala, usiku wamelala akaanza kumpapasa Hidaya! Hidaya kamchomoa hapana asee leo me siwezi kukupa umenishtua mbovu! Mpaka tukacheki afya ndio nitakupa, Ismail akachanganyikiwa mara 3 akalala zake fofofo
Kandi na Joe wamerudi toka honeymoon, kandi sasa ana mimba ya miezi 5, tumbo limesogea sogea sio kitoto! Joe anampa ma care ya kufa mtu, hata kutembea hataki anamsukuma kwa wheel chair, kandi akajiuliza ivi kwanini nilimkimbiaga Joe maskini sa hivi ningekuwa mbali kweli, ama kweli alilopanga Mungu mwanadamu asilitenganishe!
Patric akarudi Lusaka amefikia kwa Maringo, usiku wamelala Maringo anahangaika tumbo la muuma, akapelekwa hospital na Patric, kumbe saa ya kujifungua imefika, akajifungua mtoto wa kiume Maringo akafurahi, wanambeba mtoto wanakiss kiss, wakashinda hospital siku 3 wakaondoka nyumbani Patric akamwambia inahitajika mama aje sasa, me naondoka nitarudi ukimaliza uzazi la hasha ukitaka nije mtagombana na mama yako. Akamwachia dola 5000 za matumizi akamfanyia shopping akamwachia mil 3 za hospital, usafiri wake akajaza Petroli, kabla hajaondoka, wakapanga jina, mtoto akaitwa Patric Junior. Akawaaga Akaondoka! Maringo akampigia mama yake Rasmi aje, wakati Rasheeda anajiandaa kutoka Patric akaja, wakasalimiana Rasheeda akampa good news Patric akampongeza akampa mil 2 ya kuuguza akamwambia me nitakuwepo hapa ukunihitaji niambie, Rasheeda akafurahi akaondoka akijua nyuma kaacha bonge la bwana linamsubiria
Neema na Masoud wamerudi toka honeymoon, Neema mimba inakua sasa ni mwezi wa 5, Masoud akamhamisha pale kwake akaenda kumweka kwenye jumba lake la kifahari na watoto wake wote, ile nyumba yake na Pastor akaipangisha! Wanapendwaje sasa! Wanaangaliwaje vzuri sasa kuanzia food, clothing, shelter, madikodiko, Masoud full mass nondo!
Selina na Drogba wamerudi toka honeymoon, Oga na Didie wapo lusaka wanaendelea na kazi, Selina mimba ishakuaaaaaaa miezi 3 sasa! Katumbo kanasukumika kwa mbele kimtindo! Drogba anampendajje sasa, kila saa anampigia simu, kamwekea maid 2, gardner, kazi kamwachisha, akawa amekaa tu ndani analea mimba mpaka atakapomaliza uzazi atafungua biashara, Selina akajiona kama malkia wa nguvu! Sio kwa kupendwa kule, mechi kila siku, simu kila siku, kha Nigeria kaamua!
Pendo yupo na biashara yake sikunyingine mamake anakuja dukani kwake wanakaa, wanarudi wote, skunyingine anaenda job na derev, maana mimba ishakuwa miezi 6 sasa Joseph anampendaje mke wake, duka limepanuliwa likawa kibwa wateja kibaoo! Wanakuja washapazoea kazi zinakuwa nyingi inabidi kungwi amsaidie
Kungwi siku 1 akakaa kwenye akili yake ya kichina, akammpigia Drogba me nina mazungumzo na weee, Drogba akamwambia me nishaoa am happily married, kungwi akamwambia me nina ukimwi na sijui nani kaniambukiza, mh Drogba akawaza akakata simu. Kungwi akajiambia na atanitafuta kama ndio au sio muhusika. Wakiwa wamekaa miezi 3 bila kuwasiliana na Manoa akaona isiwe shida akaenda kwa sonara, akaulizia ile pete alovikwa ina thaman gan?!
Akaambiwa mil 4. Akaona nyiiingi akauza, akapewa mil 4 zake akaondoka,njiani akampigia Rasheeda kama yupo akaambiwa anamzazi analea, dah akachoka akarudi kwake. Jioni akamwambia Pendo na Joseph mimba yako bado sana na mimi nimechoka kukaa Lusaka nataka nisafiri niende nchi zingine kutalii na kufanyiwa psychology! Maana nahisi akili yangu haijachangamka! Wakamchangia mil 8 wakampeleka Dubai, wakalipia matibabu yake, na ndege kwenda na kurudi Kungei kudadeki on 1st class plane! Anakaa na wazungu anashangaa shangaa kweli mama mkwe bobaaa, Dubai mojaaa english anaiweza ye si mwalimu bwana, akafika airport akakuta mtu kashika jina lake kwenye bango, akamfuata akapelekwa mpaka hotelini, 6star hotel, akapewa line mpya ya simu, akapewa time table ya kwensa na kurudi kwenye matibabu,
mwenyewe anashangaa ulaya ndogo kapelekwa ulaya ndogo hata mumewe hajawahi mpeleka, akaona hizo ndio baraka za mwisho kabla hajaondoka duniani, akajiambia Mungu asante ningefika lini Dubai kama sio ukimwi?
ITAENDELEA SAA 9 NANUSU ALASIRI