My cup runeth over ~ Na Kikombe changu kinafurika

My cup runeth over ~ Na Kikombe changu kinafurika

Good Morning
Am sorry niliumwaje! Mungu mwema shetani ameshindwa!
Bado naumwa hapa wameninyang'anya simu hawa watu wangu wa nguvu nimeidaka leo asubuhi nikaificha kwenye maziwa! Walipoenda kazini ndio nimekamatia chungu

Afu me sio mwingi wa inbox ya JF, kama unataka mazungumzo na mimi one on one njoo whatsapp kwa no +255688411043. Namba hii ni ya whatsapp tuu

TUNAENDELEA

B. TEAM BUBAAA



Waziri na waziri mkuu wakaumiza vichwa weee! Tunamsaidiaje ndugu yetu jamaa! Maana hii ishakuwa sheeda ikifika mahakaman hachomoki!
Maana sasa hapa wanalala ndani kuanzia diwani, mwenyekiti wa serikali za mitaa na mkuu wa mkoa, wakasugua kichwa wakaona wamwite mkuu wa kitengo cha usalama. Bwana Mzee!

Mzee wa usalama, kubwa la maadui, final say, akatia timu kuskiliza kesi ya mamba na kenge
Bwana Mzee: hawa vijana wana tamaa sana, sasa nini kulaghai wananchi?!
Waziri Mkuu: mzee huyu ni kijana wetu, tumemkuza, tuangalie namna ya kumsaidia
Bwana Mzee: kwani yupo kwenye system?!
Waziri Mkuu: hapana hayupo ila anaweza kuandaliwa vizuri tu
Bwana Mzee: ah huyu Patric muhuni sana!
Waziri Mkuu: Mzee wewe ndio una final say, ukisema tupige chini tunamtumbukiza mahakamano, ukisema abaki tunamleta a join the force!
Bwana Mzee: na huyu Ismail mtamfanyaje?!
Waziri Mkuu: nae kama hautamhitaji we twambie twampiga chini ila kwasababu kesi ni ya watu wawili lazima wote waingie
Bwana Mzee: wawekeni ndani kwanza mtulize fujo za wananchi, alafu baadae nitawafuata jela niongee nao nione seriousness yao. Kwani alietakiwa kushinda ni nani?!
Waziri Mkuu: ni fulan bin fulan
Bwana Mzee: mtamtangazaje sasa?! Maana hii ishu ishakuwa balaa wakibakishwa nchini watauawa haraka sana. Wawekeni ndani kwanza nitaongea nao mimi nipange na makamu wa raisi jinsi ya kufanya kuwaondoa nchini wakafanye kazi nje maisha yao yote
Waziri Mkuu: sawa mkuu
Bwana Mzee akasepa zake!

Patric akaitwa na Waziri mkuu akaambiwa aandike makosa yake yote aliofanya na asign akubali alichofanya kwa upande wake na aombe msahamaha. Patric akaja fasta! Akafanya kama alichoambiwa, alipomaliza kusaini wakaingia mapolisi, Patric you are under the rest kwa kuidanganya serikali, utashitakiwa kifungu namba so and so.. uuuwi patric akalowa, jela ndo iyoo! Na adhabu yako ni kifungo cha maisha au kunyongwa! Kama utahitaji lawyear utapewa na mahakama au utatafuta mwenyewe!

Wakampigia simu Hidaya atoke kijijini arudi kutoa taarifa za maagizo aliotumwa kijijini, akaondoka asubuhi alfajiri, mwenyewe na nguo zake! Kweli mjeshi mjeshi tu. Saa 5 asubuhi wakaingia mapolisi 20, wakasakunyua nyumba yake yoote toa kila kitu, wakaweka kwenye roli, wakamfuata Ismail nyumbani, mkewe soya akawa anashangaa kunanini, akaambiwa mama mumeo yupo chini ya ulinzi hapa tunavyoongea mtoe au si tutamburuta,
Ismail alikuwa anatoka kuoga aliposkia chini ya ulinzi akakimbia kuvaa nguo haraka haraka akajipiga perfume maana jela hamna kuoga beba the necessities! Akatoka akakutana na Soya anakuja ndani kumwita wakatoka wote, mapolisi wakamwelezea makosa yake mkewe akachoka mara 100, mume wangu jaman tamaa ya nini lakini?! Mbona watoto wanatuangalia vizuri tu jaman sa me ntaenda wapi huku sina hata sumni jaman! Uuuwi Soya analiaje majirani wakajaa wanashangaa kunanini?! Wengine wamemshika Soya wanambembeleza, soya hana raha maskini! Analia mpaka kazimia ikabidi apelekwe hospital, wakabakia mapolisi 5 wana search nyumba yote ya masoud wanabomoa milango, vyoo, wapo na mbwa wawili

Wengine wakaondoka na Ismail, wakafika ofisi ya Ismail wakawakuta wapelelezi na mbwa 10 wamefika, wameshaanza search ofisini mwa ismail, bwana bwana mapolisi ni wa kalije?! Ni shesheje?! Uuuwi! Ismail kalowa kama sio yeye akiangalia nyumba ya Hidaya ipo wazi akajua hata Hidaya kimemnukia

Wakamwambia tupeleke ulipoficha ushahidi, msitu wa kati, Ismail anashangaa wamejuaje?! Ikabidi awapeleke sio kwa yale makonde aliokuwa anapigwa mbwe mbele Ismail katikati, mapolisi nyuma, mbwa akanusa akaganda pale, tobaa roho yangu! Kufukua ndo penyewe, Ismail akatupwa akaokote akaokota akatoa, wakazifi kuchimba chini mpaka wakapata evidence zoote wakaondoka nae kwenye gari wamemfunga pingu!
Soya kapelekwa hospital akawekewa drip, baafa ya masaa 4 akaamka zake, yupo vizuri majirani wakaondoka kumrudisha nyumbani

Ismail akafikishwa Lusaka mjini, akapelekwa ofisi ya waziri mkuu, anashangaa tu imekuwaje au Patric amemsnitch?!
Akasomewa makosa yake anakataa, akaambiwa ukikataa mzee kwenyw mahakama afu mwenzio amekiri hapa na kusaini mmeshirikiana utafungwa maisha! Ismail akameza mate, akili imemwisha hajui akubali au akatae, akaendelea kukataa me sijui kitu wakamweka ndani kwa muda wa mwiezi 3 wakisubiri hukumu

Musa akaambiwa kuwa mkeo is no mote! Uuuwi aliliaje sasa?! Kiru! Ndorooboooe! Ukiona mtu mzima analiaaa ujue kuna jambooo! Musa alilia maskini kapoteza mke na watoto kumbe Mrembo alikuwa na mimba ya mapachaje! Kha huruma.
Akampigia simu boss wake kuwa amefiwa, akapigia wazazi wa Mrembo wakajaa nyumbani kwa musa, kilioooo watu kibaoo msiba mkubwaaaa Kandi nae kusikia hakuelewa imekuwaje kuwaje wakaondoka nduki na Joe wakaenda msibani kumsaidia Musa. Msiba ukawekwa kambi siku 2



Pendo amepata watoto mapacha, wakaja masoud na neema kuwaona, watoto wazuuuri hao, wa kike na kiume, wa kike wakamwita Rhoda jina la marehemu Kungwi, wa kiume anaitwa Andrew jina la baba yake na Joseph! Akina Masoud wakafurahi, little kungwi is back into the world akajisemea Masoud kimoyomoyo i hope hatakuwa na character za kungwi akamwuliza pendo kwanini umemwita jina la Rhoda?! Akajibu ah kwasababu mam ameondoka mapema bila kuaga nimeamua kumuita in a memory of her! Masoud akachoka ndani kwa ndani. Neema akampa hongera mtoto wake wa kambo Pendo, wakaaga maana nae Neema mimba ilikuwa imeshaenda miezi 8 anatakiwa bed rest muda mwingi

Rasheeda anamtafuta Patric minyege imemjaa, tobaa! Namba haipo! Mh akaanza kuwa na wasiwasi, khaaa! Kuna nini mara wakaskia kwenye redio kwenye habari uteuzi wa mkuu wa mkoa mpya na Bwana Patric yuko jela kwa kuidanganya serikali na wananchi akisubiri hukumu. Rasheeda alipiga kelele kama anazaa akaanza kulia, uuuwi jaman hii aibu nitaishi wapi sasa nitaishi na nani?! Yesu wangu analia akampigia simu Maringo, akamweleza baba yako wa kambo yupo jela, amefungwa, maringo akajikaza na wewe! Pole sana mama, pole jaman nakupenda mama yangu ngoja nakuja kukuona! Kama itakuwa ngumu njoo ukae hapa na mimi na wajukui basi, wakakubaliana Mama yake akakae nae kwa kipindi kile! Alipokata simu Maringo akalia sana lwa uchungu akawaza ndio maana Patric alifanya yale aliotakiwa kufanya! Dah jaman kwanini lakini?!

Soya kurudi nyumbani baada ya siku 2, akawapigia watoto wake simu kuwa baba yao kawekwa ndani waje wamchukue yeye hawezi kuishi pale, baada ya siku 2 watoto wakaja wote 2, wakampa pole mama yao, mama yao akawaeleza kila kitu kuhusu yeye na kila kitu kuhusu Ismail na kwamba amepewa notice ya siku 1 kuhama pale maana wanaleta mtu mwengine pale ambae ni mwenyekiti wa kijiji kuja kuishi, wakatafuta gari ya mizigo wakaweka mizigo soku hiyo hiyo, wakampakia mama yao wakaenda ofisi ya baba yao ya zamani wakamkabidhi wenyekiti mpya funguo wa nyumba wakaondoka siku 1 kabla.

Kufika mjini walipo settle, Soya akaomba wanae waende kumwona baba yao! Wakafunga safari mpaka jela wakamkuta Ismail kapunguaaa! Chezea Jela wewe?! Soya akaanza kulia mume wangu nakupenda jaman kule nimefukuzwa naishi na watoto sasa, nitakuwa nakuja kukuona usijali, ila Ismail kaisha, kaisha mbayaa! Wakamsalimia watoto wakasema tutafute wakili akusaidie kesiw akamtafutia wakili, akaja kuanza kumhudumia ismail

Usiku wamerudi nyumbani Soya anawaza jaman ntafanyaje bila mume watoto ni watoto tuu! Itakuwaje, na huu ugonjwa nawatesa watoto! Akawaza ee na kuwazua ee mpaka akapata heart attack akawa hawezi kupumua, akawa anajitahidi kunyanyuka kitandani! Iliakilimbilie chumba kingine, anajikokota mara akaufikia mlango, akawa anaita lakini hasikii, anamwita mtoto wake wa kiume aliekuwa amelala, lakini hasikiki! Kuita na ile heart attack akadondoka chini, akafa!

ITAENDELEA LEO SAA 9 ALASIRI
 
B. TEAM BUBAA

Akashtuka mjukuu wa kiume wa soya anaenda chooni! Kufika anaona bibi kalala chini akaanza kumuamsha, bibi amka, bibi amkaaa, huku anamvuta mkono! Bibi amka tafadhali bibiiiii!
Akaondoka akaenda kumgongea mama yake na baba yake, mama fungua akashtuka mtoto wa Soya akafungua mlango, baba bibi kalala pale hataki kuamka, akakimbia kwenda kuangalia tobaa roho yake blbi haamki! Uuuwi! Mshika shingo hapumui, akamwamsha amsha akamwambia mwanae kamwamshe mama toto likakimbia anajua mchezo akaenda kumwamsha mamake akaja, wakambeba mpaka kwenye garo hospitali mojaaa! Kufika wanaambiwa mama yenu alishakufa muda! Hamkuona amekuwa wabaridi?! Wanashangaa dah mtoto wa Soya Rashid akalia kwa uchungu mkewake anambembeleza.

Manoa akawazaaa na kuwazua wee! Akaona hapa atakufa anajiona bado anamaisha meengi sana ya kuishi akaenda councelling, akaanza therapy kwa muda wa miezi kadhaa. Anauliza maswali anajibiwa, biashara zinaenda vizuri sana. It's amazing wakati mambo yanafunguka kifo kinakukaribia!
Akawa anaenda kwa wajukuu wake wa Maringo, Luwi, Hashikoko, ana rotate kila week anaenda kwa mtoto m1.

Rasheeda akaamia kwa Maringo, ile nyumba alopangiwa na Patric akaipangisha tena maana walishaona hapa Don patric hayupo wanatakiwa waishi kwa akili, akajihamishia kwa Mwanae Maringo kwani ana shida gani?! Yeye ndo mama, wakawa wanaishi wote anakuja Manoa wanagombana weee Manoa anaondoka hakai hata wiki keshasimangwa na Rasheeda anaondoka



Wakaondoka na Maringo kwenda jela kutembelea Patric, kufika Patric anashangaa, wake zangu wawili wamekujaje?! Maringo akamkonyeza akajua hapa siri sirini! Wakaongea pale Rasheea anajiliza, Maringo anamtia moyo, kweli wazambia ma actress hakuna mfano wake!
Wakarudi nyumbani, wakamkuta manoa, ugomvi mpaka Maringo aingilie kati ndio wanaachana. Rasheeda anamwita mwenzake muathirika, Manoa anamwita mwenzie alieachwa, yeye si alialmuacha Manoa? How does it feel kuachwa?! Kumbe inauma ee kakae kwako na wewe unatafta nini kwa Maringo? Rasheeda anajibu na wewe kama una hela unatafuta nini kwa Maringo?!
Manoa: me nimekuja routine kuangalia wajukuu
Rasheeda: mmh usije ukawaambukiza ukimwi wajukuu mshenzi mkubwa wewe! Embu ondoka na mapepo yako ya ukimwi usiambukize kizazi chetu cha 2
Hapo ugomvi hatarious! Maringo akachoka jaman mnataka niwafukuze nini?! Manoa anajibu ndio tufukuze wote lkn sio mmoja! Rasheeda anagomba me stoki, basi ni balaa!
Manoa akaondoka akamwambia Rasheeda unanidhalilisha me ntakufanya kitu kibaya wewe utanikumbuka maisha yako yote chini ya jua! Rasheeda akamjibu bring it on looser! Manoa akasepa anasema nyau wewe lazima nikufanye tukio hautakaa usahau!

Baada ya mwezi mmoja Neema akajifungua mtoto wa kiume! Masoud akafurahi, Masoud akamwita mtoto Ishmael, Neema anavyoijua biblia akalikataa hilo jina akakataa akaomba wasubiri watafute jina lingine taratibu mtoto akawa anaitwa baby boy tu.

Baada ya wiki 2 akajifungua Kandi mtoto wa kike, Joe akafurahi sana, wakamwita jina Casandra

Mazishi ya mrembo yakafanyika pale, ibada alafu wakazika, dah Musa haamini amebakia pekeyake! Upweke nyumba anaiona ngumu, kubwaaa, akaona akiendelea kukaa pale atakufa, akaomba likizo ya mwezi mzima, akalipizia na likizo zake za nyuma, bank wakamwambia tunaelewa, chukua miezi 2 tumekupa kama mchango wetu wa bank, safiri nenda mbali na Zambia kakae huku upate hata help ya conucelors alafu urudi kazini. Akaaga ofisi akaipangisha ile nyumba akaondoka zake akaingia Cassablanka Morocco.

Mahakama ikaskiliza kesi ya Patric na Ismail, wananchi wakajaa, akina Rasheeda na Maringo!na wengine wengi lakini watoto wa Ismail hawakuwepo hata m1. Kesi ikaskilizwa pale mpaka mwisho, hamna majaji wakaomba recess. Wakaenda kutafakari na jury!
Baada ya masaa 3 wakaja tena. Patric akahojiwa pale akasema me mheshimiwa hakima nakubali kiiila kitu kweli nimefanya
Wakampandisha Ismail akakataa me sijui chochote, na Patric simfaham! Dah kudadeki
Mteteji wa wananchi nae akasimama akatoa yake! Ismail akajiona mbululaz!
Baada ya masaa 4 hukumu ikatoka!
Kabla ya hukumu Jaji akasema naomba excuse kwa Ismail amepatwa msiba, mke wake mpendwa Soya Ismail amefariki dunia juzi usiku! Ismail yupo tobaaa, jaji akamalizia kwa heart attack! Ismail akachoka mara 100 akakaa chini maana waliambiwa wasimame ivoo! Patric akamhurumia sana Ismail lkn afanyaje!
Hukumu ikasomwa sasa, uuuwi!
Patric unatunukiwa kifungo cha maisha!
Ismail unatunukiwa kifungo cha maisha ikifuatiwa na kunyongwa kwa kuwa muongo! Tunakupa wiki 1 ya kutubu dhambi zako kama ni familia uiage kuwa unaondoka! Tumekuhurumia ulitakiwa unyongwe kesho ila kwasababu ya msiba utanyongwa baada ya wiki 1.
Ismail akadondoka chini akazimia! Wakili na ma afande wakaanza kumzoa zoa pale wanambeba kwenda jela!

Bwana mzee alikuwepo, anaangalia matukio yooote, amekaa seat ya nyuma kabisa amevaa miwani meusi akawa anacheka tu!



ITAENDELEA LEO SAA 3 USIKU
 
pole kwa kuumwa Mungu amekupigania na kukushika mkono..asante kwa kujikongoja kutuletea story taamu,ubarikiwe saana
 
B. TEAM BUBAA



Mazishi ya Soya yakafanyika, si unajua waislam tena, mzigo haulali wakazika siku inayofuata, makaburi ya Lusaka maana mume hakuwepo kusema azikiwe wapi na vile serikali ishampiga chini kila kitu imemtaifisha! Wai wakaona wazikie pale pale mjini angalau watoto wake 2 na wajukuu 8 wataenda kuona kwa karibu!

Baada ya siku 5 za msiba watoto pamoja na wajukuu wa Ismail wakaenda kumtembelea baba/babu yao jela, wakaimba radhi hawakwenda kwenyw hukumu maana msiba ulikuwa wa ghafla sio kitoto! Ismail akawapa pole akawaambia nilipewa taarija na jaji nikazimia wakanileta huku! Namhurumia sana Soya tulipendana ila alipenda dyu dyu zaidi yangu sasa amevuba alichopanda. Wakaendelea kuongea mambo yao akawaelezea kesi ilivyoenda wakaongea for 2 hrs wakaondoka!

Evelyne due date ikafika akajifungua watoto mapach, Luwi akafurahi akawaita majina Betty and Betsy! Rasheeda na Maringo wakaja kuwasabahi, wanafurahia wenyewe ma twins wa kike, wazurije sasa, na Eveline alivyokuwa white mbona watoto walitoka kama machitara! Kweli Evelina Evelina Evelina, evelina ..... ah nimesahau me sio mcongoles!

Baada ya siku 2 wakati Rasheeda anamsaidia uzazi Evelyne, Maringo akaondoka akaenda kumwona Patric kwa siri amebeba mtoto wake Junior, Patric akafurahi sana, Maringo akamwambia Patric nimechoka kuishi kwenye ukapela wangu, hapa nina nyege za kuhamisha Lusaka kwenda Accra na Accra kuja Lusaka.
Patric: akacheka tu skuhizi uou got jokes mpenzi? Naomba nivumilie miezi 6 i have a feeling case yangu nitatolewa. Maringo akaguna mmh! How wakati mahakama imeamua hivyo!?
Patric: trust me Maringo nivumilie kweli i have guts, naamini nachomoka ndani ya miezi 6 ikitokea nitakuja kukuchukua na watoto wangu tutaishi wote!
Maringo akaitikia tu sawa kwa shingo upande! Maana lile alilokuwa anaongea Patric kama sio ni ukichaa basi ni fairy tale! Baada ya masaa 2 Maringo akasepa na mwanae Junior, Patric analiangalia lile sext body anamwambia Mungu kimoyomoyo Abeg nitunIe Mrembo nikitoka namuoa jumla!



Suzana akampigia wifi yake Maringi, naskia kakako kapata mapacha wifi wangu hata hauniambii?!
Maringo: nani amekwambia
Suzana: mama yako huyoo!
Maringo: mh me ndio narudi kutoka mkoa hata sijui kitu
Suzana: wifi umekuwa adimu sana we should meet up jaman hata for coffee!
Maringo: sawa weekend vepee?! Twaweza onana?! Wakakubaliana pale Suzana akaingia duka la nguo! Anamkuta Pendo, akasema makuuuubwaaa! We Pendo na wewe unafikaga maduka haya?!
Pendo: akacheka karibu dokta! Au should i say psychologist?!
Suzana: akacheeka! Shoga upo?!
Pendo: nipo karibu
Suzana: asante mwaya natafuta nguo ya mwanangu bado mdogo miezi 8 sasa nikaelekezwa hapa duka ni zuuuri asee huku anachagua nguo
Pendo: karibu sana hapa ni kijiwe changu kwa muda tu!
Suzana akampa hongera pale akanunua nguo nyingi za mtoto na zake akamwambia Pendo naanzisha this club ya wale niliosoma nao na marafki zangu kama una best yako karibu
Pendo akashukuru wakabadilishana namba za simu pale Suzana akaaga nitakutumia sms ya tarehe ya kuanza, tutaanzia nyumbani kwangu kwanza, uje tu na watoro wako na dada nyumba yangu kubwa sana hamna neno! Huyoo ndukii

Didie akawa anayaangalua maisha ya pacha yake, haelewi akaamua kujikaza aende kucheki, kumbe ndo kajiponza kuangalia matokea yametoka ana miwaya kibao yaani VVU! OGaaaaad! Me HIV ooo?!hoooow naaaaaw?! Akawa analia pale si unajua wa Nigeri walivyo dramatic?! Akaleta mapichaa pale kibao wakamlaza kwa sindano ya usingizi mpaka Drogba alipokuja kumtoa!

Usiku wakaenda club Oga, Didie na Drogba! Wakawa wanamtia moyo didie, anashangaa ameupata wapi?! Au ni yule kungwi nilipiga nae mieleka one time ndio imekuwa shida au ni yule Mary?! We Drogba ndo ulinichuza ona sasa nakufa na wewe?! Wakalaumiana pale Oga akaamua wakacha drama wakawa wanakunywa pombe. Pembeni alikaa manoa amesikia kiila kitu akaomba awa join. Akamwaga yake hata me nipo frustrated nina ukimwi na sijui nafanyaje?!
Didie: lazima tuusambaze kwa watoto wa kizambia wao ndo wametuletea me lazima nilipize kisasi
Mano: na mie nataka kumlipiza ex wife wangu ananinyanyapaa sana na huu ugonjwa sina raha nae, nataka nihakikishe nae kaupata
Didie: nipe hito kazi me ntaifanya nipe namba location mingles zake kila kitu
Manoa akakubali akafurahi waka exchange contacts wakakubaliana show ipigwe weekend maana Rasheeda anajishaua na vipesa vyake vichache anaona kila mtu ni mavi! Didie akamwambia usikonde mwana.
Wakaendelea na Plan B yao kama nigerians ya kuibia watu pesa, maana Drogba ana warning kibao ofisini akishapewa moja anaondolewa kwa kutegatega bila taarifa!
Didie akawaambia wameingia wazungu nchini ku invest na madolari yao kama vipi tuanze na wao Oga unasemaje?!
Oga: me nina akaunts za mawaziri afu kuna mjinga mkoja alichomoa hela ndefu sana kwenye akaunt yake sijui kahakisha wapi kama tungezidaka zile kudadeki ingekuwa poa sawa! Me mwenyewe nimechoka kukaa bank ila nikipata hela ndefu kazi naacha nahamia Lagos!
Manoa akabakia anatoa machi akawaambia sasa me mtanisaidiaje labda maana me mweupee. Wakamwambia mzee we hii kazi ya vijana hautaiweza kwani wajua kushika bunduki wewe?! Akajibu hapana!
Oga basi tutakufundisha hamna neno paaps! Wakapanga nae mchongo kila siku wanakutana wanafundishana hacking za kwenye ma benki mpaka Manoa akakolea! Akajua! Akaanza kuongea na Maringo kuhusu wazungu wa ofisini kwake wenye hela akitajiwa anaenda kuwapa akina Didie wanamwona mjaaaanja kweli for a grand pa you is a shit man! Wanamsifia paleee Manoa asijue kuwa m nigeria ni Mnigeria tu hata kaa awe Mzambia! Wanajua kusakiliza hakuna mfano afu wanakugeuka kama sio wao!

Dereva wa Patric akaamua kurudi kwa Mary kama upo upo basi hata tukipigana miti kuna kosa gan si sisi kwa sisi tuu! Akarudi na mapenzi mubashara kibaaao! Mary anamwangakia tu mara akamvamia wakaanza kupandiana, juu chini juu chini kama twist vile!Mary akashukuru maana hajalalwa ana miezi 8, anahisi alishakuwa bikra! Hehe! Lakini haikuwa ya mapenzi kwa Dereva. Dereva alikuwa na hasira vibaya mno! Akaona hapa ambamize Mary bonge la bubaaa asepe! Alipomalizana na mary akaanza kutunga sheria ya kuwapa miti innocents! Kweli wagonjwa wa ukimwi ni noumer! Sio kwa roho mbaya hizo, akawa anawapiga miti mpaka watoto wa shule bwana, mambo gan sa! Akaja kufumaniwa na wazazi wa watoto 2 walimpigaa piga wakamtupa jela akalala wiki 3 akatolewa kwa dhamana na mkewake, Mary hana habari maskini,

Mary akaskia Patric alipo akafunga safari mpaka Jela. Akaenda kumsalimia Patric, anamcheka anamwambia your highness has dropped low, the horse has left the owner! Nakuona ulikuwa kwenye high horses, now unatembea kwa miguu! Imekuwaje mheshimiwa?! Unalala na wanaume kama mwanamke! Nina uhakika mpaka sasa utakuwa kama mimi na ma VVU. Bora uliwekwa jela sasa nitapata custody yote ya watoto! Bora me mdhambi ila we mhujumu mali za uma hawatakupa watoto ng'o. Patric akampiga kibao cha kwanza na cha pili wakaja mapolisi wakamshika, Mary akamtemea mate Ptuuuu! Patric akayakwepa akampiga bonge la teke la tumbo Mary akaanguka chini, Wakamwondoa Patric wakamrudisha ndani Mary akajiokota mdogo mdogo akasepa zake kwake!

Baada ya miezi 3 ya mateso ya Jela na drama za hapa na pale, Bwans Mzee akaenda kuwatembelea Patric na Ismail kila mtu na time zake!
Akaanza na Patric! akamwuliza unanikumbuka?!
Patric: ndio!
Bwana Mzee: maisha yanaendeleaje
Patric: magumu kuna nini mbona uko hapa?! Au umekuja kuninyang'anya watoto wangu?!
Bwana Mzee: nimekuja kukupa uchaguzi either wa kukaa humu maisha au ulitumikie taifa uwe snitch!
Patric: snitch kivipi?!
Bwana Mzee: CIA, FBI, Police department! Your choice! Kati ya haya matatu chagua moja. Uwa sitembeleagi wana jela kila saa this is one time life offer! Take it or leave it!
Patric: nikikubali ofa yako maisha yangu yatakuwaje mtaani?!
Bwana Mzee: hayo niachie mimi, ila hautaishi hapa Zambia wala Africa.
Patric: nipe muda wa kufikiria nina familia inanitegemea nje
Bwana Mzee: mtahama wewe na familia yako
Patric: peni iko wapi nisaini
Bwana Mzee akatoa peni na karatasi akasaini, akaambiwa ndani ya masaa 48 nakuja kukutoa. Akarudishwa selo!
Patric akafurahi kweli Mungu kamkumbuka kumbe what i said kimekuwa alive. Amen to that akafurahi finally anaenda kwa Maringo na Rasheeda!

Bwana Mzee akafanya hayo hayo kwa Ismail. Ismail sijui ndio ushamba au nini akakataa kwanza akaishia kumtemea mate Bwana Mzee usoni, akamwambia *** you and your stuff! Siwahitaji washenzi wafupi nyie!
Bwana mzee akatoa handkerchief akajifuta mate, akamwambia sawa umechagua fungu jema utafia jela siku sio nyingi, akaondoka Ismail akaja kurudishwa celo.

Usiku akiwa amelala usiku wa saa 7 akaja kuamshwa na mapolisi wakampeleka nje wakampigaaa,pigaaaaa pigaaa na wewe acha kabisaa, Ismail ameshakuwa mzee sasa, hawezi tena alipigwa mpaka akafa!



ITAENDELEA SAA 5 ASUBUHI KESHO
NGOJA NILALE MIE BYE YA'LL
 
KABLA SIJAENDELEA
NATAKA KUMPONGEZA BEYONCE!
KUDADEKI *****, ANA TWINS?!
JESOOOOOS! HONGERA SANA LOVE
TWINS ALSO KNOWN AS THE NATURE FREAKS
SHE GOT DOUBLE DOUBLE FOR ALL HER HUSBAND'S TROUBLES!
FOR MORE NEWS FUNGUA VIDEO



B. TEAM BUBAA

Maringo akaja kumtembelea ex wifi yake Suzana, wakapiga umbea weee mpaka maka, masaa 8 wanaongea, wanasimuliana maswahiba walioyapata kipindi chote tangu walipoachana, Suzana akamwambia me nafikiria kufungua this group ya watu kama 5 mpaka 7 kama unamfahamu any friend of yours mkaribishe! Tuanze next weekend! Maringo akakubali, wakapeana muda na mahali.
Suzana: maaana nafanya research ya mambo ya ndoa na maisha yake! Tuone kama tunaweza saidiana sisi wanawake!

Kuamka asubuhi Patric yupo excited kuwa leo anatoka anaenda kuonana na wapenzi wake wakatangaziwa kuwa Ismail amefariki, dah alijiskia uchungu kweli ismail rafkiake kipenz akawa haelewi imekuwaje alipouliza akajibiwa kunya akaondoka zake, akasubiri weee mpaka muda alioambiwa lakini hakutokea Bwana Mzee, mpaka lunch mpaka usiku hamna kitu akajua tuu hii nimepigwa bubaaa nimeaminishwa na kupigwa chini!

Watoto wa Ismail wakapewa taarifa kuwa baba yao amefariki, wakajiskia vbaya sana maana hata kuzika hawakupewa ruhusa wakaambiwa mali ya baba yenu ni ya serikali kwa sasa! Wakaondoka na huzuni hawajamuona hata baba yao!

Akina Didie na Drogba na Oga wakaanza kuibia watu. Tukio la kwanza likapigwa kwenye ma bank na atms. Wakafanya mchezo wa kids sniffing
Huu mchezo unafanywa hivi:
Ta kwanza:
Una register demo akaunt kwenye laptop yako, unatafuta zile tarakimu 3 za mwisho kwenye atm card ya mlengwa, hacker anaweza kusoma una bei gani kwenye bank akaunt yako.
Kwenye ile demo ya hacker wanakuwa na software ambayo inamfanya aweze ku-hack password ya mtu / mlengwa!
Tukio la kwanA walilifanya kwa mzungu mmoja investor alikuja ku invest kwenye oil and gas Zambia, bwana bwana wee Nigerians wapo kwenye level ingine, mzungu alisafiiishwa, kwanza akina Drogba walimtega, wakamsoma ramani ya atm zake zoote anazoenda, wanasoma kwa muda wa wiki na hivi, zungu akifanya shoppung anatumia atm card, wakaanza ku move! Kila akienda atm akaweka card akitoka wao wanaenda kuweka ka small mini camera ukutani adjacent na atm ambayo anaweza kuona password!

Wiki ya pili mzungu akatokea kwenye atm ya bank, wao wamekaa home wanamzoom tu!
(Yeeesu na Maria, jaman me naandika wizi woote huu si ntakamatwa?! Kiruu JF mnisamehe hii ni stori tu)
Akaandika password yake raia wakadaka mtaa wa 3. Mzungu akaendelea na business zake jamaa wakavuta pesa sio kitoto, akaunt ilikuwa na dola laki 1 wakambakishia dola elfu 10 tu nyingine yote mijeda wamepausha!
Mzungu kuja kushtuka wajeda wana throw parties za kufa mtu! Alafu hela zao akina didie na oga na drogba wanazipeleka kwaoo Nigeria yani wapo radhi wapande business class au 1st class lakini wapitishe hela walioiba wafkishe kwao! Kiruu



Tukio la pili wakamchapa nalo waziri mmoja ivi, kuja kushtuka ana dola 1000 bwana bwanaa alidataje, alikomaaje na banks?! Wakamwambia we ndo umetoa kwenye atm so and soo saa fulani, waziri anakataa. Wanamwonyesha na password ulioweka waziri anakataa! Eh mpaka waziri aje kukaa sawa kujua amekuwa hacked Nigerians washachanua kwaoo!
Drogba akawa hafiki ofisini akafukuzwa kazi kabisaa, akaona poa tu, wakaendelea na mchezo wai wa kiiila siku hawapumziki! Serikali ikaskia kilio cha wananchi, hata wananchi matajiri nao wakapigwaa! Ikabidi waweke wapelelezi!


Maringo na ukame wa dyu dyu uchi unavuuutaa! Hajui cha kufanya Patric kamuahidi anarudi mpaka sasa hajaja akaskia kwa Kandi kuwa Oga ana helaaaa ana heeeeeeeelaaaaa akaamua kumtafuta, analegeza sauti nene, Oga akajua anaitwa, wakapanga wakutane hotelini maringo akamwomba mama yake aje amwangalizie junior akamfuata Oga.
Oga kufika akampa dola elfu 10. Mh! Maringo akashtuka anauliza ya nini?! Akamwambia zawadi yako. Maringo akachukua ila shida yake haswa ilikuwa ni dyu dyu, waka rent chumba oga kalipa kiila kitu, wakapigana miti, Maringo ham feel kiviile Oga, kitandani sio kiviiile kama Patric, lakini afanyaje kama una njaa ya chips ukaletewa ugali si utakula tu ilimradi upooze njaa?! Ndo alichofanya maringo!



Asubuhi akaamka alfajiri akawa anataka kuondoka akadakwa akapewa kichapi kingine na Oga cha alfajiri! Akasepa zake job njiani anawaza Oga amepata wapi hela kibao?! Hajui!
Tabia ikawa ni kama mazoea, Maringo akisikia haja anamtafuta Oga sasa kwa pesa na sio dyudyu mechi anagawa tu ilimradi mtu mwenyewe anamoa hela, skunyingine dola 5000 skuingine dola 2000 akunyingine dola 3000 hajawahi shuka chini ya dola 2000 Maringo being smart akawa anasave zile hela!

Rasheesa na ukame wa ukame akawa anamwona Maringo anarudi na hela nyingi anapewa akaamua na yeye aulize nani kakupa?! Akaambiwa baby daddy wangu, akauliza kwao wana hela?! Akajibu ndio wanazo kibao, akashangaa siku Maringo amelala akaiba namba ya Oga, baada ya wiki kupita, akampigia Oga wakutane, skuhiyo wanaenda kukutana akamwona Oga amekaa na Didie wanamsubiria! Akampenda Didie zaidi ya Oga akaamua asiende akasubiria amfuate Didie baadae akamfuata mpaka anapoenda, skuhiyo didie akawa yupo hotelini, Rasheeda akaiba nguo za hotelini akajivalisha kama hoteli akaenda kugonga room service!
Akafunguliwa akawa anasafirsha huku ana flirt na Didie, didie nae mwingi akapokea ujumbe, wakaanaa kupigana miti, Rasheeda nae mpuuuzi anakula kavu kavu mru hamjui!
Baada ta mechi maana Rasheeda alitoa mechi ya kufa mtu didie aka appreciate, akiwa anajiandaa kuondoka Didie akampa namba yake ya simu na hela dola 5000 Rasheeda akaona kweli hili bonge la bwana asijue ana bwana soon ataenda kukutana nae Mbinguni!

Club ikaandaliwa na Suzan warembo wakatia timu
Maringo akamleta Evelyne, Pendo akaja na Kandi, Hidaya akaja na Kipofu (Betty ila skuhizi anaona na anatembea uzuri tu)
Club na wewe wakaanza kutambulishana, ilipofika zamu ya Kandi Maringo akasema namjua aliniibia bwana wangu ila namshukuru sana maana maisha yangu yapo mara 100 zaidi ya kandi, kandi akawa mpole, Maringo akamkejeli weee mwanzo mwisho! Lakini wapi! Kandi kawa mpole kama mbwa koko!
Kila mmoja akajielezea yeye ni nani na anafanya shughuli gani, Hidaya ni rafiki na suzana walisoma wote, hidaya akasema me ni mwanasheria, Kipofu akasema me ni mfanya biashara!
Suzana akasema tutakuwa tunadiscuss kila kitu kuhusu maisha yetu! Tuwe free kudiscuss vitu vinavyotusumbua! Mmoja mmoja akaanza kufunguka kivyake, kukawa na kelele hamna maskilizano basi shida suzana akaingilia kati basi me ntakuwa monitor tuanze naaa. Naaaa ngoja tuanze na Hidaya
Hidaya akafunguka akapitaaa... Evelyne akafunguka akapitaaaa... kandi nae hivyo hivyo akapitaaaa... Maringo akajibwaaayaaa akapitaaaa Pendo akaongea dk 10 akamaliza wakamshangaa....betty akaongeaaa akamalizaaa... suzana akasema me nitaongea skunyingine wakaanza kushauriana club ikaisha tukutane next time wakapeana muda

Didie akakutana na Manoa na Drogba, Didie akamwuliza Manoa ex wife wako yupoje nianze kaI akapewa picha! Tobaaa kumbe kazi alishaianza muuuuda akamdanganya sawa nitaifanya unataka nimfanyaje?! Akamwambia we mchape dudu tu ila usimwuue, Didie akasema iyo imepita kuna lingine?! Manoa akasema hapana

Oga akaja akawaambia jamaa ile issue yetu ya Atm tuache kwanza twende na hii ya pili maana naskia wameshawekwa wapelelezi kurufuatilia tuzime kwanza programme tuende ingine!
Wakaingia kwenye chemba no 2.
Ya pili:
Ni kuzitumia zile atm cards ku swap kwenye matumizi ta kila siku, basic needs, kwenda ma club hatulipi kwa cash tunalipa kwa atm card! Dah mchezo ule ule ila rangi tofauti!
Wakampa Manoa dola 10000 manoa anaona nyota hela zote hizi?! Wenzake wanamcheka mzee chukua ukale maisha, dah manoa hakuaminj na ivi anaishi na VVU akaamua kwenda kuji pimp awe wa ukweli akawa anazunguka na totos wadooogo anawapeleka shopping keshakuwa sugar daddy tena afanyaje!


Maisha yamemwendea vizuri hananstress pesa ipo, maisha ndo hayo anayafaidi! Mungu mwema anasambaza ukumwi kama anasambaza biashara take ya kuku, anavipiga vitoto vya lusaka bila kinga, hawajui maskini wanajaaje pale kwake sasa! Ni sheedah!

ITAENDELEA SAA 9 ALASIRI
 
C. TEAM KUFURIKAA

Rasheeda akarudi tena kupewa chezo na Didie, ikawa kama sheria! Ukimwi umemjaa Rasheedah bila kujijua, siku ameamka asubuhi kwa Maringo anakohoa damu, Maringo akampeleka hospital wakampima majibu kutoka ameathirika! Mungu weee akajibu Rasheeda how?! Akajibiwa how. Akalaani hii hospital waongo naenda kwengine akajipeleka kwengine sasa aibuu! Majibu yale yale akapelekwa hospital kama 4 akapata majibu sawa sawa kama pa kwanza akaomba arudishwe nyumbani kupumzika.

Bwana Mzee akaenda jela jela, akamtoa Patric kwa kibali cha makamu wa Raisi, Patric haamini anaona kama movie akasahau hata kama Bwana mzee alichelewa kuja. Akapelekwa moja kwa moja kwa makamu wa raisi ambapo waziri wa mambo ya ndani na nje walikuwepo! Patric anaogopa haelewi akapewa mwongozo pale kuanzia leo tunakutuma nje ukatumikie taifa la nje ukiwa nje! Wewe na watoto wako na familia yako, hakuna kurudi uki mess up utapata so and so consequences!



Patric atakataaje! Akawa escotted mpaka ofisini kwa Bwana Mzee kupewa maelekezo ana masaa 36 ya kuondoka nchini! Wakawa wanongea na Bwana Mzee palee masaa kibao soku ikaisha akaambiwa alale pale pale afundishwe kazi

Maringo akaondoka kisiri siri akaenda kumwona Patric, kufika Patric hayupo anashangaa imekuwaje au amekufa akaambiwa hajafa ila hayupo mtafute kwenye simu akamtafuta kwenye simu hapatikani akajirudia zake home

Rasheeda akakumbuka ile statement ya Manoa kuwa atanifanyia kitu mbaya akauliza sasa how?! Sikulala na Manoa nimelala na Didie akampigia simu didie akamweleza hali yake, Didie akamwambia hata mie nimetoka kupima nimeambiwa nimethirika nipo hapa nimechanganyikiwa nahisi we umenipa miwaya! Rasheeda akachoka akakata simu haelewi ameupatia wapi mbona Patric alimwacha msafi!? Mmh haelewi kudadeki kwa hasira za kudumu na nini akachukua hela akaenda kununua AK47!

Akaenda kumtafuta Manoa akamkuta anafanya bonge la sherehe! Akamfuata waongee manoa akakataa akamlazimisha manoa akakubali akamnyea palee, Manoa akamwambia me sijafanya chochote labda ni mwanaume ulienae ongea nae vizuri Rasheeda akakomaa na Manoa manoa anaongea innocent kabisa maskini uuuwi! Rasheeda kwa hasira za kudumu akatoa bastola akamwambia me sifi kiboya boya akamchapa nayo moja usoni, watu waliokuwa kwenye party wakaskia wakaanza kukimbia, Rasheeda nae akatoka amemwacha manoa dead


Akaenda kumfuata Didie akamkuta amekaa kwa hotel, anakula mwenyewe akamvizia ametoka! Didie hana habari anatembea kwenda parking lot Rasheeda yupo kwa mbele akamwambia simama hapo hapo! Eh! Rasheeda what is it naaaw akajibu Didie put that gun down naaaw! Rasheeda analia umeniharibia maisha yangu we mngese nakuua leo me siwezi kufa mwenyewe!
Mh! Ikawa ngumu kumeza kwa didie! Akajaribu kuongea nae akawa anaona Rasheeda anatetemeka akainama chini Rasheeda akafyatua risasi ikampita Didie ikaenda kumpiga mtu wa nyuma Rasheeda akakimbia hakuangalia nyuma. Didie kuamka mamaa mama mama mama ni Ogaa, anamiminika midamu! Fighting for his life, akamshika mdogowangu oga wake up abeg! Watu wakajaa na mapolisi wakaingia, wakamwuliza akasema kuna mwanamke kamshoot anaitwa Rasheeda mapolisi wengine wakamfukuza Rasheeda wengine wakabakia kuzoa zoa maiti

Didie alilia kama mtoto mdogo hakuelewa how og alikuwa nyuma yake?! Ye anajua walishaagana muda sasa haelewi, Oga kapewa ya kifua upande wa kushoto kwenye moyo hamna kitu! Pigwa na wewe midamu nyang'a nyang'a!



Kukimbiza hospital Didie analiaje sasa! Madokta wakamwuliza vipi kuhusu ndugu yako hawezi ongea wakamwacha apoe kwanza wakamwambia tupe jina la ndugu yako akajibu sina ila wazazi wapo lagos, wakamtoa hospital wakampeleka nyumbani kwake akawa chini ya uangalizi wa polisi mpaka wazazi waje. Wazazi wakapewa taarifa wakajiandaa kuja kubeba mzoga wao OGa

Kwenye redio wakatangaza, oga raia wa nigeria amepigwa risasi na raia wa kizambia anaitwa Rasheeda, uuuwi Maringo akaskia, akampigia Luwi na Hachikoko wakajisalimisha kwa pilato polisi! Rasheeda mama yetu hatujamwona hii siku inaisha! Wakapewa kila kitu kutokana na mazungumzo ya Didie! Maringo analiaje wakawa wanampigia baba yao hapokei mara akaongia polisi tumetoka kupeleka mwili wa baba mm1 amepigwa risasi na mtu asiejulikana tulipoangalia kwa video camera ya nyumba alikuwa mwanamke, Luwi akauliza nani huyu baba akajibiwa manoa, uuuwi ganzi kwenye miguu! Akaanza kulia wakaja Hachikoko na Maringo wakaambiwa Manoa kauawa na mwanamke, kwa hasira wakauliza mwanamke gani kuonyeshwa picha mama yao, Maringo akazimia mikononi mwa Hachikoko kaka yake!

Rasheeda akajikimbilia mistuni mapolisi wanamtafuta raia wema wakaelekeza wakawa wanamfukizia na gari yete tupo na mguu na madamu usoni! Kimbia kimbia na wewe! Kufika mbele ni dead end kuna mteremko mkuuubwa sana! Mapolisi wakaja wakamwambia asimame akakataa akajiwekea bastola kichwani mkinisogelea najiua, wakajaribu kumtuliza hataki, waliposogea zaidi akajifunga risasi ya kichwa akaangulia kwenye dead end! Mapolisi wanashangaa!
Alfajiri kufika waka manage kuupata ule mwili wakapeleka hospital wakaenda kutoa ripoti central polisi, akina Luwi kuskia kilio mara 2! Wakalia weee lia lia na wewe!

Mary akawa amekaa zake nyumbani, mara akaingia mke wa Dereva, wakaanza kugombana, wanapigana piga na wewe, Mary na ule ugonjwa akazidiwa nguvu, akapigwa chupa ya kichwa akaanguka chini!
Mke wa Dereva akakimbia! Usiku sana saa 8 usiku akaja dereva anamkuta Mary amelala chini damu zinamwagika, akapiga simu polisi wakajaa pale wakamshikilia yeye kuwa ndio muuaji!

Akawekwa ndani Dereva kwa kosa la kutokukusudia! Mkewe akajikausha akaja kumtembelea Dereva akamwambia nimesingiziwa nimeua! Lakini sio kweli! Mkewe akamwambia pole bwana Mungu atakutetea utatoka tu jela. Akaondoka anamcheka kimoyomoyo kuwa to hell with my husband, now fyucha yangu itakuwa brighter!



ITAENDELEA SAA 5 USIKU LEO
 
Hehe jaman nyie si mlikuwa mnalalamika watu wengi hamwelewi?! Basi ngoja niwapunguze au sio?!



Meona ee



Dah poleni mabest me naumwa ivoo! Nitairusha baadae nikitoka hospital



Huwezi jua huenda picha ndo linaanza!
hahahaaaa basi sio kwa utamu huuuu
 
Back
Top Bottom