Tulituma muda mrefu sana ndani ya ile underground city, kunatisha sana kule chini hususan ukiwa alone au mkiwa wawili tu. Cha kushangaza kuna dada mmoja wa kirusi ambae tulikutana nae chini kule kule akizunguka zunguka mwenyewe (solo traveler). She joined our team tukawa watatu. Aisee yule dada nilimvulia kofia, haogopi na iliingia mpaka sehemu ambazo mimi nliona noma kuingia. alikuwa akituita kwenye mapango ambayo mtu utaogopa kuingia. Kwa kweli alituona kwamba sisi si kama yeye hivyo baada ya muda tukaachana nae. Baada ya kama masaa mawili hivi tuliamua kutoka kwa hiyo tour yetu kwa kivutio hichi cha kitalii ikawa imeishia hapo.
Kufika nje unafikizia kwenye maduka ya kununua vijizawadi kidogo. Nkasema ngoja tukaangalie kama kuna vitu vya bei nafuu tunaweza pata maana ki-kawaida zawadi tunanunua 2 days or a day before our flight ya kurudi. Katika pita pita zetu nkakutana na taa flani hivi za kuweka kwenye nyumba. Zile taa ni nzuri na nilidhamiria kuzinunua. Nlitaka 17 pieces ambazo zilitosha nyumbani kwangu na siku zikifungwa ntawaletea picha humu maana ni urembo mzuri sana. Mbeleni huko mtakuja ona kwamba nilifanikiwa kuzinunua.
Kufika kituo cha daladala ili turudi Goreme tukakutana na yule dada wa kirusi anaelekea kaymakli (ile sehemu nyengine yenye underground city). Tulipiga story mbili tatu pale na ndio nkapata lesson kwamba decision ya hayati rais Magufuli ya kusema hakutokuwa na lockdown wala masharti makali kwa watalii wanaotaka kuja Tanzania ilikuwa na faida zake kiuchumi. Huyu dada aliniambia kwamba nchi pekee alizoweza kusafiri ni Turkey au Tanzania. For her Tanzania was expensive, ndio maana akaamua kwenda Turkey. This means kama Tanzania ingekuwa somehow affordable basi angekwenda Tanzania. This was another lesson for me, pengine watunga sera wa Tanzania wanatakiwa waone hili, kwamba okey tunaweza opt kwenda na Quality tourism instead of quantity lakini nchi bado haipo na miundo mbinu ya kufanya Quality tourism. bado the number of tourists tunaowataka waje nchini ina mashiko sana. Baada ya muda kidogo daladala ikatokea hao tukarudi zetu mpaka kwenye junction ya kuelekea Goreme ambapo tuliamua kwenda kununua nguo za watoto. Nguo ki ukweli si ghali sana hapa japo baadae tulikuja gundua kwamba nguo zilikuwa bei rahisi zaidi kwenye mji uliofuata (Antalya). Ile ndio ilikuwa night yetu ya Mwisho Cappadoccia. Tulirudi Goreme around saa moja usiku na cha kwanza kabisa tuliamua kutafuta taxi driver ambae angetupeleka airport ya Kayseri kesho yake. Unajua kwa wenzetu watu si sana kuzungumza lugha za kigeni, unless uwe unajishughulisha na issue ambazo itakubidi ujue lugha hizo. The driver tuliyempata was a good person, alikuwa na appointment haswa maana asubuhi yake he was at our hotel ontime. He was knowledgable na alijua mambo mengi kuhusu Cappadocia ka Kayseri. Kwa kweli alikuwa very proffession na I recommend him kwa mtu yoyote ambae atafika Cappadoccia amtumie yeye. Haya ndio mawasiliano yake, japo kadi imeandikwa English spoken driver
😀 😀 😀
Tulispend time kubwa sana kwenye jacuzzi that night maana ndio hotel pekee ambayo tuli-book na ilikuwa na Jacuzzi.
Mapenzi yana-run dunia wazee, hii yote ni power of love. When you love you can go out of your way, mshairi mmoja wa kiarabu anasema "mpenda akipenda hutaka kutomuudhi na kumfurahisha ampendae". My wife deserves so much! Yaani ni ule msemo wa " A woman who does not ask for anything, deserves everything" na hawa viumbe wa hivi wapo wachache sana. Ndio rafiki yangu
Karucee once aliwahi niambia nimtunze sana huyu mwanamke and that's what I do and I am going to do for many years to come (as long as I am alive).
Safari ya kuelekea Keysaeri (ambao ni mji wa nne kwa ukubwa / kiuchumi nchini Uturuki) ilianza saa kumi kamili alfajiri iliyofuata. Ni mwendo wa lisaa moja speed 80 kwa saa. Around saa kumi na moja na nusu tukawa tumefika, checking in na procedures mbali zikafanyika na mpaka saa kumi na mbili na nusu tukawa tumetulia tunasubiri boarding. Around saa moja kama na robo hivi tuka-board na saa mbili hivi tukaruka. Tuliingia Antalya around saa nne na huu ndio ulikuwa mji wetu wa mwisho kabla hatujarudi tena Istanbul kuchkua ndege na kurudi Tanzania.
Until then....................................