My Corona relief trip and lessons therefrom

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,988
22,379
Mwaka ulikuwa mrefu sana, mipango mingi ikaharibika, kifedha wengi kati yetu waliathirika (tuweni pole sote).

Kama ilivyo kawaida niliyojipangia maishani mwangu, nitaacha yote lakini kila mwaka lazima niende holiday nje ya Tanzania. Hii ni ahadi niliiweka na siko tayari kuacha kuitekeleza ahadi (provided circumstances allow) hii kwa yule niliyemuahidi, same way alivyoniahidi kwamba hatoolewa na mtu mwengine yoyoyte zaidi yangu.

Uzi huu nauleta kwenu uwe ni inspiration kwenu na utoe elimu kwenu kuhusu Utalii, ni muendelezo wa nyuzi zangu na za watu wengine mbali mbali zinazohusu utalii na kusafiri huku nikiamini kusafiri ni hobby ya watu wengi sana duniani. Uzi huu kwa kuwa utakuwa ni mrefu basi ntauandika hatua kwa hatua na wale wapenda story basi tuvumiliane.

Mnamo katikati ya mwezi Oktoba 2020, iliwadia tarehe yangu ya safari ambayo mwaka huu nilikuwa naelekea nchini Uturuki/ Turkey. Ipo nyuzi moja nzuri humu iliyoandikwa na ndugu yangu isajorsergio kuhusiana na nchi hii, japo wakati uzi ule unaandikwa nilikuwa tayari nimeshafikia maamuzi ya kwenda Turkey, but nikiri nao ulichangia kunifanya nijue ninachokwenda kukifanya kule.

Ndege yetu ilikuwa inaondoka saa tatu kasoro usiku pale JKIA, tulifika mapema sana mnamo saa kumi na mbili kamili maana tulijua protocal za kusafiri zimekuwa complicated kutokana na janga zima la corona. Taratibu zimebadilika, a lot of paperwork need to be done pale airport and so on and so forth. Check in ilifanyika vizuri, na watu wa airport security wakatukagua na kutuhoji na kuturuhusu.

Nilichukizwa na maswali yao ambayo kiukweli hayana msingi wowote na ni aibu kwao, kwangu mimi nawaona wamekariri maisha. Hebu fikiria mtu anakuuliza una kiasi gani "in cash"? (na ni kwa sababu tu umemwambia naenda Turkey kutalii) unamwambia nina enough amount, hapo ameshakagua hotel documents zako, visa, insurance, almost everything na bado anakwambia naweza jua ni kiasi gani au unaweza nionyesha?? Huu ni ushamba wa hali ya juu!

Anajitetea eti tunafanya hivi kwa sababu hatutaki waTanzania wasafiri kama hawawezi kusafiri (financially), kwa sababu athari zake ni kubwa kwa taifa. Unajaribu kutaka kumuelewa maelezo yake lakini ukifikiria zaidi na zaidi unaona bado hawa watu wapo kwenye dunia ya ujima.

Baada ya hustle mbili tatu na maswali haya tunafanikiwa kugongewa exit stamp na Immigration officers na tunakuwa rasmi tumepata ruhusa ya kutoka nchini na serikali.

By saa mbili na nusu watu tuna board na saa tatu kasoro juu ya Alama ngoma inaondoka.

Naomba tu nikiri hii ni mara yangu ya kwanza kupanda Qatar airways na hakika hili shirika linastahili kuwa ni best airline hapa duniani. Qatar airways ni 5 star airline company maana huduma zake, facilities zake na hata sterwardess wake wako next level kabisa.

Baada ya masaa 8 tukajikuta tupo Hamad Internationla airport (Doha), tukawa transit pale kwa masaa mawili tu na ilipofika saa kumi na mbili tukaanza safari ya kuelekea jijini Istanbul. Watu wameendelea haswa, inashangaza sana hawa viongozi wetu wa kisiasa huwa wakienda hizi safari za kikazi huwa wanakwenda kujifunza nini?? Au ndio safari za nje sasa hazipo?

Mnamo majira ya saa sita au saba mchana hivi tulitua Ataturk/Istanbul International airport, moja ya jambo nililojifunza almost kila nchi niliyotembelea ni kwamba, law inforcement officers wanaokuwepo site be it immigration officers, police, tourism polices, soldiers, correctional officers ni vijana wadogo wadogo tu tofauti na huku kwetu ambako utakuja traffic police ni jitu lina mkitambi huo unakaribia kupasuka, aged na hawataki kutoka site. Sijui kwa kuwa site ndio kuna pesa zaidi za kuwadhulumu wananchi au vipi?

Nchi za wenzetu huwezi kuta officers waliokuwepo site wakiwa aged. Ni young fellas (men and women).

Tulichukua taxi kuelekea hotel kwetu mitaa ya Sultanahmet area ambako ni European side ya jiji la Istanbul, kwa wasiojua ni kwamba jiji hili ndio huyagawa mabara mawili ya Europe na Asia na European side ndiko ambako kuko much developed na most of hotels and tourist attractions zipo huko. Taxi ilitugharimu TL 180 ambazo ki kama TZS 50,000 hivi na ni mwendo wa saa moja na dakika 15 wakati wa foleni. Bahati mbaya sana kuna mida ikifika (ya foleni) magari private na taxis zinakuwa haziingi kule eneo yalipo mahotel mengi kwa sababu Tourism polices wanajaribu kuzuia misongamano maeneo hayo. Tulishushwa kaika kituo cha Tram na ikabidi tu-pull begi letu mpaka hotel ambayo ilikuwa about 5 minutes away.

Tunafika hotel tu na mkasa wetu wa kwanza unaanza...

Alamsik!
 
Wakati tunasubiri muendelezo tuoshe macho kidogo
cb46f5aa2385a3e3bcf4676273f4c038.jpg
4557edd8ede1c029ba4ed4a8bf9ad594.jpg
 
Safi sana. Kuwa maskini kuna tufanye wengi tuone kutalii ni jambo la hovyo lakini ni jambo ambalo lina umuhimu wake na thamani yake kwenye maisha.

Hongera sana
I take it positively!
Ni kweli mkuu. Lakini sio kuwa maskini tu Bali hata kukosa elimu ya utalii.

Fuatana nami, nadhamiria kuainisha gharama zote tulizotumia juu ya safari hii
 
Safi sana na hongera! Kwa kuiwakilisha JamiiForums na taifa kimataifa. Shukrani pia kwa kutambua mchango wangu katika safari yako, naamini wengi tu/watajifunza juu ya Uturuki.

Ülker umenibebea? 😎
Shukran mkuu!

You are the best Joh.

Nimekubebea mwanangu, naachaje yaani?? Next time I come over there ntakudondoshea
 
Alamsiki tena!

Khaa....ishakuwa hadithi za Akajasembamba! Inaendelea wiki ijayo😆
Series episodes zinafuatia!

Everyday is Saturday............................... :cool:
Hahahahahahaahahah

Mkuu, tunapokuwa na free time tu ndio tunaandika aiseee. Tuna majukumu ujue
 
Back
Top Bottom