Alfajiri na mapema jua lishachomoza, yaani saa kumi na mbili kasoro mwanga tayari unapita dirishani. Mimi na mwanga hatupatani kabisa, nilikuwa nakereka sana! This was holiday and I wanted to always sleep long.
Jumamosi ile ikiwa ni siku yetu ya tatu pale Istanbul tulidhamiria kwenda Galata tower ambapo of course tungekatiza Galata bridge, taksim square (kinaponukaga always) na Dolmabahce palace. Safari ilianza around saa tano asubuhi na ni walking distance tu from our hotel. Ilituchkua about 25 minutes kufika pale.
Turkey inayo historia flani kuhusu Christianity. Kabla ya Ottoman empire, niseme tu Uturuki ilikuwa ni himaya ya Wakristo kwahiyo majengo na mambo mengi kuhusu Istanbul yalifanywa na kumilikiwa na wakristo. Galata tower ilitengenezwa kama Christea Turris (Tower of christ) mwaka 1348 wakati wa upanuzi wa colony la Genoese ndani ya Constantinople. Galata tower hapo mwaka 1348 lilikuwa ndio jengo refu zaidi pale Istanbul na hii tower ilikuwa na urefu wa mita 66 tu. Yaani by 13th Century watu duniani tayari wanajenga majengo marefu haswa, funzo nililolipata ni kwamba, politically tukitaka kujifannaisha na mataifa makubwa duniani tunahitaji kuangalia mambo mengi sana. May be sio busara sana kujifananisha na mataifa haya kwenye mijadala yetu japo hii haiwezi kuwa excuse kwa under-achievement zetu kwenye mambo yetu.
Galata tower
Beautiful View from Galata tower.
Ndani ya Galata tower kuna restaurant nzuri ambazo one can opt to have some tea/coffee or icecream. It is a museum with a lot of history of Byzentine as a state na kutekwa kwake by Ottoman empire.
The below is the picture inside Galata tower. Hiyo ni minyororo iliyotumika kama zana ya kivita kipindi hicho, ilifungwa kutoka one point to another point along bosphurus area kuzuia meli za kivita za maadui zisikatize eneo hilo.
Baada ya kumaliza tour hii safari ya kuelekea Taksim square ilianza. Hii ni sehemu ya kihistoria sana ndani ya Uturuki na kama nlivyosema kikitaka kuwaka ndani ya nchi hii maandamano yote huanzia hapa.
Ni square kubwa kwa kweli, safi na imetunzwa vyema. Central station ya Metro network ya Istanbul ndio inaanza hapa. Ni underground train system inayotumiwa na watu kama usafiri. Foleni zote za dar zingekupungua kwa mifumo kama hii ya metro lakini tuwe tu wakweli, mataifa yetu ya kiafrika yatafikia maendeleo haya labda 50 years from today. or even 100 years from today.
Hapa ndipo yalipotokea yale mauaji maarufu ya watu wanaoitwa leftist demonstrators hapo Mei mosi 1977. Waliokufa ni watu kati ya 34-42 na walioumizwa walikuwa kati ya 126-220. Kujua zaidi nenda google ukajifunze.
Limegeuzwa ni eneo la kihistoria na kitalii pia. Na kuna monument kabisa imewekwa pale kuwaenzi wapigania uhuru wa Turkey.
Kutokea Taksim square sio mbali sana na ulipo uwanja wa mpira wa klabu maarufu ya Basiktas. Kwa vile mimi ni mtu wa mpira, ilinilazimu kumalizia siku yangu hapa. Unfortunately ni kipindi cha corona na viwanjani hawaruhusu washabiki kuingia. Ilibidi niishie tu nje na niendelee na safari yangu kuelekea Dolmabahce palace ambalo lipo hapo hapo tu. Hili ni miongoni mwa majumba makubwa ya makazi ya wafalme wa zamani. Hapa ndipo palikuwa makazi ya wafalme wapatao 6 kuanzia 1856 na kuendelea mpaka 1924.
Mfalme wa mwisho kuishi kwenye hili Palace aliitwa Abdulmecid Efendi, kuna sheria ambayo ilitungwa mwaka huo na kuifanya hii palace kuwa National heritage of a new Turkish Republic. Baada ya kufika hapa nkamwambia mke wangu, angalia namna watu walivyoishi na familia zao, na leo wako wapi?? wote wamerudi ndani ya tumbo la ardhi, walikuwa ni wafalme wenye nguvu na mamlaka. Kama walitenda mema sasa hivi wanapokea malipo yao na kama walitenda mabaya sasa hivi wanapokea malipo yao.
Maishani hakuna haja ya kujikwaza, kuwa unavyokuwa lakini mwisho wa siku tunarudi ardhini. Unapata hisia kali sana juu ya Maisha na kwa watu wa dini basi unapofikiria mambo kama haya, kuna kitu una-gain kwenye suala zima la spiritual life.

Jumapili murua, nililala nikapitiliza. Kiupande flani hii ilikuwa ni fursa ya mimi kulala nitakavyo maana I was on a holiday, lakini kwa upande wa pili nilidhamiria kutembea haswa maana hiyo pia ilikuwa ni sababu mojawapo ya kuwaacha "madogo" Tanzania. Saa tatu ilifika haraka, breakfast mwisho saa nne asubuhi. Wife ananiambia fanya tutoke tuelekee restaurant tukapige breakfast. Saa tatu na nusu sharp tuko kwenye breakfast table na as usual mwendo ni ule ule, sausage moja, matunda ni zabibu tu kidogo pamoja na apple 1, yai moja la kuchemsha, mikate as many as you want na vimikate vyao vitamuuu vya kituruki. Kama kawaida nakula kiafrika sio kizungu but kwenye mikate ni mimi na siagi tu, Nutella, chocolate syrup, honey, na vitu hivyo vyote narudisha tu wala hatutumii.
Hii ndio siku tuliamua kwenda kutembelea Basilica cisterns, Grand Bazaar na Sulaymaniye Mosque.
Basilica cisterns: Cistern ni eneo ambalo hujengwa au huchimbwa ili kuhifadhia maji, mara nyingi hutumika kuhifadhia maji ya mvua na mara nyingi eneo hili linakuwa linawekwa/ kujengwa chini ya ardhi. Basilica cistern ni cistern iliyo takriban mita 150 tu kusini magharibi mwa museum ya Hagia Sophia, cistern hii ilijengwa karne ya 6 wakati wa utawala wa Byzentine na makala za kale zinaeleza kuwa watumwa wapatao 7000 walishiriki katika ujenzi wa Cistern hii. Leo hii halitumiki tena kwa kazi hiyo, na limebaki kama kivutio cha utalii tu.
Cistern hii ipo chini ya ardhi kiasi ya mita 20 kushuka chini ya ardhi, eneo lake ni mita 138 urefu wake kwa mita karibia 65 upana wake (huko huko chini ya ardhi). Wale wenzangu na mimi ni kwamba, eneo hili ni kama kiwanja cha mpira wa miguu kimoja na nusu. Maajabu ni kwamba eneo hili lilichimbwa na binaadamu wa enzi ambazo hakukuwa na makatapila wala hizi mashine kubwa kubwa za kuchimbia kipindi hicho cha karne ya 6. Ceiling ya hii cistern imekuwa supported na nguzo zenye urefu wa mita 9 kila moja, ambazo zimewekwa katika rows 12 za column zipatazo 28 na kila nguzo imewekwa umbali wa mita 5 kutoka nguzo nyengine. Ni maajabu wakuu na ili kuyaona vizuri inakuhitaji ufike eneo hili ili ujionee mwenyewe.
Baada ya kutoka Basilica, tuliamua kuelekea Grand Bazaar, utakachoambiwa mitandaoni kuhusu Grand Bazaar ni mazuri matupu, ni eneo moja lililo under one roof likiwa na maduka zaidi ya 4,000. Yes maduka zaidi ya 4,000 na mitaa isiyopungua 60. Soma tena mkuu, maduka zaidi ya 4,000 na mitaa isiyopungua 60 ndani ya eneo moja (under one roof area). Eneo lake la mraba ni square meters 30,700 na katika hali ya kawaida eneo hili hutembelewa na wageni kati ya 250,000 mpaka 400,000 kwa siku. My audience, you haven't just read something as a mere story, you are reading something real. Utachkua masaa zaidi ya matatu kuzunguka humu ndani kuangalia vitu mbali mbali.
Ndani ya Bazaar hii kuna kila aina ya bidhaa, kuanzia electrical items to ornaments, clothes to souvenirs, vipochi, glasses, mikanda, viatu, mabusati na mazulia, mashuka and everything. Moja ya jambo baya kabisa ndani ya eneo hili ni kwamba things are over-priced, vitu ni ghali mno, ukitoka nje na kwenda maduka ya kawaida ambayo yapo labda 20 meters outside the bazaar utakuta bei ziko chini sana. Halafu pia things are super negotiable, usiogope ku-bargain ukiwa humu aisee. Kitu unanziwa Lira 450 kumbe ukipata unaweza ukakipata kwa Lira 75. Si mchezo sheikh wangu jamaa wanajaribu bahati zao, wakikipata kichwa wanakiramba haswa. Mentality yao ni ya kushngaza kidogo maana baadhi ya wateja ukiwatajia tu bei kichaa kwa baadhi ya bidhaa bsi huondoka. Wao hawajli wewe kuondoka lakini wanajaribu bahati yao.
Moja ya tabia zao mbaya kabisa wauzaji wa maduka yaliyomo Grand bazaar ni kujaribu ku-set bei based on Nationality ya mnunuzi, yaani sisi waafrika wanakupuuza au kukupa bei halisi kiasi, wanapenda sana kujifanya friendly kwa hiyo ukifika tu utaskia "welcome habibi", how are you??? "where are you coming from habibi"??? Ukiwajibu tu natoka U.S, au lets say natoka Qatar au U.A.E jiandae na price kupanda. Ila ukiwaambia natokea Tanzania, watakuuliza "Africa"???? Ukiwajibu yes yes basi utaona wananywea na kutokukupa ile attention kama wateja wengine.
Sisi watu wengi walikuwa wakidhani tunatokea nchi za middle east, mara nyingi wanatuuliza, Oman???? are you from Oman habibi?? Najua kwanini walikuwa wanatuhusisha na nchi hizi na kwa kweli inaleta feelings mbaya sana.
Hatukukaa muda mrefu sana maana tulishaona kila tunachouliza basi bei juu. Moja ya zawadi nlitaka kununua ni mkanda (trouser belt), huwezi amini eti mkanda wa kawaida kabisa jamaa wanataka kutuuzia lira 150 ambazo ni sawa na karibu TZS 44,000 na ni mkanda wa kawaida tu, kwa kweli tuliamua kusepa.
By this time njaa ilikuwa tayari na tukaamua kuelekea restaurant yetu bora kabisa Chef Esmer Cafe kwa ajili ya mlo. Aisee wadau hii restaurant kama ikitokea nafika tena Istanbul basi its a place on my priority list. Hebu cheki mlo huo aisee.
Hiyo sahani inagharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania 15,000 na ukiongezea na soda ambayo ni TZS 3,000 basi burdaani wakuu.
Kufikia saa kumi jioni tukaelekea Sulaymaniye mosque kwenda kumalizia siku yetu. Hii ikumbukwe kuwa tulikuwa sasa tushakaa siku 4 na tumebakisha siku moja tu kuwepo pale.
Sulaymaniye mosque ni msikiti ulioanza kujengwa mwaka 1550 na kukamilika mwaka 1557, msikiti huu ulijengwa na mfalme Sulaymaniye wa Empire ya Ottoman sio yule king Solomon wa kwenye bible au mtume suleiman wa kwenye Qur an. Huyu alikuwa ni Mfalme wa Ottoman Empire na ilikuwa ni karne ya 15 tu hapo.
Sulaymaniye mosque ipo kwenye third hill ya istanbul na unapokaa katika baadhi ya maeneo nje ya msikiti huu unaipata vizuri sana view ya Bosphurus. Mimi binafsi ninaposafiri hupendelea sana kufika kwenye miskiti ya mji husika kutokana na Imani yangu na hupenda angalau kuswali ndani ya miskiti husika maana I fell aproud to have got a privilage to prostrate in different parts of the world. I feel aproud to bend and put my forehead in different lands in this world so utaona mara nyingi sana niko radhi kuelekea somewhere during my holiday where I could go and do so.
Huu msikiti ni miongoni mwa miskiti mikubwa pale Ututruki ukiwa na eneo kubwa na design nzuri ndani na nje. Utashangaa hawa jamaa walikuwa na utaalam kama huu karne ya 15 huko, no wonder they are where they are right now.
Apart from many other areas ndani ya msikiti huu, kuna library ambayo kuna professor mmoja anakaribisha watu wanaotaka kuuliza mambo mbali mbali kuhusu Uislam na msikiti ule specifically. Had a very good chat with the guy and he encouraged me to go and do my master's degree in Turkey na kama nikitaka anaweza kunisaidia kuhusu scholarship. Unfortunately, Turkey is not one ofthe country I have in mind for my master degree, I will take my chance and pass the opportunity. Hizi sometimes ndio minongoni mwa fursa mtu unaweza kutana nazo unapotembea.
Siku ilimalizaika na hakukuwa na cha muhimu zaidi ya usingizi kwa muda ule, super tired. Kuna baadhi ya wadau watauliza, "vipi mkuu ulikuwa huli mzigo""?? Mbona hutuambii??? Hahahahahah the answer is, we had fun!
Kesho yetu ndio siku ya mwisho ya kuwepo istanbul kabla ya kurudi tena for our last night before flying back home.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.