Jumaanne tulivu ilikuwa imefika, siku zangu za kukaa Istanbul kwa mujibu wa itinerary yangu zilikuwa zimemalizika na ingenibidi tu kuondoka na kuelekea Ankara. Kiukweli sikufanikiwa kutembelea baadhi ya sehemu kama nilivyopanga lakini kwenye maisha nimefunzwa kuridhika na ninachopata.
Sehemu ambazo sikupata kutembelea ni pamoja na Topkapi Palace, Istanbul Archeological museum na sikupata kufika Fenerbahce kwa Samatta.
Ankara ndio mji mkuu au mji wa kiserikali wa nchi ya Turkey. It was my first time kupanda hizi treni za mwendokasi, wanaita high speed trains. Nilitumia shirika la serikali ya Uturuki liitwalo TCDD. Kutokana na ukweli kwamba kuna ubaguzi juu ya ngozi nyeusi duniani huwa mambo yangu nayafanya kwa ustadi mkubwa sana niwapo nchi za watu. Niliamua kukata business class ambako obvious kungekuwa na watu wachache tu unlike economy classes, in terms of toilets hata watumiaji pia tungekuwa wachache na ingeepusha kuchukuliana poa, na ni imani yangu pia watu wanaosafiri kwenye business class of first classes wanakuwa ni watu wa upper class in a community so hata kiwango chao cha ustaarabu kinakuwa tofauti.
Saa nne kasorobo juu ya alama tulikuwa tumeshaingia ndani ya train na tushapata seat zetu, COVID-19 measures were in place na social distancing was one of them. Tulikaa seat za mbali mbali kidogo lakini katiba row moja so tulikuwa tunaonana from side ways. Hii ilimpa wife muda wa kulala na mimi muda wa kutosha wa kushangaa mandhari nzuri sana ya nchi hii ya Uturuki.
Ni mwendo wa masaa manne na nusu wenye kukava kilometa kama 218 hivi. Mnamo saa nane na nusu tulikuwa Ankara gar station (kituo kikuu cha train pale Ankara, baada ya kutoka tu ndani ya train tulifuatwa na askari ambao walikuwa wamevalia kiraia na kutuonyesha ID zao na wakataka tuwape passports zetu. Bila kusita na wala kuuliza maswali mengi nilitoa passport zote nikawapa, mmoja akazipiga picha kwa simu yake na akazituma somewhere through Whatsapp na mwengine akawa anatuuliza friendly kwamba tunafanya nini tunategemea kukaa muda gani Ankara and questions like that, tulijibu kila swali na baada ya dakika chache tu tulipewa passport zetu na jamaa wakatuambia "Enjoy your journey"
Nisiwe muongo, kiukweli nlichukia sana kwamba out of all passengers, kwanini wale askari walitufuata sisi tu??? na walionekana kwamba walijua hata kabla ya treni kufika kwamba kuna waafrika wawili ndani ya train. Hii ilinifanya kujiona mnyonge sana. Nafahamu kwamba ni procedures lakini why kwetu tu??
Baada ya dakika kumi hivi tulikuwa nje ya station na namna palivyo pale kupata taxi mfumo wake ulituchanganya kiasi, ilibidi tutembee kwa mguu mwendo wa dakika kama tano hivi na tukakuta kituo cha taxi ambapo tulichkua kuelekea hotelini kwetu.
Tulifikizia hotel inaitwa "Cinnah" ipo city centre kabisa na nadhani ni karibu kabisa na Ubalozi wa Marekani. Usiku huu kulikuwa kuna game ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE nadhani PSG vs MANU, aisee nilihangaika kuitafuta hii game sana sana sana tu ila hawa jamaa sijui ndio uzalendo au ushamba, hawaonyeshi hizi game. Kwanza hawatumii DSTV kabisa ilibidi tu nijirudie hotel nilale huku nikiwa sina furaha.
Unfortunately, Ankara tulipanga kukaa siku moja tu maana kama nlivyosema huu ni mji wa kiserikali zaidi, sio mji wa kitalii. There is not much to see to be honest.
The next day was gonna be our trip to Cappadocia, beautiful place to be in Turkey. Lets meet then............................