Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,976
- 22,409
- Thread starter
- #21
Miss,Ndo imeisha?? Aya ngoja nijibebeleze nilale
Nakusalimia!
Miss,Ndo imeisha?? Aya ngoja nijibebeleze nilale
Ni tram by the way.Train zinafanya route kama daladala au mwendokasi. Lakini pia njia zake zinakatiza kwenye barabara za lami mitaani ambako magari ya binafsi na mabasi ya abiria mjini yanapita kama picha zinavyoonyesha.View attachment 1627190View attachment 1627191View attachment 1627192View attachment 1627193View attachment 1627194
Now nimerudi kuendeleaKwahyo mkuu utarudi saa ngapi kumalizia?
Najua alimaanisha Tram na sio train.asante sana Drizzle nimeelewa kuwa ulimaanisha Train na siyo Tram
Kwamba haujui kuwa kuna limit ya kiasi ambachi unaweza kusafiri nacho kama cash?Nilichukizwa na maswali yao ambayo kiukweli hayana msingi wowote na ni aibu kwao, kwangu mimi nawaona wamekariri maisha. Hebu fikiria mtu anakuuliza una kiasi gani "in cash"?
Relax mkuu.Shida stori mnaileta Kama mnauza leta stori hata kama ina parts usichelewe sana.Naona Hii imekua trend na stori haiishi!
Baada ya masaa 8 tukajikuta tupo Hamad Internationla airport (Doha), tukawa transit pale kwa masaa mawili tu...
Yeees! Asante 😋Shukran mkuu!
You are the best Joh.
Nimekubebea mwanangu, naachaje yaani?? Next time I come over there ntakudondoshea
Haha true bro! Sema suspense ndio shida!Relax mkuu.
Life is not that tough
Istasyon walichokufanyia ni tabia ya Kituruki sasa... Pole.Nakumbuka nilipopata tu wifi connection pale airport ya Istanbul ziliingia email kwenye account ya wife ambayo ndio tuliitumia ku-book some hotels pale Istanbul ikimtaka a-verify card details zake au abadilishe details hizo maana wanashindwa kuichaji. This email was from booking.com maana tuli-book hotels kupitia wao.
Nilishangazwa na email ile lakini nikaamua kuweka na details za kadi yangu pia. Si unajua tena ugenini and tumechoka so I wanted not to take any risk with not being somewhere I wanted to be for the bigger part of the year.
Sasa tulipofika hotel yetu tukamkuta receptionist, anatuambia hotel room yenu tumei-cancel, what???!!!!!! Why?? The told us we couldn't reach you over the phone (Tanzanian number) and we tried to charge the card but it wouldn't go through na Leo si ndio check in date. Kwahiyo tukawatumia email (through booking.com) kwamba mtoe card details nyengine na baada ya 2 hours without response ikabidi tu-cancel reservation yenu na tuuze hii room ili isije ikawa hasara kwetu.
Understandable, right guys?????
Jamaa akaendelea, "but relax, tutawapeleka kwenye our sister hotel and you will stay there kwa bei ile ile mliolipia kwetu"
Sikutaka hata mjadala nkawaambia okey twendeni and I had already made my mind that ninachotaka sasa ni kulala tu. Wakatupeleka kwenye hotel just jengo la tatu tu. Kufika zipo hotel mbili hapo hapo, jamaa akatuambia chagueni mnayoitaka. Nkaangilia rooms zao then nkachagua moja. Baadae nlichokuja gundua ni kwamba, huu ni mchezo tu haya mahotel yanacheza. Ile hotel ya kwanza ambayo nilibook ikiitwa Istasyon hotel ni nzuri na watu wengi wanaipenda, so all the time wanatafuta tu sababu za kisheria zitakazowapa wao fursa ya ku-cancel reservation yako na ukifika wanakupeleka kwenye hotel zao nyengine ambazo online haziuzi sana huku wakijua most of the tourists wakifika pale wanachotaka ni kupumzika tu kwa hiyo 95% watakubaliana na hoja zao na kukubali kukaa hizo hotel nyengine. Remember, wanatafuta sababu ambazo kisheria zinawalinda. Hahahahahaha! Stupid them
Baada ya kupumzika kidogo tukatoka kuelekea restaurant kupiga mlo, hapo ni around saa kumi na moja jioni, tukarudi na kupindua kidogo. Tulilala mpaka around saa mbili hivi then tukatoka kwenda kuranda kidogo.
Beautiful garden we found, just by the ocean and where people sit and chit-chat. Relaxed there for two hours and our day ended just like that.
Siku iliyofuata ilikuwa ni ijumaa. Ratiba yetu ya kukaa Istanbul ilisema tutembelee maeneo yafuatayo
1. Hagia Sophia museum
2. The blue mosque museum
3. Topkapi palace
4. Hippodrome of Costantinople
5. Basilica Cisterns
6. Suleymaniye Mosque
7. Istanbul archeology museum
8. The grand bazaar
9. Galata bridge and galata tower
10. Taksim square
11. Dolmabahce Palace
12. Fenerbahce stadium (hii ilikuwa kumpa heshma yake el capitano- Samatta).
Around saa sita mchana ule tulitoka na kuelekea hagia Sophia, nilidhamiria kuswali swala ya ijumaa pale kwa sababu ijumaa ile ilikuwa ni ya 4 au ya 5 tangu this museum ilipofungulia tena as a mosque baada ya kufungwa kwa zaidi ya 80 years.
Hagia Sophia au Turkish Ayasofya au kwa kilatini Sancta Sophia au pia unaitwa Church of the holy / divine wosdom is an important Byzantine structure ndani ya Istanbul na pia ni moja ya greatest monument in the world. Ilijengwa kama kanisa la wakristo in the 6th century (532-537) under the directives of Byzantine emperor wa kipindi hicho , Justinian I. Baadae it became a mosque mwaka 1453 chini ya Ottoman empire sultan Mehmed II na kubaki hivyo mpaka 1934 ilipokuwa securalized. Mwaka 1935 ikawa museum na mwaka huu 2020 serikali ya bwana Edorgan kupitia mahakama kuu ya Turkey ikaurudisha kuwa msikiti tena. Hilo lilinifanya nikaweka dhamira kwamba lazima nikaswali pale japo swala moja ya ijumaa.
It was a beautiful experience and I learned a lot. Nilijifunza kwamba waislam Sisi wa huku Africa mashariki tuna-practice uislam unavyostahili kuliko wenzetu wa kule. Sisi no conservative muslims na jamaa ni modern/liberal muslims. Dada anaswali na skin tight na hana wasiwasi, masela wanaswali na bukta tu na hawana wasiwasi, watu wanaswali kama wanakimbizwa. Dakika 0 amesharukuu, mara ka-postrate tayari yaani harakahharaka kama anafukuzwa. Nilijisemea kumbe bado Sisi tuna uafadhali mkubwa sana juu ya namna tunavyo-practice dini zetu.
Baada ya swala tukapata fursa ya kuingia ndani ya msikiti, aisee utashangaa technology iliyotumika. Ukijaribu kufkiria kwamba this was built in 6th century na engineers walikuwa deep kiasi hiki back then unabaki kustaajabu tu.
View attachment 1627307
Mengi ya kujifunza ndani ya museum hii maarufu duniani. Either go to Google or go to Istanbul maana nkiweka hapa kila kitu huu uzi utakuwa mrefu mno.
Out of this mosque there is a beautiful gardens, restaurants, tourism polic wa kutosha kuhakikisha usalama wa watalii, mbwa wa ulinzi na hali ni shwari kabisa unlike in our countries ambapo maeneo ya kitalii machafu balaa, hakuna ulinzi wa kutosha kwa watalii, hakuna migahawa yaani vurugu tupu. Nliwahi kwenda Saadani national park, ilibidi twende kijijini kule kwa mamantilie ndio tukale au tununue biscuit na Tanga fresh kutoka duka la kijiji pale.
Tulimaliza tour yetu ya Hagia Sophia na kuamua kuunganisha Blue mosque kabisa. Huu ni msikiti ambao uko pale pale karibu na Hagia sophia. Unaitwa hivyo kutokana na tile zake surrounding the walls of the interior designs kuwa ni za blue. Msikiti huu ulijengwa na mfalme au sultan Ahmet kati ya mwaka 1609-1616. Miongoni mwa sehemu zake kuu ni eneo alilozikwa sultan Ahmet na Madrassa iliyomo mule ndani msikitini and other areas like kitchen and library etc.
Mpaka Leo msikiti huu unatumika kwa matumizi ya ibada kwa waislam lakini pia unatumika kama tourist attraction. So it is closed for non muslims worshippers for 30 minutes before every prayers in a day.
View attachment 1627342
Mpaka tunamaliza tours hizi mbili tu tayari ilikuwa ni around saa kumi na moja jioni. Kilichofuata ni kutafuta restaurant na kwenda kujilia vyetu hahaahhahah.
Siku hii tuliporudi hotel ndio jamaa akatuelekeza restaurant za high end maana tulimwambia jana tulikula chakula hakukuwa standard ile. Nlipoona hatufahamiani vizuri akaamua kutupeleka restaurant inaitwa chef esmer restaurant aisee hapo ni balaa. I recommend everyone ambae atapata kufika Istanbul aende hapo akapige msosi. Chakula kizuri mno yaani first class pamoja na soda unapata kwa TL 60 ambazo ni sawa na about TZS 18,000/=
Siku ilimalizika hivyo na tulikuwa excited and looking forward for our next day there.
Baadae kidogo tutaendelea......
Sasa yeye hakuuliza katika mnajili huo.Kwamba haujui kuwa kuna limit ya kiasi ambachi unaweza kusafiri nacho kama cash?
Acha mbwembwe mzeeSasa yeye hakuuliza katika mnajili huo.
Yeye aliuliza kana kwamba hatuna kitu.
Na nlipomwambia amount ndio akaanza kujibaragua kwamba we have to make sure Tanzanians out there do not suffer or get into trouble because of finances. Hiyo unaleta taswira mbaya kwa taifa na inashusha hadhi ye JKIA kimataifa (in best airport in the world)
Kwa kweli aiseeeeHaha true bro! Sema suspense ndio shida!
HahahahahahaahIstasyon walichokufanyia ni tabia ya Kituruki sasa... Pole.
Karibu mkuu.Acha mbwembwe mzee
Unajikuta mturuki sio 😂Karibu mkuu.
Umekaa kama wewe ndio yule mlinzi 😀😀😀😀
Sio wahuni kivile, sema kunatabia za KiSwahili! Kwa kuwa ni Waturuki itoshe kusema tabia za Kituruki Turkey.Hahahahahahaah
Jamaa wahuni wahuni sio???
Endapo ungelisema huna pesa, sifahamu labda angekupatia usipate shida ughaibuni.Sasa yeye hakuuliza katika mnajili huo.
Yeye aliuliza kana kwamba hatuna kitu.
Na nlipomwambia amount ndio akaanza kujibaragua kwamba we have to make sure Tanzanians out there do not suffer or get into trouble because of finances. Hiyo unaleta taswira mbaya kwa taifa na inashusha hadhi ye JKIA kimataifa (in best airport in the world)