RealMan
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 2,367
- 1,388
RealMan,
Kuhusu wezi ni tatizo ambalo linaweza kudhibitika. Namna gani utadhibiti wezi ni kuwa lazima uajiri mlinzi ambaye atakuwa anakulindia wakati wa usiku, kama unavyojua huu ni mradi na unahusisha pesa nyingi za uwekezaji hivyo ni muhimu wakati unapanga bajeti ya huo mradi wako ukajumuisha gharama za mlinzi.
Kuhusu kufugia mikoani hakuna shida yeyote kwani wakati wa kuuza utakodi canter na utawapakia mbuzi wako tayari kuwapeleka sokoni Dar au kwenye miji mikubwa. Gharama za usafiri ni ndogo sana kwa kila mbuzi na mara nyingi huwa haizidi tshs. 5000/= .
Kama utaona kufugia mikoani kutaongeza gharaza za usafiri au labda siyo mzoefu kwenye usafirisha wa wanyama na kwenda kuwauza Dar unaweza ukatafuta shamba Mkuranga au Babagamoyo ambako wafugaji wengi nimewasaidia kuwaanzishia miradi yao ya mbuzi na Kuku huko na kwamba hali ya usalama ni kubwa tu ukilinganisha na maeneo yaliyo jirani zaidi na Dar.
Hakya nani kiongozi kunako majaaliwa mwakani mbuzi wa maulid/chrismas/idd utamtoa kwangu.
Nina maeneo makubwa Mkoa Mwanza labda nifanye utafiti wa ziada kujua wasafirishaji wanalipa kiasi gani kufikisha mbuzi mmoja Dar..
Wazo la kupata shamba mkuranga ama bagamoyo lina mantiki zaidi kwa maana ya usimamizi wa karibu ingawa bei ya mashamba maeneo haya imekwenda juu siku za karibuni.
Kwa kifupi nimesha shawishika 100% kufanya ufugaji wa mbuzi. Mipango ikikaa sawa baada miaka 2 naweza kuwa navuna mbuzi 150 - 200 kwa mwaka.
Nikikamilisha matayarisho nitakutafuta kiongozi.