Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa

RealMan,
Kuhusu wezi ni tatizo ambalo linaweza kudhibitika. Namna gani utadhibiti wezi ni kuwa lazima uajiri mlinzi ambaye atakuwa anakulindia wakati wa usiku, kama unavyojua huu ni mradi na unahusisha pesa nyingi za uwekezaji hivyo ni muhimu wakati unapanga bajeti ya huo mradi wako ukajumuisha gharama za mlinzi.

Kuhusu kufugia mikoani hakuna shida yeyote kwani wakati wa kuuza utakodi canter na utawapakia mbuzi wako tayari kuwapeleka sokoni Dar au kwenye miji mikubwa. Gharama za usafiri ni ndogo sana kwa kila mbuzi na mara nyingi huwa haizidi tshs. 5000/= .

Kama utaona kufugia mikoani kutaongeza gharaza za usafiri au labda siyo mzoefu kwenye usafirisha wa wanyama na kwenda kuwauza Dar unaweza ukatafuta shamba Mkuranga au Babagamoyo ambako wafugaji wengi nimewasaidia kuwaanzishia miradi yao ya mbuzi na Kuku huko na kwamba hali ya usalama ni kubwa tu ukilinganisha na maeneo yaliyo jirani zaidi na Dar.

Hakya nani kiongozi kunako majaaliwa mwakani mbuzi wa maulid/chrismas/idd utamtoa kwangu.

Nina maeneo makubwa Mkoa Mwanza labda nifanye utafiti wa ziada kujua wasafirishaji wanalipa kiasi gani kufikisha mbuzi mmoja Dar..
Wazo la kupata shamba mkuranga ama bagamoyo lina mantiki zaidi kwa maana ya usimamizi wa karibu ingawa bei ya mashamba maeneo haya imekwenda juu siku za karibuni.

Kwa kifupi nimesha shawishika 100% kufanya ufugaji wa mbuzi. Mipango ikikaa sawa baada miaka 2 naweza kuwa navuna mbuzi 150 - 200 kwa mwaka.

Nikikamilisha matayarisho nitakutafuta kiongozi.
 
Huko Dodoma wamejaa tele kila kona ama unawafuata wapi?

Contacts?
Maundumula,

Dodoma mbuzi ni wengi isipokuwa ukihitaji lazima uwasiliane nami kwa ajili ya kukutafutia kwa wafugaji ambao mradi wa uboreshaji wa mbuzi uliwapitia na pia kukuchagulia mbuzi wazuri na wenye afya.Maana kama utatafuta mwenyewe kuna uwezekanano ukawanunua mbuzi wagonjwa au waliokwisha kuzaa na wakati mwingine unaweza kuwanunua mbuzi wasioboreshwa. Kwa maelezo zaidi wasiliana nami kupitia simu 0767989713 au 0776989713.

Karibu sana umasikini unaweza ukatokomezwa kwa ufugaji wa mbuzi.
 
Wana JF

Nmepata ushauri kutoka kwa wafuatiliaji wa mada zangu kuwa nitumie jina langu halisi ili kuwarahisishia kulitamka na kunifahamu hivyo nimesikia ushauri wao na nimetekeleza hivyo jina langu halisi ni Aman Ng'oma ndio jina langu halisi ambalo nitakuwa nilitumia kuanzia leo na kuendelea.Asante kwa ushirikiano wenu.

Nakumbuka hii ni mara yangu ya tatu kubadilisha jina mwanzo nilitumia Kichwa mbovu,nikashauriwa nibadilishe, nikaja na Zantsan pia nimeshauriwa nibadilishe na sasa nimekuja kwa jina langu halisi.

Maada inaendelea, karibu sana.
 
Bei zipoje kabla hatujaanza kuwasiliana
 
Wana JF,

Tunashukuru sana Bwana Amani, mm ni mmoja wa waliosave no zako so ninaziamend accordingly. Nimecheka sana hapo kwenye jina lako la kwanza duh ni vzr kwamba ulibadilisha maana ndoto zote hizo zitoke kwa kuchwa mbovu? Niko kwenye michakato fulani kwa sasa nikiwa tayari nitakutafuta mkuu.
 
Wana JF,

Nmepata ushauri kutoka kwa wafuatiliaji wa mada zangu kuwa nitumie jina langu halisi ili kuwarahisishia kulitamka na kunifahamu hivyo nimesikia ushauri wao na nimetekeleza hivyo jina langu halisi ni Aman Ng'oma ndio jina langu halisi ambalo nitakuwa nilitumia kuanzia leo na kuendelea.Asante kwa ushirikiano wenu.

Nakumbuka hii ni mara yangu ya tatu kubadilisha jina mwanzo nilitumia Kichwa mbovu,nikashauriwa nibadilishe, nikaja na Zantsan pia nimeshauriwa nibadilishe na sasa nimekuja kwa jina langu halisi.
Maada inaendelea, karibu sana.

Ahsante mkuu Amani. Mm nilizisave no zako so nitabadili jina pia. Umenichekesha sana kwenye jina lako la awali. Duh ni vzr ulilibadili maana nondo zote unazoshusha unawezaje kuwa kichwa mbovu?

Niko kwenye michakato fulani nikiwa tayari nitakutafuta!
 
Mradi mzuri kwa ukweli, Mbuzi wanavumilia mwendo wetu wa kibantu_bantu.

Ningependa kufahamu jinsi ya kudhibiti kuzaliana kwa Mbuzi wanaofugwa kwa mtindo wa huria ili kulinda afya ya vizazi ndani ya shamba na pia kama hutajali kueleza japo kwa uchache wa maneno vigezo vinavyotumika kuangalia afya na ubora wa Mbuzi.
Salaam.
 
Ndiyo kiongozi ni mimi ila ni Ng'oma siyo Ngoma ingawa maana ile ile.
Mkuu naona kuna swali la idadi ya mbuzi kwa eneo ukiulizwa hulijibu, tunaomba utupe jibu mkuu

Mbuzi 200 wanahitaji eneo la ukubwa wa hekari ngapi kama utawafuga kwa mtindo wa free range??
 
tunashukuru mkuu nimejifunza jambo jipya kwenye kichwa changu kuhusu mambo ya ufugaji na ujasiliamali
 
Nashukur kwa kunipa ufahamu wa ufugaji huu wa mbuzi

Kama ungeweza saidia contact ingependeza ili na sisi tuweza kufuatilia !
 
Mkuu naona kuna swali la idadi ya mbuzi kwa eneo ukiulizwa hulijibu, tunaomba utupe jibu mkuu

Mbuzi 200 wanahitaji eneo la ukubwa wa hekari ngapi kama utawafuga kwa mtindo wa free range??
Asigwa,
Sio kama sitaki kulijibu bali nakabiliwa na majukumu mengi,so ninapopata muda kidogo ndio huo nautumia kwa ajili ya kujibu maswali mbalimbali yanayoulizwa.

Kwa kifupi tazama jedwali lifuatalo hapo chini ili kujua idadi ya mbuzi wanahitajika kukaa katika eneo la ekari moja

Maoni
Mbuzi/Ekari
Vizuri sana
10-15
Vizuri
16-20
Wastani/kawaida
21-28
Mbaya
29-40

Kwa matiki hiyo, katika shamba la ekari moja haishauriwi idadi ya mbuzi izidi 28.
 
Wana Jf hasa wafuatilliaji wa uzi huu,

Kwa muda kidogo nimekuwa sipatikani mara kwa mara kwenye huu mjadala wetu kutokana na kukabiliwa na majukumu kidogo yanayonifanya niwe busy. Pamoja na mambo mengine nilipata kazi ya kumnunulia mbuzi mwenzetu ambaye ni mfuatiliaji mkubwa sana wa mada mbalimbali hapa jamii forum hasa kwenye hili jukwaa la ujasiria mali.

Alinipatia kazi ya kumnunulia mbuzi 50 majike na 2 madume. Katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikifanya kazi nilijitahidi kuandika na kutunza kumbukumbu kwa kila sent niliyokuwa naitoa kusudi nije kutoa hapa jamvini ili watu wengine wapate kujua gharama za kuwanunua mbuzi hao, kuwasafirisha pamoja na gharama nyinginezo zinazohusiana.

GHARAMA ZA UNUNUZI WA MBUZI DODOMA.jpg
Kama kuna mtu atakuwa na swali nitamjibu.Kwa hakika namshukuru mwanajamvi huyu kwa kunipa nafasi ya kumfanyika kazi.
 
Wadau wa uzi huu,

Leo tuendelee kidogo na mada yetu. Kwa ujumla ufugaji wa mbuzi haukati hata kidogo kama mfugaji atakuwa makini na mradi wake. Mara nyingi mbuzi husumbuliwa zaidi na ugonjwa wa mapafu na ugonjwa huu mbuzi wakicheleweshwa kupata matibabu hufa kwa wingi. Daliliya ugonjwa wa mapafu mbuzi anakuwa na homa kali, kukohoa, kifo hutokea baada ya siku 1-2 tu. Ni muhimu kutambua mapema dalili za ugonjwa huu ili mbuzi wawahi kutibiwa haraka.

Mbuzi ni tofauti na ng'ombe ni wastahimilivu sana dhidi ya ukame. Wanakula nyasi pia wanakula majani ya miti. Ikitokea nyesi zimekwisha au kukauka watandelea kuishi na kuzaliana kwa kula majani ya miti.Wakati wa kiangazi mmiliki wa mradi wa ufugaji wa mbuzi huwi na presha juu ya chakula cha kuwalisha mbuzi.

Thamani ya mbuzi imekuwa kubwa hasa mjini kutoka na watu wengi kuhitaji nyama choma ya mbuzi hivyo hutoa hakikisho la faida kwa mwenye mradi .Isiteshe mbuzi huzaliana haraka sana ndani ya muda mfupi na kufanya kundi lao liongezeka kwa kasi. Kwa wastani toka mbuzi ashike mimba hadi kuzaa(Gestation period) huwa inamchukua siku 150 sawa na miezi 5,ndani ya mwaka mmoja mbuzi anazaa mara 2.

Ukiwa na mbuzi 50 majike na madume 2 katika uwiano wa 1:25, ndani ya miaka 3 utakuwa na mbuzi majike jumla 200+madume 152 hawa ni wazazi na watoto wao +118 majike na 118 madume hawa ni watoto wa watoto. Kwahiyo jumla kuu utakuwa na mbuzi 588 hii idadi na ndani ya miaka 3 kati ya hao madume yatakuwa 270 na majike yatakuwa 318. Hii hesabu niliyofanya kupata hii idadi ya mbuzi jumla kwa miaka 3 ni hesabu kali sana. Unaanza na mbuzi hamsini unamaliza na mbuzi 588 ndani ya miaka 3
 
Back
Top Bottom