Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa

Samahani wakuu yawezekana nauliza swali la kijinga ila naombeni jibu hivi market ya mbuzi iko vipi kwa dar kama ukiwa unambuzi 200 waweza kuuza wapi waishe wote. Kwa ufahamu wangu nadhani itabidi upeleke vingunguti machinjioni.
 
Nahitaji mbuzi na kuku ambao ni kwa ajili ya Ufugaji, nikipata wale ambao ni kama (hybrid) nadhani ingekuwa pouwa,
Kwa ushauri na upatikanaji naomba tuwasiliane.

Asanteni.
 
Nahitaji mbuzi na kuku ambao ni kwa ajili ya Ufugaji, nikipata wale ambao ni kama (hybrid) nadhani ingekuwa pouwa,
Kwa ushauri na upatikanaji naomba tuwasiliane, asanten

Karibu Sayuni Poultry, Wafugaji na watotoleshaji wa vifaranga chotara. Tupo Dar - mbezi luis

Tuwasiliane zaidi 0712 057514
 
Nashindwa kuweka picha hapa, kuna banda la mbuzi ambalo nimeliona linakuwa na ngazi na mbuzi wanapanda na wanalala humo,ila nimeona sakafu ni ya mbao,swali langu sasa: je, vipi kuhusu usafi, kwa maana usiku watajisaidia haja ndogo/kubwa, hizi mbao si zitaoza?

Nalog off
 
Nashukuru sana wadau, nimeelimika kiasi cha kuweza kuwekeza.

Swali.

Mbuzi mmoja akiwa amefugwa vizuri, akichinjwa na ikachukuliwa nyama pekee, yaani fillet tupu zikaachwa sehemu nyingine za mbuzi kama kichwa, miguu, ngozi, utumbo nk. inawaza kubaki kilo ngapi?
 
Hivi punde nitaendelea kujibu na kuleta nondo mpya za namna ya ufugaji bora wa mbuzi, kaani mkao wa kuendelea kufyonza maarifa.
 
Naomba kuuiza kwa Mwanza wapi naweza pata hii mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha?

Mwenye kufahamu ani pm nawahitaji a.s.p

Kwa mara nyingine tena, leo nimeona haja ya kuanzisha mada nyingine na tujadiliane kwa pamoja juu ya ufugaji wa mbuzi baada ya kujadili kwa muda mrefu ile mada ya ufugaji wa kuku Ni kwa wafugaji/wanaotaka kuanzisha mradi wa ufugaji kuku

Ufugaji wa mbuzi hapa Tanzania ni fursa adhimu ambayo Watanzania wengi hawajaiona. Ni ufugaji ambao wenyewe kama mfugaji atazingatia kanuni na misingi ya ufugaji Bora, ni rahisi sana mfugaji kujiondoa kutoka kwenye umasikini na kuwa tajiri. Kitu cha msingi na muhimu ni kwamba,mfugaji lazima awe na eneo pamoja na mtaji wa kuanzia.

Mbuzi wanatakiwa kufugwa shambani. Shamba ambalo mbuzi wanatakiwa wafugwe linapaswa liwe na sehemu ambayo mbuzi wanaweza kwenda kuchungwa na pia kuwe na chanzo cha maji. Mbuzi kitabia hupenda kulala juu hivyo mabanda yao yanapojengwa lazima yainuliwe juu. Mabanda ya mbuzi si ghari,kwani hujengwa simple.

Mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara mbili na ukipata ile mbegu ya wanaozaa mapacha faida yake huwa ni kubwa zaidi, itategemea na mtaji wa mfugaji, lakini kama mfugaji ataweza kuanza na mradi wa mbuzi 50 inakuwa vizuri zaidi. Ukiwanunua mbuzi 50@ tsh.50,000/= utapata Milioni 2 na nusu, madume 2 kila moja likanunuliwa kwa tsh 75000/= kwa madume mawili itagharimu tsh laki moja na nusu. Usafirishaji wa mbuzi hauzidi laki tatu na nusu. Kwa hiyo itajikuta ukiwa na milion 5 utaweza kuanza na mradi wa ufugaji wa mbuzi majike 50 na madume mawili,pamoja na kuwajengea sehemu ya ya kulala.

Kama nilivyoainisha hapo awali, mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara 2, hivyo kama kila mbuzi atazaa hebu chukulia kila mbuzi atazaa mbuzi mmoja tu, ingawa kuna wengine watazaa mapacha hasa ukipata ile mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha, mwishoni mwa mwaka utakuwa na idadi ya mbuzi 100 wapya waliozaliwa na ukujumlisha na mtaji ule wa mbuzi 50 utakuwa na jumla ya mbuzi 150, hii ni ndani ya mwaka mmoja, pata picha utakuwa na mbuzi Idadi gani baada ya miaka 3 hasa ukizingatia kuwa wale watoto wa mbuzi watakapofikia miezi 8 utaanza kuwapandisha nao watazaa nk. Ili kufikia malengo, inashauriwa kuwa mbuzi wa mtaji wanaonunuliwa lazima wawe na umri mmoja ili kusudi waweze kupata mimba kwa wakati mmoja na waweze kuzaa kwa wakati mmoja pia.

Magonjwa ya mbuzi mengi yanafahamika na ni rahisi kudhibitika,hivyo mbuzi si rahisi kufa hovyo.

Toka mbuzi anapata mimba mpaka anazaa,hutumia muda wa wiki miezi mitano yaani siku 150.

Kwa sababu hili pia ni eneo langu nilililolisomea, nawaruhusu kwa wale wote wenye Interest na uanzishaji wa Mradi huu wa ufugaji wa mbuzi kuuliza swali lolote lihusulo ufugaji bora wa mbuzi nami nitajibu.Lengo likiwa ni lile lile la kusaidiana kama Watanzania ili kuondokana na hili lindi la umasikini.

Karibu kwa majadala.
 
Naomba kuuiza kwa Mwanza wapi naweza pata hii mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha???
Mwenye kufahamu ani pm nawahitaji a.s.p

Ngamba,
Kwakweli kwa Mwanza sijajua wanakopatikana ila kama kwa Dodoma ni Hombolo, Bai na Kondoa, na kwa Morogoro wanapatikana Kilosa.
 
Ngamba,
Kwakweli kwa Mwanza sijajua wanakopatikana ila kama kwa Dodoma ni Hombolo, Bai na Kondoa, na kwa Morogoro wanapatikana Kilosa.

So inaweza kunigalimu sh. ngapi kuwasafirisha toka Dodoma hadi mwanza? Na Je, Mbuzi wa maziwa wanapatikana wapi, maana next year nataka anzisha mradi wa kufunga mbuzi wa maziwa na nyama.
 
so inaweza kunigalimu sh. ngapi kuwasafirisha toka dodoma hadi mwanza?? na Je Mbuzi wa maziwa wanapatikana wapi, maana next year nataka anzisha mradi wa kufunga mbuzi wa maziwa na nyama

Kwa kawaida gharama za usafiri inategemea na Idadi ya mbuzi unaowasafirisha, wakiwa wengi gharama huwa chini, na kinyume chake, lakini kwa awastani itakugharimu shilingi elfu 7 kwa kila mbuzi utakayemsafirisha.

Mbuzi wa maziwa wanapatikana kwenye vyuo vya mifugo na pale SUA
 
Kwa mara nyingine tena, leo nimeona haja ya kuanzisha mada nyingine na tujadiliane kwa pamoja juu ya ufugaji wa mbuzi baada ya kujadili kwa muda mrefu ile mada ya ufugaji wa kuku wanaotaka kuanzisha mradi wa ufugaji kuku

Ufugaji wa mbuzi hapa Tanzania ni fursa adhimu ambayo Watanzania wengi hawajaiona. Ni ufugaji ambao wenyewe kama mfugaji atazingatia kanuni na misingi ya ufugaji Bora, ni rahisi sana mfugaji kujiondoa kutoka kwenye umasikini na kuwa tajiri. Kitu cha msingi na muhimu ni kwamba,mfugaji lazima awe na eneo pamoja na mtaji wa kuanzia.

Mbuzi wanatakiwa kufugwa shambani. Shamba ambalo mbuzi wanatakiwa wafugwe linapaswa liwe na sehemu ambayo mbuzi wanaweza kwenda kuchungwa na pia kuwe na chanzo cha maji. Mbuzi kitabia hupenda kulala juu hivyo mabanda yao yanapojengwa lazima yainuliwe juu. Mabanda ya mbuzi si ghari,kwani hujengwa simple.

Mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara mbili na ukipata ile mbegu ya wanaozaa mapacha faida yake huwa ni kubwa zaidi, itategemea na mtaji wa mfugaji, lakini kama mfugaji ataweza kuanza na mradi wa mbuzi 50 inakuwa vizuri zaidi. Ukiwanunua mbuzi 50@ tsh.50,000/= utapata Milioni 2 na nusu, madume 2 kila moja likanunuliwa kwa tsh 75000/= kwa madume mawili itagharimu tsh laki moja na nusu. Usafirishaji wa mbuzi hauzidi laki tatu na nusu. Kwa hiyo itajikuta ukiwa na milion 5 utaweza kuanza na mradi wa ufugaji wa mbuzi majike 50 na madume mawili,pamoja na kuwajengea sehemu ya ya kulala.

Kama nilivyoainisha hapo awali, mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara 2, hivyo kama kila mbuzi atazaa hebu chukulia kila mbuzi atazaa mbuzi mmoja tu, ingawa kuna wengine watazaa mapacha hasa ukipata ile mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha, mwishoni mwa mwaka utakuwa na idadi ya mbuzi 100 wapya waliozaliwa na ukujumlisha na mtaji ule wa mbuzi 50 utakuwa na jumla ya mbuzi 150, hii ni ndani ya mwaka mmoja, pata picha utakuwa na mbuzi Idadi gani baada ya miaka 3 hasa ukizingatia kuwa wale watoto wa mbuzi watakapofikia miezi 8 utaanza kuwapandisha nao watazaa nk. Ili kufikia malengo, inashauriwa kuwa mbuzi wa mtaji wanaonunuliwa lazima wawe na umri mmoja ili kusudi waweze kupata mimba kwa wakati mmoja na waweze kuzaa kwa wakati mmoja pia.

Magonjwa ya mbuzi mengi yanafahamika na ni rahisi kudhibitika,hivyo mbuzi si rahisi kufa hovyo.

Toka mbuzi anapata mimba mpaka anazaa,hutumia muda wa wiki miezi mitano yaani siku 150.

Kwa sababu hili pia ni eneo langu nilililolisomea, nawaruhusu kwa wale wote wenye Interest na uanzishaji wa Mradi huu wa ufugaji wa mbuzi kuuliza swali lolote lihusulo ufugaji bora wa mbuzi nami nitajibu.Lengo likiwa ni lile lile la kusaidiana kama Watanzania ili kuondokana na hili lindi la umasikini.

Karibu kwa majadala.

vyakula vya mbuzi ni vipi hasa ukiachana na pumba pamoja na nyasi!!
 
Mr Aman, kuna namna yoyote ya mimi kujiridhisha kwamba ni kweli hao mbuzi wanazaa pacha? na je kuna guarantee yoyote kwa hilo?
 
Kwa mara nyingine tena, leo nimeona haja ya kuanzisha mada nyingine na tujadiliane kwa pamoja juu ya ufugaji wa mbuzi baada ya kujadili kwa muda mrefu ile mada ya ufugaji wa kuku Ufugaji wa mbuzi hapa Tanzania ni fursa adhimu ambayo Watanzania wengi hawajaiona. Ni ufugaji ambao wenyewe kama mfugaji atazingatia kanuni na misingi ya ufugaji Bora, ni rahisi sana mfugaji kujiondoa kutoka kwenye umasikini na kuwa tajiri. Kitu cha msingi na muhimu ni kwamba,mfugaji lazima awe na eneo pamoja na mtaji wa kuanzia.Mbuzi wanatakiwa kufugwa shambani. Shamba ambalo mbuzi wanatakiwa wafugwe linapaswa liwe na sehemu ambayo mbuzi wanaweza kwenda kuchungwa na pia kuwe na chanzo cha maji. Mbuzi kitabia hupenda kulala juu hivyo mabanda yao yanapojengwa lazima yainuliwe juu. Mabanda ya mbuzi si ghari,kwani hujengwa simple.Mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara mbili na ukipata ile mbegu ya wanaozaa mapacha faida yake huwa ni kubwa zaidi, itategemea na mtaji wa mfugaji, lakini kama mfugaji ataweza kuanza na mradi wa mbuzi 50 inakuwa vizuri zaidi. Ukiwanunua mbuzi 50@ tsh.50,000/= utapata Milioni 2 na nusu, madume 2 kila moja likanunuliwa kwa tsh 75000/= kwa madume mawili itagharimu tsh laki moja na nusu. Usafirishaji wa mbuzi hauzidi laki tatu na nusu. Kwa hiyo itajikuta ukiwa na milion 5 utaweza kuanza na mradi wa ufugaji wa mbuzi majike 50 na madume mawili,pamoja na kuwajengea sehemu ya ya kulala.Kama nilivyoainisha hapo awali, mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara 2, hivyo kama kila mbuzi atazaa hebu chukulia kila mbuzi atazaa mbuzi mmoja tu, ingawa kuna wengine watazaa mapacha hasa ukipata ile mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha, mwishoni mwa mwaka utakuwa na idadi ya mbuzi 100 wapya waliozaliwa na ukujumlisha na mtaji ule wa mbuzi 50 utakuwa na jumla ya mbuzi 150, hii ni ndani ya mwaka mmoja, pata picha utakuwa na mbuzi Idadi gani baada ya miaka 3 hasa ukizingatia kuwa wale watoto wa mbuzi watakapofikia miezi 8 utaanza kuwapandisha nao watazaa nk. Ili kufikia malengo, inashauriwa kuwa mbuzi wa mtaji wanaonunuliwa lazima wawe na umri mmoja ili kusudi waweze kupata mimba kwa wakati mmoja na waweze kuzaa kwa wakati mmoja pia.Magonjwa ya mbuzi mengi yanafahamika na ni rahisi kudhibitika,hivyo mbuzi si rahisi kufa hovyo.Toka mbuzi anapata mimba mpaka anazaa,hutumia muda wa wiki miezi mitano yaani siku 150.Kwa sababu hili pia ni eneo langu nilililolisomea, nawaruhusu kwa wale wote wenye Interest na uanzishaji wa Mradi huu wa ufugaji wa mbuzi kuuliza swali lolote lihusulo ufugaji bora wa mbuzi nami nitajibu.Lengo likiwa ni lile lile la kusaidiana kama Watanzania ili kuondokana na hili lindi la umasikini.Karibu kwa majadala.
Ushauri wako ni mzuri sana ila kama ungeweza kutupa picha ya namba banda la kuku laweza kuwa ingefaa sana.
 
Vipi umeshapata ranch uliyokuwa unatafuta? Kuna sehemu wilaya moja ilitaka kuanzisha ranch,kwa sababu ya urasimu wilaya hiyo imeshindwa kuanzisha. Ni pazuri sana na mimi nimefika,pia hapo mahali apples za kisasa zinamea sana. Na kuna Mzungu anapafukuzia kiaina.

Makete kitulo
 
Back
Top Bottom