Michael Paul
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 403
- 319
Mkuu tunashukuru kwa maelezo mazuri. Umenipa hamasa ya kuwa na "karanch" kangu...
mkuu ukipata wasaa tembelea mashamba ya mifugo utapata kila kitu.Nimewahi kutembelea shamba la narco Kongwa ,chuo cha mifugo Lita Mpwapwa na shamba la mifugo pale iringa mjini kama unaelekea kilolo wana mbegu nzuri sana ila wenye ngombe wazuri sana ni iringa
Kitomari anatuhumiwa kuingiza wadau mjini hapa hapa Jf . Tujihadhari nae.Heshima kwako mkuu, the idea is sweet but for me you have to be so elaborative on how to share your idea.
mkuu wapi naweza pata hao mbuzi wa maziwa jamani nahitaji kwa kweli MKUU Kitomari NIMEM PM WALA HAJIBU SIJUI NATAKA KUPIGIWA????????????????
Ni mzaliwa wa kule..rufiji sehemu gani?.maana nako kuna mgogoro wa wafugaji na wakulima
UFUGAJI WA MBUZI NI UTAJIRI ULIOJIFICHA
Hawa mbuzi wanapatikana wapi kwa hapa TanzaniaHawa ni mbuzi na wala si Ng'ombe. Ni mbuzi aina ya Boer wenye asili ya nchi ya Africa Kusini. Ni moja ya kosaafu bora kabisa katika mbuzi wa nyama. Sifa yao kubwa ni kuwa na miili mikubwa kama wanavyoonekana katika picha hapo chini. Dume mmoja anauzwa kwa Tsh 250,000/= na jike lake Tsh 350,000/=. Umri wao wa kuuzwa ni miezi 6. Madume ya Boer yanafaa sana kwa ajili ya kupandishia majike ya mbuzi wa asili na hivyo kusaidia kuboresha mbuzi hao na kuwafanya wawe wenye tija zaidi.
Ufugaji wa mbuzi ni utajiri uliyojificha. Kwanza huzaliana kwa haraka kwa maana kwamba kwa mwaka mmoja mbuzi mmoja ana uwezo wa kuzaa mara mbili lakini vilevile hawasumbui kwenye masoko. Wanakula majani zaidi kwa kuwa wao ni aina ya wanyama wenye matumbo manne yaani Ruminant animals ambao kwa kiasi kikubwa hutegemea zaidi majani kama chakula chao kikuu. Mbuzi si kama kuku ambao huhitaji chakula kilichotengenezwa maalum na kwamba kila siku watahitaji utoe pesa yako mfukoni kwa ajili ya kuwanunulia chakula. Mbuzi wanauwezo wa kuishi wenyewe bila kuhitaji hela yako ya mfukoni kwa ajili ya chakula kwa muda mrefu ilimradi tu wawe wazima. Ni muhimu ukawa na daktari wako maalum ukaingia nae mkataba kusudi kila baada ya muda fulani awe anakufanyia ufuatiliaji wa maendeleo ya mbuzi wako japo kwa mwezi mara moja na pale linapotoke tatizo hasa mripuko wa ugonjwa. Kutokuwa na daktari wa mifugo katika mradi wako wa ufugaji wa mbuzi ni sawa na kutembea barabarani huku ukiwa umefungwa kitambaa usoni. Daktari wa mifugo si lazima umtoe mbali, kila kijiji kuna madaktari hao au maafisa mifugo ambao unaweza ukaongea nao mmoja wapo ili awe anakupa huduma pale inapohitajika.
Mbuzi wanahitaji uwe na shamba kubwa lenye maji ya kutosha na majani. Pia kuwe na vijana wa kazi waaminifu kwa ajili kuwachunga na ulinzi. Na ni muhimu pia shambani kukawa na Mbwa kwa ajili ya kuongeza ulinzi katika mradi wako.
Tanzania tuna mapori makubwa ambayo unaweza ukafanya uendeshaji wa mradi wako wa ufugaji wa mbuzi kwa ufanisi mkubwa bila kujali ni umbali kiasi gani. Watakapokuwa tayari kuvunwa, utatafuta gari na kuwapakia mbuzi wako na kisha kuwapeleka mnadani ambako utawauza kirahisi sana. Kuna minada mingi ya mifugo hapa Tanzania. Kuna ile minada ya awali ambayo wafanyabiashara wa mifugo wanaenda kuchuuza huko na kuwapeleka kwenye minada ya upili ambayo ni minada mikubwa iliyo chini ya wizara ya mifugo. Sasa kwa mfugaji wa mbuzi, utaamua wewe mewe mwenyewe kama uwapeleke mnada wa awali au mnada wa upili. Lakini vilevile kwa sasa kuna machinjio za kisasa za mifugo mfano machinjio ya kisasa ya mifugo ya Kizota Dodoma mjini ambayo mahitaji mbuzi yamekuwa makubwa kupita maelezo kutokana na nyama yake kuhitajiwa zaidi katika nchi za kiarabu hasa Oman na Dubai. Kwahiyo mahitaji hayo ya mbuzi yametengeneza soko kubwa na la uhakika. Shughuli za kilimo katika ufugaji hazisumbuliwi sana na masoko kama zilivyo shughuli za kilimo cha mazao mfano nafaka na matunda kutokana na kwamba minada minada ya mifugo imekuwa mkombozi mkubwa kwa wafugaji.
Changamoto katika ufugaji wa mbuzi ni magonjwa ambayo kimsingi yanadhibitika kupitia wataalamu wa mifugo.
Aman Ng'oma
0767989713
Dodoma
Hiyo mbegu ya ukweli sana ukiipata aisee..hawa mbuzi wanapatikana wapi kwa hapa tanzania