Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Uchaguzi mdogo wa madiwani ulikamilishwa na wapiga kura nchini Jumapili October 28, Chadema kimepata funzo kubwa lenye kutoa tafsiri kadhaa zenye kuleta matumaini kwa wenye moyo mkuu au kufifisha kwa wenye moyo mchache.
Kauli ya Freeman Mbowe yazaa tunda la kwanza
Mwenyekiti wa Chadema miezi michache iliyopita alitoa kauli ya kuwaasa vijana wasomi na wengine kujitokeza na kuchagua maeneo ya kugombea nafasi mbalimbali zikiwemo za uwakilishi ili waandaliwe. Wengi tulipongeza kwa utashi huo, kwa bahati nzuri katika uchaguzi huu mdogo wa Madiwani uliomalizika, kuna kijana mmoja msomi ambaye ameamua si kusubiria nafasi ya kugombea ubunge, bali ameamua kuanzia nafasi ya udiwani naye si mwingine bali ni diwani mchaguliwa wa kata ya Mlangali katika wilaya ya Ludewa ndani ya Mkoa mpya wa Njombe. Tunampongeza kwa kujituma, kutetena azima yake na kushinda. Kwa wengi haikuwa katika picha kwamba Chadema yaweza kupata kiti cha udiwani huko kuliko ngome ya CCM miaka nenda rudi kwa akina hayari Horace Kolimba, ni dalili kwamba mipango ikifanyika kwa umahiri na kumsimamisha mwenye sifa yawezekana, na imewezekana. Ni dhahiri Chadema imeshafunguliwa mlango Ludewa.
Diwani mchaguliwa ametoa mwanga kwa vijana wengi ambao pengine kwa kutokuwa na ujasiri wa kuthubutu wanahofia kitu wasichokuwa na hakika nacho kama watashinda au la, lakini kwa uchaguzi huu tumapata jibu kuwa wananchi wengi wanatuhitaji vijana katika kuleta mabadiliko katika jamii na maendeleo ya taifa letu. Chadema zoezi hilo limefana sana, wana mfano wa kuwafunda vijana wasomi wengi wajitokeze.

Kutofanya vizuri uchaguzi huu chadema sababu kusimamisha wagombea dhaifu
Maeneo mengi ambayo nguvu kubwa ya Chadema imetumika tumekuja kushuhudia kutoambulia hata kiti kimoja. Unaweza kujengeka utetezi wa aina mbalimbali, lakini kubwa zaidi ni Chama kuwaandaa wagombea wanaofaa ndio tatizo. Chama kisitegemee tu jina la Chadema limpatie mgombea kura, ila auzike na wapiga kura ndipo waridhie. Tatizo kubwa ambalo naona wagombea wengi wa Chadema kula mwanguko wa mende ni kukosa sifa kulinganisha na wagombea wa CCM. Eneo hilo linatakiwa kufanyiwa kazi na Chama.
Mbinu za Chadema kujitanua zibadilishwe kuendana na upepo unavyovuma.
Yale maandamano na mikutano ya hadhara inaonekana kutokuwa na nafasi kubwa kwa watanzania leo, kwani kama kuwasikia Chadema tumewasikia sana tu na jina la Chadema linalia masikioni mwa wengi kama mwangwi wa mlima Kilimanjaro. Tabia ya kinyonga kujibadilibadili rangi kuakisi mazingira yanayomzunguka ndiyo inayohitajika kwa Chadema sasa hivi.
Pendekezo kwa Chadema ni:
[*=1]Kuachana na maandamano kwani yanachelewesha watu kuwajibika katika kujenga uchumi wa nchi
[*=1]Kupunguza mlolongo wa mikutano kwani inapoteza nguvu na rasilimali za chama wakati chama sera zimeshafahamika.
[*=1]Kuanza mkakati wa kupeleka wajumbe vijijini na mitaani kwa kusaka wafuasi watakao kuwa wanachama hai nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa hapo uchaguzi ujapo Chadema itakuwa na uhai wa kura kuanza kuhesabu wanachama hai walio nao kama CCM ifanyavyo, la sivyo watabaki kuvimbisha mishipa usoni majwakwani na kuambulia patupu kura zipigwapo.
[*=1]Zoezi la kuwapata wanachama mijijini liwe endelevu na kuimarisha kuwa na wajumbe wa nyumba kumi wenye kuhakiki wanachama kwa kulinda na kuhamasisha uhai wao chamani.
[*=1]Chama kuweka msingi vijijini na kuwa na wanachama ni mtaji mkubwa kwani ndiko kwenye wapiga kura wengi na majimbo mengi ya uchaguzi.
[*=1]Chambo cha mawasiliano kitaifa iwe ni radio au TV ili harakati na sera za chama ziweze kuwafikia wengi badala ya kutumia tu blog kwa njia ya online ambayo mwenye kufikiwa ni Candid Scope badala ya walengwa wapiga kura walio wengi wa vijijini.
Posho za watumishi wa matawini
Kufanya kazi kwa ridhaa kuna madhara yake. Mfano, unaposikia Katibu Mkuu wa Chadema analipwa Tsh. 7,000,000 huku watumishi wa matawini, katani, mikoa na wengineo wakifanya kazi kwa ridhaa huathiri utendaji na ukuaji wa chama. Chama kiwe na mkakati maalumu kuwapa posho walao kidogo kinachowezekana hawa watumishi.
Ruzuku inayopewa isielekezwe kwenye mikutano na maandamano tu, bali watumishi wa mawawini, katani, mkoani na wengineo wafikiriwe ili wafanya kazi kwa moyo wa matumaini zaidi. Pengine ongezeko la wadiwani sasa hivi litapandisha dau la ruzuku, hivyo ongezeko hilo bora lingeelekezwa kuwapa posho watumishi hao kila mwezi kila inapowezekana ili kupunguza manung'uniko ya hapa na pale na hivyo kuathiri utendaji na uwajibikaji wao. Kumbuka CCM inatumia mwanya wa ukata wa vyama vya upinzani kuwarubuni wapiga kura.

Kuandaa wagombea nafasi mbalimbali wenye sifa
Jitihada kubwa zinatakiwa kuwekwa katika kuandaa nguvu ya kutosha katika kuwaandaa wagombea katika chaguzi mbalimbali zijazo kwa kipindi kirefu kutosha. Isitumike ila ya zima moto. Kama alifanikiwa Nasari wa Arumeru mashariki kwa mtindo wa zima moto tusitazamie mtindo huo huo utatumika kufanikisha chaguzi nyingine, kwani wagombea wanatakiwa umma uwafahamu kwa kipindi cha kutosha na hivyo wanatakiwa kuwa karibu na maeneo yao wanakotegemea kugombea mara kwa mara.
Kuunganisha nguvu za upinzani
Mwenyekiti wa Chadema ambaye ni mbunge na mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita alisema kuungana kambi ya upinzani wapate muda kwanza kwa sababu ya majeraha ya uchaguzi. Hilo lilieleweka. Sasa majeraha ni karibu yamepona labda kama yapo ambayo yamegeuka kuwa donda ndugu.
Viongozi wa Chadema kitaifa wanatakiwa wataremke kutoka pale walipo ili wawafikie wenzao na kupika na kula meza moja chakula kinakuwa kitamu zaidi. Unyenyekevu ni siri moja kubwa katika kujiwekea malengo ya mafanikio. Ushupavu umewaweka wengi katika hali ya kubakizwa isolated. Ukiwa na mtoto jifanye kama watoto wafanyavyo, kwa wachezaji utajifanya mwanamichezo, wasomi utaongea mambo ya kisomi nk. Ndilo linalotakiwa Chadema wawaone wenzao vyama vya upinzani ni hazina katika kubuni, kupanga na kufanikisha mikakati ya kuikomboa nchi. Kura nyingi katika uchaguzi mdogo uliomalizika utakuta kama wangeunganisha nguvu CCM ingetelekeza viti vingi zaidi, sasa bora lipi? Kuthoofisha nguvu za CCM kwa kunyang'anya himaya yao kuwa chini ya umoja wa upinzani au kubaki na unyonge wa mwenye kiti kimoja abaki kivyake na wenye viti vingi wajisikie kujitutumua huku kuchukua dola ikibaki ndoto za kufikirika?

Viongozi kitaifa watambue kasoro zisemazo wajitahidi kujirekebisha
Viongozi wa kitaifa Chadema yanayolalamikiwa na baadhi ambao wamewahi kufanya kazi nao na kisha kuamua kujitoa hayawezi kubezwa, kwani lisemwalo lipo kama halipo laja, na tujue hawa ni binadamu kama tulivyo wengi tulivyo na kasoro nyingi tu za kimaumbili, kimaadili, kifikra, kujikuza, kujiona baora, na kiutambuzi. Siyo kubeza tu, wanatakiwa kujitathmini, maana kuendekeza sana tabia binafsi na nafsi ya mtu katika uongozi ni hatarishi katika nyanja za siasa. Yalisemwa, yanasemwa, lakini kuyaacha yapite tu kama tunataka mageuzi ya kweli hatutakuwa wa kweli na kuwatakia mema.
Hulka ya kiaongozi katika jamii:
Hulka ya kiaongozi katika jamii:
[*=1]ushirikiano na ushirikishi,
[*=1]unyenyekevu na ukakamavu,
[*=1]uvumilivu na ustahimilivu,
[*=1]hekima na busara
ni mambo ambayo yanamjengea heshima na mafakio katika utumishi. Maamuzi ya papo kwa papo ni hatari, majuto ni mjukuu kwani maji yakishamwagika hayazoleki.
Viongozi wanatakiwa kuondokana na kulewa sifa, kulewa umati wa wahudhuriaji mikutano. Wanaohudhuria mikutano ya Chadema walio wengi ni mashabiki ambao si wapiga kura tofauti na mikutano ya CCM ambayo wahudhuriaji ni wapiga kura. Mkutano wa CCM wahudhuriaji 75% ni wapiga kura wake wakati wahudhuria wa Chadema kiwango hicho hicho wahudhuria ni mashabiki tu kama inapotokea tukio fulani watu wanafurika isivyotegemewa ndivyo Chadema wanavyotakiwa kusoma mwelekeo huu unavyowalaza chali katika chaguzi. CCM inapobeba watu kwa malori ni wanachama wake si mashabiki wakati mikutano ya Chadema wanaofurika ni mashabiki wasio wapiga kura. Hii ndiyo hali halisi ya tathmini yangu.

Diwani wa Mlangali, Ludewa ni changamoto na hasa kwa vijana wasomi
Vijana wasomi na wahitimu wengi vyuo vikuu tumekuwa na kasumba ya kuhangaika huku na kule huku tukilazimika kumaliza kandambili zetu kwa ajili ya kutembeza RESUME wakati tuna nafasi tele kama za huyu msomi mwenzetu kuelekeza nguvu huko matawini, vijijini, katani na wilayani kujenga msingi wa maisha. Ametufunza mengi, ametufunza mengi, wenye upeo wa masafa marefu wamempata, wenzangu mimi wenye kufikiria leo na kesho tu tutabaki kuchakaza kandambili kutembeza resume huku na kule.