Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
- Thread starter
- #61
Hivi wewe, umeshafanya tafiti za kina za HUJUMA ZA CCM KWENYE CHAGUZI NA UKAZIJUA KISAWASAWA NA KIUNDANI NA IMPACT ZAKE KWA CDM? au umefanikiwa tuu kuchambua kasoro za CDM???
Majimbo na viti vingine vya udiwani ambako Chadema wameshinda hujuma hizo hazikuwepo? Kama Chadema ilifanikiwa kuzima hujuma katika viti walivyovichukua kwa nini ishindikane hilo viti vingine ambavyo hawakuvichukua?
Chadema isimamishe watu wenye sifa ambao wanauzika kwa wapi kura amini Chadema itazoa viti vingi. Akina Samwel Sitta walishaliona hili waliposema Chadema hawana safu ya kutosha, ndio hapo. Kufanya jitihada kusimamisha watu wanaokubali ndio ushindi si wa kuokoteza wasio na ushindani.
Kumbuka kuwa kushindanisha watu kadhaa katika kutafuta mgombea wa kiti ndiko kupata anayefaa, lakini sehemu nyingi utakuta Chadema anajitokeza mmoja tu kama mbovu au mzuri, anauzika au hauziki ndiye ataakayepeperusha bendera ya chama dhidi ya vyama vingine. CCM wanao wengi na anayeibuka huwa amewazidi wenzake na hivyo kuuzika katika kampeni.
Pamoja na kuwa makini hujama katika chaguzi, lakini tusifikirie msingi wa ushindi CCM ni hujuma tu, la hasha, sifa ya mgombea inawasaidia zaidi.