Akili ni nywele na kila mmoja ana zake. Lakini pia naheshimu sana mchango wako. Haya ni maoni yangu binafsi nikichukulia mifano ya waliofanikiwa kwa kutumia njia hiyo kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Katu kidole kimoja hakivunji chawa.
Uhuru wa visiwa vya Zanzibar na Pemba vilivyafanikiwa baada ya vyama vya wazawa kuwa na umoja, na hivyo mapinduzi yalipangwa kwa pamoja, la sivyo mambo yasingewaendea kama ilivyokuwa.
Mwai Kibaki wa Kenya alifanikiwa kumng'a kisiki Daniel Arap Moi baada ya kutaabika mara kadhaa bila mafanikio, mwishoni aliamua kuteremka awakute wenzake kwenye kambi ya upinzani, alipounganisha nguvu ndipo dhoruba kali ya umoja wao ilimshinda nguvu Daniel Arap Moi.
Zambia tumeshuhudia mageuzi ya kisiasa yametokana na kuunganisha nguvu hizo pia.
Tanzania kabla ya uhuru kulikuwa na vyama vingi ambayo vingi vikiwa ni social clubs, lakini Nyerere akianzia na kile cha TAA alifanikiwa kuunganisha hata club za akina Kawawa huko makazini na kuwa na nguvu ya pamoja katika kudai uhuru na hivyo kuwa chimbuko la TANU.
Kama hali itaendeleea hivi hivi kwa kuwaweka kando wapinzani hapo CCM itakuwa imefanikiwa copy and paste ya mfumo wa mkoloni mwangereza ya divide and rule.