Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,884
- 6,885
- Thread starter
- #41
Wadau,
Vichwa vya habari vya baadhi magazeti ya leo vimewanukuu baadhi ya viongozi wa ccm wakikibeza cdm eti kwa ushindi finyu wa uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika hivi karibuni nchini. Nimesoma pia humu jamvini maoni ya watu ambao inawezekana ama ni wanachama wa cdm au viongozi wa cdm wakitoa maelezo yanayodhihirisha kukatishwa kwao tamaa na matokeo hayo. Kwanza nianze kwa keeleza jambo moja ambalo ni bayana kwamba kuking'oa chama tawala siyo kazi ya lelemama na muda mfupi kama wengi wetu tunavyodhani. Ni kazi nzito na inahitaji nguvu kubwa na yenye mabonde na milima mingi. Kwa hiyo, inahitaji uvumilivu mkubwa sana. Binafsi, nakishukuru sana cdm kwa kutuonyesha watanzania kuwa ni chama kilicho na dhamira ya dhati ya kumwondoa mkoloni wa pili ambaye ni ccm. Vyama vingine viliibuka kwa nguvu hiihii na sasa vinaelekea kaburini au tayari vipo kaburini.
Waswahili wanasema siku njema huonekana asubuhi. Matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika nchini hadi sasa yanaashiria cdm ina-gain na ccm ina-lose. Ukichora graph ya ushindi wa ccm tangu mwaka 2005 bila shaka utabaini hiki ninachoandika hapa. Wakati upande huo wa ccm ukiwa hivyo, upande wa cdm unaendelea kuongeza ushindi yaani graph inapanda. Huo ndiyo ukweli na utaendelea kubaki kuwa ukweli.
Kwa wana ccm makini na wasomi kamwe hawawezi kufurahia matokeo ya kupoteza kata 4 na kuziacha ziende kwa wapinzani wao cdm. Hali kadhalika, kwa wana cdm makini na wasomi hawawezi kusikitika kupata ushindi kwenye kata chache ikilinganishwa na ccm wakati katika kata walizopata, 4 ni mpya.
Ndugu zangu wana cdm na wapenda mabadiliko, tafadhali msikate tamaa kabisa. Ushindi upo na endeleeni kuongeza bidii. Sumu iliyowekwa na ccm kwenye vichwa vya watanzania ni kali. Inahitaji utaalam na commitment ya hali ya juu kuiondoa na kuwakomboa watanzania.
Kama ulisoma paragraph ya kwanza katika mada yangu utagundua nimeongelea hicho unachokisema kwa kifupi sana kama ifuatavyo:
Wewe ni mmoja kati ya wenye moyo mkuu wa kutambua hayo, wengine wamekata tamaa na kusema wameshauri uongozi hawasikii sasa bai. Hayo sikubaliani nayo, siasa ni sayansi lazima kusoma upepo unavyokwenda na pia huhitaji muda kupata mang'amuzi katika nyanja hizi.Uchaguzi mdogo wa madiwani ulikamilishwa na wapiga kura nchini Jumapili October 28, Chadema kimepata funzo kubwa lenye kutoa tafsiri kadhaa zenye kuleta matumaini kwa wenye moyo mkuu au kufifisha kwa wenye moyo mchache.
Mambo ambayo tunayaona kama yameweza kusababisha ndiyo tunayojadili hapa ili viongozi wahusika wayafanyie kazi. Kunyang'anya viti vilivyoshikwa na chama tawala si lelemama.