Mwl. Nyerere kujilimbikizia madaraka haikuwa shida kubwa aliyotuachia bali ujamaa na kujifungia kwenye chungu

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,243
Reaction score
90,302
Kuna watu wanamlaumu Nyerere kwamba alijilimbikizia madaraka, kujiweka kama mtawala wa kiimla na hatimaye kutuachia mfumo huo mpaka sasa ambao tunahangaika nao. Ni kweli alifanya hivyo lakini karibia mataifa yote hadi yale yaliyoendelea sana viongozi wake wa mwanzo(founders) walifanya hivyo pia.

Kuanzia Korea Kusini, Singapore, nchi za Ulaya zilizoanza kama ufalme mkamilifu(absolute monarchies) mpaka Malawi ya Kamuzu Banda, Zambia ya Kaunda, Ghana ya Nkurumah, Kenya ya Jomo Kenyatta n.k kote tawala za mwanzo zilizounda mataifa zilifanana katika Rais au Mfalme kuwa na mamlaka makubwa mno yasiyodhibitiwa(unchecked powers).

Hata hivyo mengi ya haya mataifa yameweza kurekebisha hiyo kasoro taratibu au kwa haraka hasa baada ya kupata maendeleo.

Tatizo kubwa zaidi la Africa baada ya uhuru ilikuwa ni kuletewa na watawala mfumo wa kigeni wa ujamaa. Kwa Tanzania ilikwenda mbali zaidi kwa raia kufungiwa kwenye chungu(kwa propoganda na kutofundishwa Kingereza) watu wakabaki hawajui jinsi mataifa mengine yanavyoendelea huko duniani kwa ukweli na uhalisia, sio ajabu mwaka 1992 wengi waliamini mfumo wa vyama vingi utavuruga nchi wakataka kubaki na chama kimoja.

Kama ni kuhukumiwa, Nyerere atahukumiwa kwa haki zaidi kwa haya mambo mawili ya Ujamaa na raia kufungiwa kwenye chungu.
 
Haha! hapo kwenye kujua kiingereza umepuyanga ndugu!.. maendeleo hayaletwi na kiingereza kama wananchi wako wanavichwa vya maendeleo lugha yao mama inawatosha tu!, na kama ni mazumbukuku hata uwachape bakora za shingo ni mazumbukuku tu!.

Kuna vitu wakati wa nyerere wala sio vya kulaumiwa maana viliamuliwa kutokana na mazingira ya wakati huo!, mfano ilihitaji kuwaleta watu karibu waishi kijamii na pia ili waweze kuletewa huduma zakijamii hivyo ililazimika watu kuwahamasisha na kuwalazimisha kuhama maeneo waliyokuwa wanahama nakuwaleta karibu!.

Chengine fatilia mahali pote binadamu huogopa kitu kipya ama mabadiriko!, aidha kwasababu mbalimbali ila mabadiriko yoyote yanayohusu mfumo huchukua muda watu kuyakubali!..

Kuna watu wachache hujifanya vichwa vigumu sana kwenye kuelewa mambo!, na wengine hupinga kihisia kisa tu hana uchangamano na jamii fulani ama chuki, pasipo kupima hicho kitu kwanjia ya utambuzi yakinifu!.. Hivyo ni heri kuwa mchambuzi kwa kila hoja inayoletwa bila kuangalia hisia, mlengo n.k

Hakuna uongozi utakaoongoza halafu ukawa perfect kwa asilimia zote!, kiongozi anachotakiwa nikuwa kupunguza asilimia tu zakuwa mkosefu!, hivyo maarifa kwake ni lazima, upembuzi yakinifu, kusikiliza, nakujua namna nzuri yakuchagua bila kusahau kusimamia misimamo ya anachokisimamia!.

Ninapata tabu kwa baadhi ya watu kushindwa kuelewa baadhi ya mambo yaliyotendeka hapo awali yalitendeka kwanini na kwamazingira yapo!. na hapo ndipo napochuja nakujua kuwa kama leo hii wanawaza hivyo basi hiyo jana wangekuewepo wao halafu wakapewa nafasi yakuongoza basi tungetumbukia!.
 
Mataifa yote yanayotuzunguka angalau nusu ya raia wake pamoja na kuwa wana lugha zao wanajua kwa ufasaha lugha kubwa mojawapo za kimataifa kama Kingereza, Kifaransa au Kireno.
Umewahi kujiuliza kwa nini sisi peke yetu ndio sehemu kubwa ya raia wake hawajui lugha za kimataifa na athari zake? Psycholinguistics.
 
Angalia mataifa ya asia halafu ndo uangalie hoja yako!, watu wapo na lugha zao na hatuwafikii kimaendeleo!. kama kichwani hamna ni hamna tu mkuu lugha utaisingizia bure!.
 
Unpopular opinion, yule mzee alipenda sifa kwenda kuhangaika na mataifa mengine kwa kigezo cha (ukombozi wa bara la afrika) wakati kwake kuna ungua kwangu it was insane, we were not that stable kiuchumi na kila kitu, kuanza kwenda kuhangaika na shida za wengine ulikuwa ni uwendawazimu.
 
Unpopular opinion, yule mzee alipenda sifa kwenda kuhangaika na mataifa mengine kwa kigezo cha (ukombozi wa bara la afrika) wakati kwake kuna ungua kwangu it was insane.
Hakuwa mzuri sana kwenye suala la ku manage uchumi.
 
Back
Top Bottom