Mwizi ananiibia ndizi shambani

Kuna jamaa miaka ya nyuma huko ilikuwa ukienda kuiba mbao zake badala ya kupeleka ulikokusudia, unapeleka nyumbani kwake.

Ukifika unamkuta anakusubiria, anakuelekeza sehemu ya kuweka then ndio akili zinakujia unaondoka kwa aibu.
Yaani yeye ukienda kuiba tu, anapata alert anaanza kukusubiri nyumbani kwake na kuandaa vizuri sehemu ya kuweka.
 
Weka walinzi at least wawili.

Habari zenu wanandugu natumaini mtakuwa salama sana....

Miezi 10 nyuma nilifanikiwa kununua eneo nikiwa bado najichanga changa nione nitalifanyia nini hili eneo liweze kunipa matunda muda huo ikanibidi nianze kulipanda ndizi nikaanza kuchimba mashimo ya migomba kwa mikono yangu na nilipoona panapohitaji nguvu kazi kubwa niliweka vibarua wakunisaidia mpaka nkakamilisha mashimo 580 na mbegu za migomba nilichukua kwa majirani zingine nilinunua kwa pesa mpaka nkafanikiwa kupanda shamba zima likiwa na migomba (ndizi) za kupika 350, kuvundika ndizi 100 na ndizi za kuchoma 25 mpaka sasa sijapanda mashimo mengine...

MAFANIKIO.
Ndugu zangu ni kwa muda mchache sana kama miezi 8 naanza kuona mafanikio baadhi ya NDIZI zimebeba sana na kuna shule ipo jirani ya mtu binafsi kila ijumaa nmepewa oda niwe napeleka mikungu 20 ya ndizi na kila mkungu wa ndizi nauza mpaka Tsh. 12000 na naweza vuna mikungu ya ndizi zaidi ya 30 kwa mara moja , ndizi zinatoka kubwa na zenye afya kwa sababu kila shimo la mgomba niliweka mbolea ndoo mbili ya samadi.. Na maji yapo karibu kwa hiyo hainipi shida kumwagilia

CHANGAMOTO..
Hapa ndo penye umuhimu mkubwa sana na ndo hasa lengo kuu la kuuanzisha Uzi huu kuna wezi wameisha anza kuniibia ndizi shambani nmepata wamekata migomba kama 6 na wameondoka na NDIZI inaniuma sana wadau naombeni msaada najua humu JF kuna watu walishawahi kupitia changamoto kama yangu ama zaidi ila walitatua kwa namna yoyote ile nipo tayari...

"tusameheane kwa mwandiko wangu wakubwa"
 
Mkuu uko mkoa gani ndizi zinastawi?maana mi ninaeneo langu hapa dar maji yapo inakaribia miaka miwili eneo linakaa tu naona nimeshawishika na hiyo kilimo chako sasa ndo sijui kustawi kwake
Ndizi zinastawi sehem yenye maji kiasi na udongo mzury wenye rutuba ndizi ,ule udongo wa kukuza muhindi unatosha kuotesha mgomba na ukawa vema nipo tarime -Mara(musoma)
 
Mkuu uko mkoa gani ndizi zinastawi?maana mi ninaeneo langu hapa dar maji yapo inakaribia miaka miwili eneo linakaa tu naona nimeshawishika na hiyo kilimo chako sasa ndo sijui kustawi kwake
Mkuu shughuli za utalii kwa sasa zinaendaje ?
 
Bravooo
Weka mlinzi, Zungusha wavu, kisha otesha bougainvillea, na mbwaa (wanasaidia usiku na mchana manake mlinzi aweza sinzia/ama akaenda kutafuta utumbo wa kuja kupikia ndizi)
Ongee vizur na majirani -- huenda mwizi ni alokuuzia shamba
Hahaa hizo ndizi za kupika na utumbo ndio atakuwa anapatia hapo hapo mkuu?
 
Mambo ,nikodishe hilo eneo
Mkuu uko mkoa gani ndizi zinastawi?maana mi ninaeneo langu hapa dar maji yapo inakaribia miaka miwili eneo linakaa tu naona nimeshawishika na hiyo kilimo chako sasa ndo sijui kustawi kwake
 
Kuna jamaa miaka ya nyuma huko ilikuwa ukienda kuiba mbao zake badala ya kupeleka ulikokusudia, unapeleka nyumbani kwake.

Ukifika unamkuta anakusubiria, anakuelekeza sehemu ya kuweka then ndio akili zinakujia unaondoka kwa aibu.
Yaani yeye ukienda kuiba tu, anapata alert anaanza kukusubiri nyumbani kwake na kuandaa vizuri sehemu ya kuweka.
Hii nzuri😂😂 ila mimi akili zikinirudia nazibeba tena hizo mbao hapo kwake aaii ,yaani nimbebee bure bure tu😂
 
Mkuu uko mkoa gani ndizi zinastawi?maana mi ninaeneo langu hapa dar maji yapo inakaribia miaka miwili eneo linakaa tu naona nimeshawishika na hiyo kilimo chako sasa ndo sijui kustawi kwake
Raha ya ndizi nipale ninapokata kwa ajili ya chakula cha familia yangu nasikia raha sana
 
Back
Top Bottom