Mbunge Malleko awasilisha maombi ya Teknolojia kwenye Kilimo cha Ndizi, Kilimanjaro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE ESTHER MALLEKO AWASILISHA MAOMBI YA TEKNOLOJIA KWENYE KILIMO CHA NDIZI, KILIMANJARO

"Tanzania tunazalisha kahawa tani 80,000 kwa sasa, huko nyuma tulikuwa tunazalisha tani 61,000 za kahawa, tumepiga hatua. Lakini pia fedha za kigeni tunazoziingiza kupitia mauzo ya kahawa ni takriban dola milioni 230" Esther Maleko, mbunge viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Tunahitaji teknolojia katika zao la ndizi ikiwemo mashine za kisasa za kuchakata na kuongeza thamani zao la ndizi, jambo litakalopelekea kuuza ndizi ambazo zimeshachakatwa nje ya nchi kama malighafi na itatuongezea kipato" Esther Maleko, mbunge viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Katika zao la ndizi akina mama wa Mkoa wa Kilimanjaro wanahitaji kupata miundombinu ya umwagiliaji ili waweze kupata mavuno ya kutosha, katika hili naishauri serikali iweze kuboresha mifereji ya asili ya zamani ili iweze kusaidia katika kilimo cha umwagiliaji" Esther Maleko (Mb)

"Jambo la muhimu kwa Wizara ya Kilimo ni kuona namna ya kutupatia masoko ya zao la ndizi nchini na nje ya nchi, pia tunaweza kutumia balozi zetu kutangaza zao na ikizingatiwa mkoa wetu wa Kilimanjaro una uwanja wa ndege hivyo tutautumia kusafirisha ndizi zetu" Esther Maleko (Mb)

"Katika Mkoa wa Kilimanjaro tuna changamoto ya vituo vya kuuzia ndizi zetu akina mama wanateseka sana, ukienda kwa Sadala saa 12 asubuhi utawakuta akina mama wetu wameshafika na mikungu ya ndizi shida ni kwamba hakuna soko, hivyo jua linawapiga na mvua zinawanyeshea, akina mama wa Mamsera hivyo hivyo hata wa Mwika nao wanauza ndizi barabarani na kuna msongamano mkubwa" Esther Maleko, mbunge viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Naiomba Wizara ya Kilimo ione umuhimu wa zao la ndizi na iwape wakulima wa Kilimanjaro mbegu bora za ndizi zinazoendana na hali ya hewa ya mkoa huu ili akina mama wa Mkoa wa Kilimanjaro waache kulima ndizi za kizamani ambazo sasa zimepitwa na wakati zinazotoa mavuno machache na kushambuliwa sana na magonjwa" Esther Maleko, mbunge viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro

Mbunge viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Esther Maleko ameiomba Wizara ya Kilimo iangalie uwezekano wa kuwekeza katika utafiti ili kuweza kupata mbegu bora za zao la ndizi ambazo zitaweza kuwaingizia kipato cha kutosha wakulima wa zao hilo ikiwemo wakulima wa mkoa huo

"Wizara ya Kilimo ione namna gani ya kuwasaidia akina mama wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwakopesha ili waweze kufanya biashara zao na kuwekeza zaidi katika kilimo cha ndizi" Mhe. Esther Maleko, mbunge viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro.

FvnA8pnWwAIl5SV.jpg
 
Back
Top Bottom