SOKO LA VANILLA KAVU BADO KIZUNGUMKUTI KAGERA

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Maonyesho ya kilimo 2023 yamehitishwa jana nimeshuhudia mazao kadhaa yakipigiwa chapuo kama ilivyokuwa nyuma kwa zao la Vanilla tuliaminishwa bei mpaka Tsh.100, 000/@ lakini mwaka huu imenunuliwa bei sawa na bure Tsh.3, 000/@ wakulima wameamua kutokuirudisha nyumbani maana matumaini ya kupata pesa yameyeyuka ghafla na kugeuka mzigo hii imenikumbusha miaka ya nyuma kidogo nilienda kwenye gulio moja uko Karagwe nikakuta ndizi nyingi bei ilikuwa sh, 800 mpaka Tsh, 500 mkungu mkubwa ila kadili muda ulivyokuwa unasogea ndivyo bei ilizidi kushuka kufika jioni nilishuhudia mikungu ikiwa haina wenyewe uku mgambo wakikimbizana na watu nikataka kujua kwanini mgambo wanakimbizana na wananchi apo ndipo nilichoka akili kabisa mgambo walisema wanawalazimisha watu kuondoa ndizi kwenye maeneo yale kutokana na wananchi kukosa wanunuzi ivyo ukimbia na kuziacha gulioni hali inayosababisha uchafu katika maeneo ayo ndizi zikioza panakuwa hapatamaniki hali inayosababisha wao kufanya usafi kwa siku mbili mpaka tatu.
Naweza kuona kama story lakini ndivyo ilikua miaka kumi nyuma.

Nirudi kwenye Vanilla ivi vitu haviliwi unaweza kufa njaa unavyo ndani japo kwenye soko la dunia vinaoneka kuwa na bei kubwa sana kila kukicha mkoa wa Kagera tunaendelea kukumbwa na vikwazo vya kiuchumi uku serikali ikipiga taralila mpaka tunajiulia mbona serikalii ilinunua Korosho zote za wakulima kule kusini?

Kwanini Vanilla ikose soko wakati tuna wabunge? Mbunge asiyeweza kutatua kero uyo ana tofauti gani na kero yenyewe? Leo Vanilla imekuwa mzigo kwa wakulima ni mbunge mmoja tu alinipigia simu kutaka kujua hali halisi ya Vanilla apa Kagera nitamleta kwenu akifanikiwa kuleta mnunuzi wa Vailla kavu inayotesa wakulima mpaka sasa. Kumbuka Vanilla mbichi imeuzwa lakini kuna waliokuwa wameisha ikausha kuepuka uharibifu lakini sasa inawatesa mpaka sasa inasekadiliwa kuwa tani 10 hizi ni fedha nyingi ni zaidi ya 200B kama ingeuzwa sh.200, 000/@ fikiri mkoa unapoteza pesa zote hizi alafu tuanatafuta mchawi wa maendeleo ya Kagera?
Jibu ni moja wabunge wote wa kusini waliazimu kuiadhibu serikali isipopata muafaka wa soko la KOROSHO mnakumbuka Serkali ilizinunua sijui walipekeka wapi?
Sasa Kagera tuna wabunge wa aina gani? Je wanastahili kuendelea kutuwakilisha? Kama tungekuwa na katiba inayorudisha madaraka kwa wananchi awa wabunge wote tungewaondoa kabisa wabunge wasiojua wajibu wao, Kahawa haina mtetezi, Vanilla haina mtetezi, Ndizi hazina mtetezi tulichakazwa na mnyauko wa migomba mapa leo miaka zaidi 20 tupo tunateseka wenyewe lakini wabunge kwa miaka yote hii wanaangaika na matumbo yao na familia zao.
Apa dawa ni moja kuwafuta wabunge wote tupeleke wawakilishi sio awa wanaosubiri kwenye kampeini kuja kudhamini vyama vya ujima na sakosi na kulala misibani ili wanunue gongo na kulevya wananchi wasioweza kupambanua.
Umasikini wa Kagera unatokana na ujinga ambao ndio mtaji wa watawala.
@Katikamabama
IMG_20230724_120716_080.jpg
 
Ogopa kulima zao linalo tiliwa mkazo na serikali ya tanganyika na wanasiasa wake. Ukiweza pishana nao kwenye maagizo yao.
 
Back
Top Bottom