Mwizi aliyetajwa na Magufuli kuiba milioni saba kwa dakika asomewa mashtaka 199

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Mtuhumiwa mkuu wa kesi ya kughushi risiti na kuisababishia TRA ukosefu mkubwa wa mapato Mohamed Mustafa Yusuffali na wenzake wanne wamependishwa mahakama ya Kisutu na kusomewa mashataka.

Mshatakiwa wa kwanza Mohamed Mustafa Yusuffali anakabiliwa na mashtaka 199 na wenzake 4 wanakabilwa na mashtaka ya kushirikiana kughushi nyaraka, ila kuna shitaka la utakatishaji fedha ambalo linawakabili washtakiwa wote watano, watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi shauri lao litakapotajwa tena.

Watuhumiwa wengine ni Alois Gonzaga Mandago, Mohamed Seif Kabula, Isack Wilferd Kasanga Tahlal.

Mawakili wa serikali wa kesi hiyo ni Shadrack Kimaro, Raymond Swai na Pius Hilla
 
Nilitarajia kesi hii ingepelekwa Mahakama ya Ufisadi iloanzishwa majuzi na serikali ya Mzee Pombe. Nilitarajia hivyo kwa sababu inagusa kwa sehemu KUBWA wstumishi na watendaji wa serikali - TRA na Wizara. Imekuwaje kesi rahisi ya kusikiluzwa na Makama ya chini kama Kisutu!!!???
 
Sanaa zimeanza kwa hiyo kesi za mafisadi zimeanza kusikilizwa kisutu, hiyo mahakama ya mafisadi itafanya kazi gani sasa
 
acha waisome namba ndo inavyotakiwa na bado ,mwaka huu mengi yatatokea ya watu iliokuwa inaaminiwa ni watu wasioshtakika kushtakiwa
 
Mtuhumiwa mkuu wa kesi ya kughushi risiti na kuisababishia TRA ukosefu mkubwa wa mapato Mohamed Mustafa Yusuffali na wenzake wanne wamependishwa mahakama ya Kisutu na kusomewa mashataka
Mshatakiwa wa kwanza Mohamed Mustafa Yusuffali anakabiliwa na mashtaka 199 na wenzake 4 wanakabilwa na mashtaka ya kushirikiana kughushi nyaraka, ila kuna shitaka la utakatishaji fedha ambalo linawakabili washtakiwa wote watano, watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi shauri lao litakapotajwa tena
Watuhumiwa wengine ni Alois Gonzaga Mandago, Mohamed Seif Kabula, Isack Wilferd Kasanga Tahlal
Mawakili wa serikali wa kesi hiyo ni Shadrack Kimaro, Raymond Swai na Pius Hilla

Usishangae akipangua mashtaka hayo yote 199
 
Nilitarajia kesi hii ingepelekwa Mahakama ya Ufisadi iloanzishwa majuzi na serikali ya Mzee Pombe. Nilitarajia hivyo kwa sababu inagusa kwa sehemu KUBWA wstumishi na watendaji wa serikali - TRA na Wizara. Imekuwaje kesi rahisi ya kusikiluzwa na Makama ya chini kama Kisutu!!!???
Miluzi mingi..... mkuu Nyetk pamoja na wengine nadhani mmeshaelewa na ndio maana unahoji. Kuwa makini maana ukihoji utahojiwa!
 
Nilitarajia kesi hii ingepelekwa Mahakama ya Ufisadi iloanzishwa majuzi na serikali ya Mzee Pombe. Nilitarajia hivyo kwa sababu inagusa kwa sehemu KUBWA wstumishi na watendaji wa serikali - TRA na Wizara. Imekuwaje kesi rahisi ya kusikiluzwa na Makama ya chini kama Kisutu!!!???
Kesi zote zinaanziaga mahakama ya Kisutu na kuhamishiwa mahakama za juu. Wakipelekwa Kisutu wanakatazwa kujibu mashtaka kwa kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi husika.
 
Back
Top Bottom