Kesi ya aliyetajwa na Rais Magufuli kuhamisha mil 7 kila dakika na wenzake yafutwa, wakamatwa tena na kupelekwa mahabusu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
aliyetajwapic.jpg


Mahakama ya Hakimu Mkazi imewafutia mashtaka mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa alikuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake wanne.

Mfanyabiashara huyo na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif wanakabiliwa na mashtaka 198 ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni.

Washtakiwa hao wamefutiwa kesi hiyo, chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashim Ngole amedai mahakamani hapo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea nalo dhidi ya washtakiwa hao.

Hakimu Augustina Mmbando amesema shauri hilo lilikuja chini ya kifungu namba 91(1) cha CPA, sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Hakimu Mmbando amesema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa mahabusu.

Chanzo: Mwananchi
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Safi Sana Sana
Tajiri Anaweza Kufanywa Chochote
 
Kwahiyo hakuna ushahidi kwamba alishiriki kujipatia Tsh7m kila dakika. Nahisi ingekuwa hivyo angekuwa moja ya matajiri maarufu Tz
 
Yasije yakatokea tena kwa wale askari waliokamata dhahabu huko Mwanza, kwani Rais alisema anaouhakika walipewa taslim Sh 700,000,000.
 
Safi sana, tunashukuru kuna jamaa yetu hapo yuko huru, kapewa nafasi nyingine kimaisha aishi kama sisi (maskini), ila raha...
 
Back
Top Bottom