Aliyetajwa na Rais Magufuli kuiba Mil.7 kwa dakika asomewa "mashtaka 600".

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
January 11, 2019 Mfanyabiashara Mohamed Yusufal aliyetajwa na Rais John Magufuli kuiba Mil.7 kwa dakika na mfanyakazi wake, Arital Paliwala wamesomewa mashtaka 600 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya Bilioni 14.98.
YUSUFALI-660x400.jpg


Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la Mawakili wa serikalo wakiongozwa na Hashimu Ngole mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Katika mashtaka hayo yaliyosomwa kwa takribani saa mbili, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kuwasilisha taarifa za mwezi za mahesabu ya uongo kwa TRA, kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya sh. 14,987,707,044.58

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kuisababishia serikali hasara, ambapo wanadaiwa kukwepa kodi ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2015 kupitia kampuni ya Pamplant ltd iliyokuwa inamilikiwa na mshtakiwa Yusufali ambapo mshtakiwa Paliwala alikuwa mfanyakazi wake.

Pia inadaiwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakiwa wanatumia stakabadhi za kughushi pamoja na kutumia makampuni ya kughushi wakidai kuwa wamenunua vitu kutoka katika makampuni mbali mbali wakati wakijua baadhi ya kampuni hizo ni za kughushi huku zikiwa hazijasajiliwa Brela.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeshakamilika ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi
January 24, 2019.
 
Nakuahidi kuwa nitayasoma yote mkuu.
Trust me!!
Utakutana na DUPLICITY OF CHARGES, MISJOINDER OF COUNTS, MISJOINDER OF ACCUSED PERSON. Weaknesses na Error of Facts and Law kibaooo, kama zote mkuu!!!

All the best kaka, ila nisamehe nliandika comment ilekwa masihara sikudhani ulikua unahitaji CHARE SHEET ya hawa jamaa (Ila nikiipata ntaku PM).
 
Back
Top Bottom