Yule Mfanyabiashara kinara wa kutakatisha Milioni 7 kwa dakika hatimaye afikishwa Mahakamani


Hot Lady

Hot Lady

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
1,035
Likes
230
Points
160
Age
67
Hot Lady

Hot Lady

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
1,035 230 160
1.jpg

Mfanyabiashara Mohamed Mustapha (anayeongea na simu) na wenzake, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kukabiliana na tuhuma za kuibia Serikali kodi ya Sh milioni 7 kwa kila dakika kwa kipindi kirefu.
**
Hatimaye mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuwa amekuwa akiibia Serikali takriban Sh7 milioni kwa dakika, amepandishwa kizimbani na wenzake wanne na kusomewa mashtaka 199, wote kwa pamoja.

Mfanyabiashara huyo, Mohamed Mustafa Yusufali na wenzake Alloyscious Gonzaga Mandago, Isaac Wilfred Kasanga, Taherali Sujjauddin Taherali na Mohamed Seif Kabla, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa mamlaka za Serikali, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh15 bilioni.

Katika ya mashtaka hayo, Yusufali maarufu kwa majina ya Mohamedali, Choma au Jamalii anakabiliwa na mashtaka 198 yeye peke yake huku wenzake wakikabiliwa shtaka moja la utakatishaji fedha.

Kutokana na wingi wa mashtaka hayo, waendesha mashtaka wawili; Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai walilazimika kubadilishana ili kuwapa muda wa kupumua.

Kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na shtaka la kutakatisha fedha, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kulingana na mashtaka yanayowakabili, hayana dhamana.

Baada ya kumaliza kuwasomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hivyo, Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo aliamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu hadi Julai 25, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Kabla ya kupandishwa kizimbani, Yusufali alitajwa na Rais Magufuli kuwa ana mashine inayotoa risiti za kielektroniki (EFD) nje ya mfumo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuzisambaza kwa wafanyabiashara wengine, hivyo kujiingizia Sh7 milioni kwa dakika.

Rais Magufuli alieleza kuwa mtandao wake unawashirikisha watumishi wa TRA na Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela), hivyo kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.

Katika mashtaka hayo, Yusufali anakabiliwa na mashtaka 181 ya kughushi, mashtaka 15 ya kuwasilisha nyaraka za uongo, udanganyifu katika kulipa kodi moja, shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh15,645,944,361, huku shtaka moja tu la utakatishaji fedha ndilo likimhusisha na wenzake.

Waendesha mashtaka hao walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akighushi nyaraka za kampuni mbalimbali, kuonyesha kuwa zimesajiliwa na zinaendesha shughuli zake nchini kihalali wakati akijua siyo kweli.

Pia, walidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akiwasilisha nyaraka za uongo TRA.
Kuhusu shtaka la kutakatisha fedha, upande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja kati ya Machi 2011 na Januari 2016, walitakatisha Sh1,895,88500 kwa kujifanya kuwa ni malipo ya mikopo waliyoipokea kwa watu mbalimbali.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa kati ya Januari 2008 na Januari 2016, mfanyabiashara huyo alifanya udanganyifu katika kuwasilisha kwa Kamishna Mkuu wa TRA taarifa ya uongo ya marejesho ya mapato, hivyo kuikosesha Serikali mapato ya kodi ya VAT zaidi ya Sh15.6 bilioni.

Kwa Hisani ya MPEKUZI
 
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Messages
11,295
Likes
7,320
Points
280
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2014
11,295 7,320 280
Yaani hata pingu hawajafungwa... kweli wapo Salaama !!!!!!
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
Safi sana Rais JPM. Yaani mahakama ya majizi na mafisadi yakianza kazi, lazima watu wakimbie nchi
 
Nduka

Nduka

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2008
Messages
8,524
Likes
833
Points
280
Nduka

Nduka

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2008
8,524 833 280
Kuna vijana kadhaa waliwahi kufungwa kwa wizi wa shilingi bilioni saba benki ya Barclays, hawa jamaa wawili hapo Gonzaga na Isaack ndio walikuwa ma mastermind. Sasa naona Mungu anawaadhibu sasa kwa kukatisha ndoto za wale vijana.
 
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Messages
16,255
Likes
15,360
Points
280
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2014
16,255 15,360 280
Mahakama ya mafisadi ikifika lazma tuazime magereza nchi jirani ya Rwanda!
 
alberaps

alberaps

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
1,545
Likes
881
Points
280
alberaps

alberaps

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
1,545 881 280
Sasa kumbe kaiba Bilion 15.6

Ina maana alitumia masaa chini ya 38 kuiba. Kulikuwa na haja gani ya kutafuka Kiki kwa kusema 7M Per Min?
 
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Messages
11,295
Likes
7,320
Points
280
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2014
11,295 7,320 280
Mkuu, uliwahi kwenda Mahakamani? Au ndo utaahira wenyewe huu?
Mkuu nimeona wakipanda private car baada ya kutoka mahakamani kama vile wapo huru mzagaozagao....
"kwa nchi zingine 500m tu unavushwa border ktk dkk 10 tu"
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
Kuna vijana kadhaa waliwahi kufungwa kwa wizi wa shilingi bilioni saba benki ya Barclays, hawa jamaa wawili hapo Gonzaga na Isaack ndio walikuwa ma mastermind. Sasa naona Mungu anawaadhibu sasa kwa kukatisha ndoto za wale vijana.
Safi sana. Rais Magufuli ni mtetezi wa wanyonge
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
Mkuu nimeona wakipanda private car baada ya kutoka mahakamani kama vile wapo huru mzagaozagao....
"kwa nchi zingine 500m tu unavushwa border ktk dkk 10 tu"
Mkuu, una uhakika na unachosema? Pole sana ndugu inaonekana chuki yako kwa serikali ni ya mwendokasi
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
Mahakama ya mafisadi ikifika lazma tuazime magereza nchi jirani ya Rwanda!
Kuna nchi nilisoma kuwa inataka kufunga magereza yake 19 kwa kukosa wafungwa. Inafaa tuwahamishie huko
 
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Messages
11,295
Likes
7,320
Points
280
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2014
11,295 7,320 280
Mkuu, una uhakika na unachosema? Pole sana ndugu inaonekana chuki yako kwa serikali ni ya mwendokasi
Mkuu, Wewe mbona umerukia neno CHUKI !! yaani tusijufunze tahadhari au tusijizoeshe weledi wa kufanya kazi !! Dunia ya 1900 siyo tena Dunia ya 2016 !!! Share knowledge kama mwendokasi!!
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
13,596
Likes
10,820
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
13,596 10,820 280
Hukumu ya kifo itumiwe kwenye makosa kama haya.
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
Mkuu, Wewe mbona umerukia neno CHUKI !! yaani tusijufunze tahadhari au tusijizoeshe weledi wa kufanya kazi !! Dunia ya 1900 siyo tena Dunia ya 2016 !!! Share knowledge kama mwendokasi!!
Chuki, husda, wivu vitawaangamiza vijana wengi
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
Hukumu ya kifo itumiwe kwenye makosa kama haya.
Tukimnyonga hatajutis. Naona tutumie ile Sheria iliyopo kwenye Sharia Law ya kumkata Mkono wa kulia na Mguu wa Kushoto. Atajutia maishani mwake. Na tukishakata huo mkono na mguu, tutengeneze supu na tumlazimishe ainywe mpaka kuimaliza na mifuoa yake atafune
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,803
Likes
49,901
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,803 49,901 280
Watumbuliwe tu maana tumechoka na mafisadi
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
13,596
Likes
10,820
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
13,596 10,820 280
Tukimnyonga hatajutis. Naona tutumie ile Sheria iliyopo kwenye Sharia Law ya kumkata Mkono wa kulia na Mguu wa Kushoto. Atajutia maishani mwake. Na tukishakata huo mkono na mguu, tutengeneze supu na tumlazimishe ainywe mpaka kuimaliza na mifuoa yake atafune
Kwa hela aliyotuibia atakubali akitoka atatengeneza mkono wa bandia na mguu wa bandia hela aliyoiba ni nyingi saana.ANYONGWE TU MPAKA AFE.
 

Forum statistics

Threads 1,237,666
Members 475,675
Posts 29,296,673