Sakata la Sh. Milioni 7 kwa dakika: Kasanga wa Easy Finance apandishwa kizimbani wasomewa makosa 199

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
976
47
Isaack Kasanga wa Easy Finance ni mmoja kati ya watu waliopandishwa kizimbani Kisutu kwa tuhuma za kuiibia TRA kupitia EFD.

isaac.jpg


Easy Finance wamewahi kujadiliwa humu JF, soma Easy Finance matapeli?

Habari zaidi zinasema...

WATANO (5) WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUJUMU UCHUMI KUPITIA MASHINE ZA EFD


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tarehe 12/7/2016 imewafikisha Mahakamani washtakiwa watano (5) ambao ni Bw. Mohamed Mustafa Yusufali ambae pia anajulikana kama Mohamedali au Choma au Jamalii; Bw. Alloyscious Gonzaga Mandago; Bw. Isaack Wilfred Kasanga; Bw. Taherali Sujjauddin Taherali na Bw. Mohamed Seif Kabula. Washtakiwa wote wanashtakiwa kwa makosa ya Uhujumu Uchumi kupitia mashine za EFD kwa Kughushi na Kuwasilisha nyaraka za uongo TRA kinyume na vifungu vya Kanuni ya Adhabu Na. 333,335(a), 337 na 342 (Cap 16 R.E. 2002. Kosa lingine ni kukwepa kodi kinyume na kifungu Na. 47 cha Sheria ya Kodi na kuisababishia TRA hasara kinyume na Aya ya kwanza na vifungu 57(1) na 60 (2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi pamoja na kosa la kutakatisha fedha kinyume na Vifungu Na. 12 (c) na 13 (1)(a) vya Sheria ya Kutakatisha fedha Haramu ( Money Laundering Act No. 12/2006 ).

Kesi hiyo Na. 28 ya mwaka 2016 ilisomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe . Shahidi ambapo Mshtakiwa wa kwanza Bw. Mohamed Mustafa Yusufali anashtakiwa kughushi Vyeti vya usajili vya Kampuni 148 na kuisababishia serikali hasara ya kiasi cha 15,645,944,361 /= kwa kukwepa kodi na 1,895,885,000/= kwa kutakatisha fedha.

Kwa upande wa Jamhuri kesi hii inasimamiwa na waendesha mashtaka wa Serikali Shedrack Kimaro na Pius Lila pamoja na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Leonard Swai.

Washitakiwa wote watano wamepelekwa rumande, wamekosa dhamana kwani makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha haramu hayana dhamana kwa mujibu wa Sheria.Kesi hii itatajwa tena tarehe 25/7/2016

IMETOLEWA NA OFISI YA AFISA UHUSIANO, TAKUKURU MAKAO MAKUU

13/7/2016

========

Wahujumu uchumi 5 wapandishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa watano wanaokabiliwa na kesi ya kuhujumu uchumi akiwemo mtuhumiwa namba moja Mohamed Mustapha wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na makosa mbalimbali ikiwemo kugushi nyaraka mbalimbali ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume cha sheria.

Wakisomewa hati ya mashtaka katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mawakili wa serikali Shadrack Kimaro akisaidiana na Pius Hila na wakili Leonard Swai kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mbele ya hakimu Huruma Shahidi, wamesema watuhumiwa hao akiwemo mtuhumiwa namba moja Bwana Mohamed Mustapha maarufu kwa jina la Mashine au mzee wa milioni saba kwa dakika moja, wanashtakiwa kwa kosa la kuhujumu uchumi baada ya kudaiwa kufanya makosa mbalimbali kwa miaka tofauti ikiwemo makosa ya kugushi nyaraka kwa kutumia majina ya makampuni tofauti ili kukwepa kodi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Licha ya kusomewa mashtaka 199 mbele ya hakimu Huruma Shahidi na kesi hiyo kuchukua muda wa zaidi ya saa 6 watuhumiwa wakisomewa mashtaka, inadaiwa kwamba makosa yaliyofanywa na watuhumiwa hao wakiongozwa na Bwana Mohamed Mustapha imesababisha serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 15.6.

Akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama wakili wa upande wa washtakiwa Hadson Lusiepo, amesema mshtakiwa namba moja Bwana Mustapha Mohamed ameonekana kuwa na makosa mengi tofauti na watuhumiwa wengine.

Kutokana na ukubwa wa kesi hiyo ya kuhujumu uchumi, watuhumiwa wote kwa pamoja hawakuruhusiwa kujibu au kuongea chochote, ambapo hawakuruhusiwa kupewa dhamana kutokana na kesi ilivyo ambapo kesi hiyo itakapotajwa tena mnamo Julai 25 mwaka 2016.

Chanzo: ITV
 
Efd na watoa mikopo wapi na wapi....labda kuna issue nyingine.
 
Nachoona hapa picture imeng'ang'anizwa caption hatimaye ikaundiwa kichwa cha habari kinachoendana na tukio la hivi karibuni. Ochu una uhakika hiyo picha na kichwa cha habari vinaenda sawa au ..........
 
hivi hawa siku zote hizi walikua hawajakamatwao_O wameumiza watu wengi sana kwa kupora magari na majumba kisa wameshindwa kulipa mikopo yao kwa style ya kitapeli tapeli... ngoja tuone mwisho wa hili sakata ni wapi, maana shida ni pale tunajua kuanzisha lakini kumalizia ni shida.
 
Back
Top Bottom