Mwita Waitara apokelewa na maelfu ya wapiga kura wake, hii ni uthibitisho kuwa aliiangusha ngome ya CHADEMA Tarime

Kila uchaguzi? Tarime miaka yote ni ngome ya upinzani tokea miaka ya 90 hilo lipo wazi.... Hilo jimbo CCM walibeba 2010 na kelele zikawa nyingi sana ila 2015 likagawanywa na bado yakabebwa na upinzani na halmashauri ikabebwa.

So hata 2025 yatarudi tu CHADEMA maadam uchaguzi utakua fair walau kma 2015 na 2010!

Ni mpumbavu tu anayeweza kuamini majimbo yote yaliichagua CCM hiko kitu hakipo duniani kote hata Mandela na umaarufu wote ule alishinda kwa 60% pekee na bado makaburu yakazoa viti zaidi ya 80!! Demokrasia ni two way traffic
Unakumbuka kampeni aliyoifanya Waitara kuivuruga Chadema huko Tarime kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020? Nini kilifanyika jibu unalo.

Ni kweli Tarime ilikuwa ngome ya Chadema, lakini baada ya Wangwe kufariki nguvu imekwisha kabisa, na Waitara ndio alikuja kumalizia kabisa kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

Kama watu wameikubali Ccm kuna ugumu gani wasichague majimbo yote mawili, acha kupotosha watu.

Usilete mfano wa uchaguzi wa South Africa ambao kura mpaka leo hugawanyika kwa kuangalia rangi na ukabila. Kwa jimbo kama Western Cape panga pangua lazima National Party wapate kura nyingi. Weka mifano inayorandana na uhalisia.

Unadhani Tarime ya mwaka 2010 ndio ileile? Chadema ya mwaka 2010 ndio ileile?
 
Wangwe aliondoka na ushawishi wa CHADEMA? Mbona Mwera na Heche na matiko wameshinda hapo ubunge tokea afariki? Vipi wale madiwani waliosomba halmashauri kwa kimbunga bado Wangwe alikua hai?

Waitara hana uwezo wa kuichafua CHADEMA sababu aliwakimbia wana Tarime walipomkataa 2010 akaenda Dar so kule wanamuona wakuja tu!! Heche amedumu toka akiwa diwani mpaka mbunge sasa so ushawishi wake hauwezi angushwa ndani ya mwezi mmoja tu.

Narudia tena ccm haikubaliki Mara majimbo 6 ya bunda,serengeti,tarime, musoma yaani yameichoka kabisa CCM na yalikua na muitikio mkubwa sana wa CHADEMA kama sio mfumo kuingilia uchaguzi kungekua na wabunge 6 wa CHADEMA hapo mara na trust me hiyo 2025 hao 6 watapeta.

Kuhusu SA inaonekana siasa zao huzifahamu hyo National party mbona kishafutika? Western cape ni chini ya DA!! My point is kwenye nchi yoyote ya kidemokrasia hata upendwe vp huwezi pata above 70% wanaokupinga watakuwepo tu.
 
Nilikosea kidogo tu nikachanganya kati ya DA na National Party. Hivyo usinihukumu kuwa sijui siasa za huko. Lakini nilichomaanisha umenipata.

Kwani kipi kinafanya chama cha siasa kukubalika? Si kuwa na sera nzuri, utekelezaji na kuwa na wanasiasa bora.

Sasa unadhani Ccm haijafanya mabadiliko ili kuwashawishi watu wa Tarime mpaka unakariri zama za 2010?

Kwamba Wangwe aliondoka na ushawishi nalo hujui?

Kwamba Waitara alifanya mikutano na kuibomoa ngome ya Chadema Tarime napo unakataa?

Eti kwa sababu ya demokrasia chama cha siasa hakiwezi kukubalika kwa 100% hata kama kinafanya vizuri kutekeleza sera zake na kuwatulikia wananchi? Sio kweli siasa sio masuala ya kukariri.

Hata wewe unafaham kidogo aliyekua anakubalika ni JPM sio CCM ndio maana 2015 mkasema chagua Magufuli sio chagua CCM hilo liko wazi kabisa.

Tarime imepaa sana chini ya CHADEMA kwa miaka zaidi ya 20 sasa!! So hawawezi rudi CCM ilihali tokea uhuru wameshindwa kuwaletea maendeleo ndio leo warudi? Cha kujiuliza maeneo kama Rorya ambayo ni koloni la CCM kwa miaka 60 sasa ina nini cha maana kuzidi Tarime??

Chama cha siasa hakipimwi kutekeleza ilani bali wawakilishi walivyosimamia matakwa ya wananchi wao na ndio maana kuna maeneo huwa Rais anashinda chama kingine na mbunge anatoka chama kingine.

Mfano wabunge wa CCM waligeuka watetezi wa serikali badala ya wananchi mfano suala la korosho ina maana Lindi na Mtwara wangeangushwa tu.

Muswada wa mapato ya gesi na mafuta walipitisha CCM na baadae wakaforciwa na JPM waufanyie mabadiliko sababu umekaa kiwizi tu. Unadhani hapo wananchi watampigia kura mbunge wa CCM??

Upinzani kwa miaka 20 sasa umejijenga sana kupitia bunge na kusimamia maslahi ya wananchi so evaluation yao iko hapo whether JPM atafanya hiki au kile mchango wa mbunge kwenye kubarakisha maendeleo utakua ndio kipimo cha kuchaguliwa bila kujali chama.

Kwa kulijua hilo waitara alikimbilia Tarime maana alijua hapo Ukonga asingeambulia hata kura moja sababu alifeli kuwakilisha vyema wananchi wake.
 
Chama cha siasa hakipimwi kwa kutekeleza ilani bali kwa kutekeleza matakwa ya wananchi? Hujui kuwa hata wabunge wa upinzani hutekeleza ilani ya chama tawala? Hapa umebugi.

Kwamba Tarime ilipaa sana chini ya uongozi wa Chadema sio kweli. Walikuwa na wabunge waliojali harakati zaidi ya kutumikia wananchi, ni hichi ndio kimewacost vibaya sana.

Kuhusu sakata la korosho,serikali ilikuwa na nia nzuri kabisa ya kuwasaidia wakulima. Kama haukuleta matokeo mazuri ilikuwa ni bahati mbaya. Sio kila nia njema italeta positive results

Muswada wa mapato yamafuta na gas ulibadilishwa kwa manufaa ya taifa au Ccm? Sijakuelewa huo wizi unaosema ukoje.

Kwa ujumla ili mbunge afanye maendeleo jimboni kwake lazima asimamie ilani ya chama tawala vizuri.

Chadema kwa hapo Tarime walishindwa na kubakiza harakati zilizopitwa na wakati.
 
1. CHADEMA kupaa Tarime siongelei wabunge tu balo halmashauri ilokua chini ya CHADEMA kwa miaka mingi sana so walijijenga sana na kuikamati haswaa.

2. Chama cha siasa ngazi ya Urais ndio atajinadi kupitia ilani sababu ni Macro economic strategy ila ngazi ya ubunge hawatoongelea ilani ya kitaifa watataka kujua ww kama mbunge matatizo yao yalikua implicated na ilani au bungeni? Ajira million 8 ni za kitaifa ila je jimboni kwako ajira zilikuja ngapi? SGR ni ya kitaifa ila je katika jimbo lako walinufaikaje? Hiyo ndio tofauti ya ilani ngazi ya ubunge na Urais. So whether ilani itekelezwe 100% ila kama jimbo lako limebaki nyuma hupati kura.

3. CHADEMA hawatekelezi ilani ya CCM bali mpango wa taifa ambao unatoholewa kutoka vision 2025, sera za taifa na ilani ya chama kilichoshinda, ukishafika tume ya mipango haiwi tena ilani ya CCM bali mpango wa taifa ambapo ndio bajeti hutengenezwa kupitia hayo maoni.

4. Muswada wa mapato ya Gesi wapinzani walipinga ila CCM mlipitisha unadhani wananchi watawapa kura? Mlikuja kuubadili after JPM kuupigia kelele kuwa umeacha loophole nyingi za kifisadi sasa unategemea wananchi hawaoni hayo? Unadhani watatoa kura tu kiaa SGR imejengwa hata kama miswada mibovu imepitishwa?

Ubunge na ilani ya chama havina correlation mkuu kuamua kura zako....
 
Nani kasema?
Kura zilizopigwa siku mbili kabla nenda ofisi za ccm pale kinondoni kaulize . Vijana wasiojielewa walipelekwa pale na kupewa kitabu kila mmoja. Walijipigia Kura za ndiyo kwa magufuli. Waliahidiwa 5000/= hawajapewa mpaka leo
Hii ilifanyika nchi nzima. Kaulize pale jumba la maendleo kibondo.nn kilitokea
Sijui unaishi wapi
 
Unakumbuka kampeni aliyoifanya Waitara kuivuruga Chadema huko Tarime kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020? Nini kilifanyika jibu unalo.

Ni kweli Tarime ilikuwa ngome ya Chadema, lakini baada ya Wangwe kufariki nguvu imekwisha kabisa, na Waitara ndio alikuja kumalizia kabisa kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

Kama watu wameikubali Ccm kuna ugumu gani wasichague majimbo yote mawili, acha kupotosha watu.

Usilete mfano wa uchaguzi wa South Africa ambao kura mpaka leo hugawanyika kwa kuangalia rangi na ukabila. Kwa jimbo kama Western Cape panga pangua lazima National Party wapate kura nyingi. Weka mifano inayorandana na uhalisia.

Unadhani Tarime ya mwaka 2010 ndio ileile? Chadema ya mwaka 2010 ndio ileile?
Sidhani kama umeelewa alichomaanisha mwananzengo. Anapotaja ngome, anazungumzia eneo maalum lenye nguvu kubwa Kinzani na yenye mizizi iliyo hai. Kama Waitara alikuwaamesha sambaratisha ngome ya CDM, kulikuwa na haja gani ya jeshi la POLISI kuvamia kambi ya Heche na kuharibu mpaka vyombo vya PA????
 
Back
Top Bottom