Liz Senior
JF-Expert Member
- Apr 19, 2007
- 483
- 53
Wakuu mambo ya kuishi bongo ndo kutumia bongo hivo
lakini the bottom line ni kwamba serikalini mshahara wanaotoa wanajua ni mdogo kumwezesha mfanyakazi kutunza familia yake na yeye mwenyewe, kulipa ada, usafiri, kodi ya nyumba etc
na serikali yenyewe ina kigeu geu. mfano ilipowauzia nyumba, kwa kuwakopesha, ilitegemea watalipa kwa hela gani kama zio mishe mishe hizi za makongamano na semina?
So kabla PM hajasema hayo, ni bora kwanza waboreshe mishara.
na ni kweli watu wa serkalini mshahara mdogo lakini maisha yao yapo juu sana kiubora kutokana na hizi nafasi nyingine....
Kaizer, sina ubishi na ukubwa au udogo wa mishahara serikalini lakini hii haihalalishi watu kufanya kazi kinyume na lililokusudiwa...ikiangalia work plan zao na hata implementation haviendani kabisa na huo mkukuta wanaowekea makongamano, vikao na elekezi! sasa hii ina tofauti gani na kuwasamehe mafisadi ikiwa watarudisha? Je tuwaache waendelee kujilipa kwa vile wanalipwa kidogo? Kwani si lilikuwa chaguo lao kufanya kazi serikalini...si soko huria jamani? Wengi wanaingia huko hivi sasa kwa vile kuna pesa nje nje...unafikiri hawajui kuna mishahara midogo? lakini na product yao unaionaje? inastahili mishahara zaidi ya hiyo wanayopata? Profit si inatokana na production? Sasa kauli km za akina Maghembe kweli zinahitaji mshahara mkubwa??