Mwisho wa Mwaka Sitosahau

Jul 26, 2015
49
30
Habari Wakuu

Ni katika Kuzidi tu kushirikishana katika Yale yanojiri Maishani.

Ni Kipindi ambacho Nilikuwa nikihitaji Pesa kuliko Chochote.Kwani Niliamua kurudi Darasani kujiendeleza Kielimu,Tayari Mtoto wa Watu nilikuwa nimemposa na Machache yalibaki kabla ya kumuita My Wife wangu.Ni wakati ambao tayar Nikiendelea kumuhudumia Mama baada ya kugundulika ana Tatizo la Figo.
Kama haitoshi Mlango nao ulikuwa umeshindwa Uvumilivu kutokana na kero za Mikono ya baba Mwenye Nyumba ambae kila Siku hakuacha kufika na kudai Kodi Yake.

Wakati yote yakijiri Ghafla napoteza Kazi...Ambayo Asilimia Tisini ya Niloorodhesha hapo juu ilikamilishwa na Mshahara wa Kazi.

Dunia haikuwa na maana kwangu kwani,kila nilomuona Mzuri wakati na kazi,hakuonekana kunijali kwa lolote sikwambii kuchuniwa Meseji na Simu nilizokuwa Napiga.Rafiki nao Walipungua kwa kiasi kikubwa.

Ilinichukua Muda sana kuja kupambana na hali halisi baada ya kukosa Ajira,Mama huy huy Mgonjw aligeuka tena sehemu ya Faraja yangu na hasa neno lake "Pambana Baba"lilijirudia sna ktk usemi wake kila uchao.

Kiukweli sikusita kupambana na Chochote kilichoitwa ajira hususan kwa njia ya halali,Ilihal tu nisiibe cha Mtu.Nikafany kazi kwa Ujira wa Ujuzi zaidi ya Mwaka Mzima.


Ila kweli Mola Hamtupi Mja wake.Sasa Namshukuru Mola kwa kile ninachoita Muujiza.
Ijapokuwa meng katika nilokuwa na Matarajio nayo hapo juu hayakufanikiwa kwa kiasi kikubwa Angalau hadi hivi sasa naweza sema Mambo si Mabaya Alhamdulillah....!!

Funzo

USIKATE tamaa
MAMA ndie Rafiki wa Kweli
MOLA anajibu


NB:Yamenitokea KWELI Maishani
 
chamsingi ukifanikiwa fanya maendeleo pia malizia masomo yako
 
Mchumba wako alikuwa na wewe kwenye hicho kipindi kigumu au? Pole kwa yote, yalikuwa ni mapito tu, so ashukuriwe Mungu kwa yote
 
Mchumba wako alikuwa na wewe kwenye hicho kipindi kigumu au? Pole kwa yote, yalikuwa ni mapito tu, so ashukuriwe Mungu kwa yote
Hiyo conclusion yake hapo kamtaja mama tu, mchumba huenda aliingia mitini.

Mtoa mada pole, pia asante kwa ujumbu.
 
Back
Top Bottom