RAIS KWA MASAA MAWILI ANATETEA SERA ZAKE KAMA KIONGOZI MKUU WA SERIKALI
Katika mahojiano mubashara, rais ameamua kuongea na waandishi wa habari wa vyombo tajwa ili kuelezea mikakati anayokusudia kukamilisha bila kutegemea msemaji wa serikali kufafafanua bali kuonesha yeye kama rais anaongea moja kwa moja na wananchi kuwashawishi kukubali, kuelewa na kuwa na subira mipango yake aliyoahidi ifanyike
View: https://m.youtube.com/watch?v=NbmiljC23oI
Katika mahojiano mubashara, rais ameamua kuongea na waandishi wa habari wa vyombo tajwa ili kuelezea mikakati anayokusudia kukamilisha bila kutegemea msemaji wa serikali kufafafanua bali kuonesha yeye kama rais anaongea moja kwa moja na wananchi kuwashawishi kukubali, kuelewa na kuwa na subira mipango yake aliyoahidi ifanyike
View: https://m.youtube.com/watch?v=NbmiljC23oI
- Sera ya mkazo ktk majenzi ya makaazi ya maghorofa ili ardhi nzuri kwa kilimo isiliwe na maelfu ya nyumba za ardhini
- Mikopo nafuu wananchi wanunue apartments na flats katika maghorofa nchini kote na hivyo kutunza ardhi yenye rutuba kilimo kifanyike anafafanua rais.
- Kupanda kwa sarafu ya dola na ughali wa maisha, rais anaeleza sababu hasi zinazosababisha hilo.
- Bei ya bidhaa kama chakula, nishati n.k kupaa, rais abainisha mikakati kupunguza makali
- Tozo, kodi za haki kama mahakama ilivyotoa hukumu, rais afafanua
- Serikali yake tayari imepata fursa za ajira 10,000 zaidi nje ya nchi mwaka huu kwa raia wenye ujuzi kama mafundi seremala, mchundo, manesi, madaktari, madereva n.k
- Sera ya bima ya afya kwa wote Wanachi Inawezekana, afafanua rais utekelezaji
- Rais ashangaa hospitali ndogo kabisa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa kuliko hospitali za Rufaa za Kanda na hata zaidi ya hospitali kubwa ya rufaa ya Taifa. Rais asema amebaini yafuatayo;
- Kupiga vita ufisadi uliopo ktk mfuko wa bima ya afya, ambapo rais anatoa mfano hospitali moja ndogo sana ina idadi ya madai ya operesheni kuliko hospitali kubwa kabisa ya Taifa ya Kenyatta National hospital
- Upigaji mfuko wa bima ya afya, hospitali ndogo huandaa huduma za wazi kupima presha n.k Halafu kuchukua taarifa za waliojitokeza kwa kliniki ya wazi ya bure kwenda kukatia bima. Kisha kudai mfuko wa bima wa afya mabilioni ya shilingi kwa operesheni complicated ambazo hazijafanyika. Rais anasema ameamua kupambana na mafisadi hao wa mfuko wa bima ya taifa
- Rais asisitiza sasa hakuna tena nafasi fedha za serikali kuibiwa kupitia ubadhirifu, wizi na rushwa
- Rais anasema mfumo wa kijiditali e-citizen sasa kila kitu kitakuwa wazi na kuminya nafasi ya ufisadi na wizi wa mali za umma
- Rais asema anatoa kila msaada wa rasilimali fedha na watu ili taasisi zote za mfumo wa haki jinai, ofisi ya DPP, mawakili wa serikali kuwa huru, na hadi sasa hajapiga simu kutoa amri kesi ihukumiwe vipi na ni marufuku waziri au ndugu kujaribu kuingilia kazi za taasisi hizi muhimu
- Mradi wa bwawa kubwa la kuvuna maji, rais asema makosa yamesababishwa serikali kudai mabilioni. Tumejifunza kilichotokea huko nyuma na sasa mikataba itakuwa makini zaidi
- Sera ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, rais ambaye ni balozi namba moja afafanua masuala hayo
- Rais asisitiza kuwa hataki kubebwa mgongoni kwa mbeleko hivyo Polisi, wakuu wa taasisi mbalimbali wasiingilie mfumo wa uchaguzi wala siasa bali wamwache apambane kisiasa yeye mwenyewe bila Tume ya Uchaguzi wala nini
- Nishati ya Umeme, nchi kugawanywa ktk zone 5 rais asema
- Deni la Taifa
- Kubana Matumizi ya Serikali
- Waalimu zaidi ya 50,000 kuthibitishiwa ajira zao asisitiza rais
- SGR Reli kipande cha Kenya hadi Uganda kuunganisha DR Congo mpaka Congo Brazaville hatutachukua mkopo bali tunakaribisha wawekezaji kwakuwa tumekopa vya kutosha rais afafanua
- Sakata la DR Congo kumwita nyumbani balozi wao, rais asisitiza Kenya ina uhuru wa habari, haingeweza kuwakamata wakongomani walioita press conference Nairobi ...
- N.k n.k