Mwisho wa mapenzi

Mwisho wa mapenzi

Ni majuto ni huzuni ni msiba inauma na kuumiza roho wengi imewatokea wengi inawatokea na wengi itawatokea ni wachache mno mno ambao hawajaumizwa kimapenzi. Wengi wamechukua maamuzi ya hovyo na ya kudhuru mwili kama kujiua na kuwa mlevi au malaya wa kupindukia
TAFAKARI HAYA
huyo anayekuumiza hukuzaliwa naye na hutakufa naye
wewe si wa kwanza kuumizwa na hutakuwa wa mwisho
Ichukulie hiyo hali kama ajali nyingine zozote
kwamba ni muda tu ndio utaponya majeraha ya mapenzi
Kwamba mwisho wa yote ni lazima maisha yaendelee
BASI FANYA HAYA
Usiwaze kupita kiasi kwakuwa huyo umuwazaye wala hana habari tena nawe
Jifunze kutambua kuwa maisha yamejaa maumivu ya kila aina
Mshukuru Mungu kwa kila jema
wakumbuke webgine wote wakupendae usiwahuzunishe kwa ajili ya mtu mmoja tu
kumbuka yote ya furaha
msiachane kwa visa kashfa na matusi italeta maumivu zaidi ya nafuu


ZIJAPOPITA NYAKATI ZA FURAHA USIHUZUNIKE BALI UFURAHI KWAKUWA ZILIKUWAKO...!

waooooo..very wise words,nmekupenda bureeeee!
 
TEMBEA NA SPEAR TYRE YA AKIBA ikipasuka tumia ile hata kama ni mchina or imezeeka ....
Lzima uwe na option b jman


.........Ni vigumu kujua funguo kama hujui aina ya kofuli.......
 
Usitafute suluhu tena kwakuwa kama hakupendi tena hata ufanyeje hakuna kitakachoyarudisha mapenzi yake kwako
Sepa kaumie kivyako utasahau na maisha yatarudi kama kawaida

Dah... Nimepapendaje hapa!!!
 
Back
Top Bottom