Joel kaigarula
Member
- Jun 3, 2014
- 28
- 16
Kampuni ya Microsoft ilinunua kitengo cha simu za mikononi cha kampuni ya Nokia mwaka 2013 kwa dola za marekani bilioni 7.17. Kama sehemu ya dili hilo, Microsoft ilipewa haki ya kuendelea kutumia jina la Nokia kwenye simu zake. Kampuni ya Nokia kwa sasa inaendelea kufanya shughuli nyingine kasoro utengenezaji simu za mikononi kama vile utengenezaji ramani na utengenezaji vifaa vya mawasiliano na mitandao (telecommunications and networking equipments).
Hatua hii maana yake ni kuwa huu ndio mwisho kamili wa kuwa na simu zinazoitwa Nokia. Je utaweza kuzoea kusema Lumia tochi?
chanzo: bofyatz.com