Mwinyi: Risasi 728 zilitumika mauaji kiwanda cha sukari

Tumbiliwaulaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2020
280
500
Mwinyi: Risasi 728 zilitumika mauaji kiwanda cha sukari

Mwinyi: Risasi 728 zilitumika mauaji kiwanda cha sukari

RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, amesema mauaji ya watu wanne katika mgomo wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero, ni miongoni mwa vikwazo vilivyoutikisa uongozi wake.

Katika kitabu chake cha 'Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu', Mwinyi anabainisha mabomo ya machozi 12 na risasi 728 zilizotumika kwenye tukio hilo, lililosababisha kuhamishwa kwa Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro.

"Mojawapo ya mambo yaliyoniuma sana kuhusu wafanyakazi mwanzoni mwa uongozi wangu ni kile kilichokuja kuitwa mauaji ya Kilombero.

"Mwezi Julai 1986, wafanyakazi kadri ya 500 hivi wa shamba la miwa la Kilombero walifanya mgomo wakidai kuwa wanapunjwa malipo yao.

"Wakagoma kwenda kazini na badala yake wakazingira ofisi na kuwazuia viongozi wa kampuni kuingia ofisini. Katika tafrani iliyotokea mawe yakarushwa na kioo cha gari la kiongozi mmoja kikavunjika," anasimulia.

Mwinyi anakumbusha kuwa askari wa FFU walijaribu kutuliza ghasia kwa mabomu ya machozi na walipoona hali haitulii wakatumia risasi na hatimaye watu wanne wakafariki dunia na wengine 16 wakaumia sana.

Anaendelea kusimulia kuwa taarifa zilipoifikia serikali, ilibidi ichukue hatua huku Bunge nalo likitaka hatua zichukuliwe.

"Chanzo chenyewe kilikuwa kutoelewana na tabia iliyodhihirika ya kuwachukulia wakatamiwa kama 'manamba' na kutojali maslahi yao katika hali ya ubinadamu.

"Kwa kawaida ilikuwa kwamba wanapoanza kazi wakitokea makwao wanawekwa kwenye kambi na kukopeshwa fedha kidogo za kununulia panga la kukatia miwa, nguo, chakula na vyombo vya kupikia.

"Mikopo hiyo ilianza kukatwa kutoka kwenye mishahara yao iliyokuwa Sh. 810 kwa mwezi. Mwezi huo wa Julai wakatamiwa wakajikuta wanabaki na Sh. 100 mpaka 200 tu baada ya makato.

"Kwa kawaida walipaswa kulipwa fedha za kufanya kazi nje ya saa za kawaida, pamoja na bonasi. Malipo hayo ndiyo yaliyokuwa yanawawezesha kuishi, lakini kwa mwezi ule wakawa hawakulipwa malipo ya ziada wala bonasi, ndipo wakajikuta wanabaki na Sh. 100 mpaka 200 tu. Wakaamua kugoma," anafafanua.

Mwinyi anabainisha kuwa askari waliokuwapo walipoona wanazidiwa, wakaomba waongezwe nguvu na Mkuu wa Mkoa akaidhinisha Kikosi cha FFF kutoka Morogoro kiende kutuliza hali.

Anasema baada ya mauaji hayo, walishauriana ndani ya serikali na hatimaye Waziri wa Kazi akateua tume huru ya uchunguzi ya watu sita, ikiongozwa na Jaji B.D. Chipeta.

"Tume ilipowahoji FFU walijitetea kuwa walipiga risasi za moto baada ya kushindwa kudhibiti hali ile kwa mabomu ya machozi. Aidha, waliona mapanga waliyoshika wakatamiwa na kuamini watawashambulia nayo, hivyo wakapiga risasi kujilinda.

"Wakasema pia kuwa kiongozi wao alijihami ndani ya gari na askari wake walipokosa maelekezo yake, wakarusha risasi kujihami kadri walivyoona inafaa.

"Tume haikuridhika na maelezo hayo maana ulipatikana ushahidi kuwa baadhi ya askari waliwakimbiza wakatamiwa hao mpaka kwenye kambi zao na mmoja wa waliouawa alikuwa amejificha jikoni na mwingine chooni.

"Kuta za kambi zilionesha matundu ya risasi. Ilikadiriwa kiasi cha mabomu ya machozi 12 na risasi 728 zilitumika. Mmoja kati ya waliofariki dunia alikuwa mpita njia," anabainisha.

Mwinyi anasema serikali ilipokea na kukubaliana na taarifa ya tume ya Jaji Chipeta na kubaini uongozi wa mkoa wa kisiasa na wa polisi haukutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuifedhehesha serikali kwa matukio hayo ya mauaji.

Anasema tume pia ilibaini udhaifu mkubwa wa uongozi kwenye kampuni ya sukari Kilombero kiutendaji na kisiasa.

"Kampuni ilikuwa shirika la umma, na enzi hizo ilikuwa bado ina tawi la CCM, licha ya tawi la JUWATA (Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania), ambayo nayo kipindi hicho ilikuwa bado jumuiya ya CCM.

"Ilibidi mimi mwenyewe niagize viongozi wa CCM kufanya uchunguzi wa udhaifu wa CCM na JUWATA kiwandani hapo.
"Tulitaka kujua, ilikuwaje wao walikuwapo lakini wakadai hawakuwapo kero na matatizo ya wakatamiwa kiasi cha kuachwa kufuta mpaka yalipolipuka?

"Tume pia ilibaini mazingira magumu sana waliyokuwa wanaishi na kufanya kazi wakatamiwa hao.

"Mmojawapo ya uamuzi wetu kama serikali ikawa kwamba shirika hodhi la sekta ndogo ya sukari (SUDECO), liikopeshe kampuni ya sukari Kilombero Sh. milioni 10 wazitumie kuboresha makazi ya wakatamiwa.

"Pamoja na mambo mengine, tume ya Jaji Chipeta ilituwezesha kufahamu matatizo mengi katika kiwanda hicho na mashamba yake ya miwa.

"Ikabidi tubadili uongozi wote wa juu wa kampuni ya sukari Kilombero na kuwahamishia kwingine waliokuwapo. Tukawahamisha pia Mkuu wa Mkoa na kumpeleka Kigoma na Kamanda wa Polisi wa Mkoa akarejeshwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
 

ngome1838

JF-Expert Member
Feb 20, 2019
655
1,000
Viwanda vingi hasa kwa "day workers"wamekuwa kama manamba hata baada ya karne kazaa baada ya Mapinduzi ya viwanda ya ulaya, huku Afrika hali ni mbaya zaidi. Vibarua wa kwenye mashamba makubwa na viwamdani Wana hali mbaya. Wanaishi kwa matumaini na kudra za Allah S.W
 

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
2,446
2,000
Utawala ulilega na kufanya mambo ya hovyo kulikabili tatizo hilo, ilipaswa waliohusika kuteketeza roho za watu bila hatia wakafie jela na sio kubadilishwa vituo vya kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom