Mwingine BAVICHA ajiunga na CCM

Mwingine BAVICHA ajiunga na CCM

hana jipya huyo/ ahadi gani aliahidiwa ? au aliahidiwa kupanda cheo

Msipate shida na hao. Ameshukiwa na "Roho mtaka mbivu" hivyo kawafuata wenzake sisiem wakanene kwa lugha.
 
Tunamkaribisha CCM kwa mikono miwili. CCM ni chama kisichokuwa na ubabaishaji kwa sababu ya kuwa na mgawanyo wa madaraka na utawala wa sheria. Ndani ya CCM kila mtu ana nafasi sawa ya kusikilizwa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina mmiliki wake. CHADEMA kina mmiliki wake.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Kigumu
 
Ish!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! wapi kumekucha sasa CDM au CCM. Nyie ndo huko CCM kumekucha video mtoe nyie roho mtoane nyie.(Membe Vs Lowasa)

ndio mnavodanganyana? Lwaka mkurugenzi wa utekaji na utesaji anaendelea kujisaidia kwenye ndoo..
 
Kumbe huyu jamaa alikuwa pale kwa manufaa yaake na sio kwa ajili ya kutumikia wananchi lol so basi imekuwa poa kabisa kwenda kwa wenzake wanaofuatilia maslahi yao binafsi CCM.Kaka kwa heri kaungane na wenzako mle nchi kifisadi hapo ndio kwako na sio Chadema ni bora umesema mwenyewe kuwa uliahidiwa ahadi ambazo hazitekelezeki kwani ulifikiria utapewa Ubunge wa kuteuliwa au viti maalum kaka kwa heri.Chadema ahadi zao ni kutumikia wananchi na sio vingine kama ulivyofikiria Gamba mkubwa wewe na bado mko wengi kama wewe njaa kubwa.Bora mtoke mapema kukiwa kweupe
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli daima Vijana wengi wanaoingia kwenye siasa Tanzania ya leo wanaweka mbele maslahi binafsi na si masilahi ya Taifa la Tanzania,vijana wengi walioko ccm na vyama vingine wanawaza na kuthamini maslahi yao kwanza nchi baadae.Nchi haiwezi kwenda namna hii.vijana tujirekebishe itafikia hatua wanainchi wanaotudhamini watatudharau na kututupa.Leo nje ya wigo anaamka anazungumza jambo kwa kulipinga kweli kweli kesho akiwa ndani ya wigo wa kula hilohilo analikubali tena kwa mbwembwe kubwa liendelee eti kwa sababu naye leo ni sehemu ya ulaji jamani tuache unafiki.daima tuweke mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi ya matumbo yetu.huu usaka tonge vijana unatuharibu.imefika pahala vijana leo hawajulikani wanasimamia nini awe ccm,cdm au cuf,tafadhali wajameni fijana tubadilikage nye vaa.
 
Vijana wachovu wanaangalia matumbo yao tu.
 
Back
Top Bottom