John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Julia Petta alifariki mwaka 1921, baada ya hapo alizikwa kwenye Makaburi ya Mount Carmel yaliyopo Chicago nchini Marekani.
Alizikwa akiwa na gauni lake la harusi, inadaiwa kuwa mara baada ya msiba huo, mama wa marehemu, Filomena alianza kuota ndoto akiona Petta anamwambia kuwa yeye (Petta) bado yupo hai.
Inaelezwa kuwa ndoto hizo ziliendelea hadi miaka mitano tangu Petta alipozikwa.
Miaka sita tangu msiba, familia yake ikiwa imeshahama Chicago na kuishi Los Angeles, Filomena akaamua kurejea Chicago na kuomba ruhusa ya kufukua kaburi la mwanaye.
Baada ya kufungua wakakuta jeneza bado zima japo kuna sehemu lilikuwa limeshaanza kuoza, walipolifungua wakakuta mwili wa Petta upo vilevile, mama mtu akapiga picha mwili huo kisha wakafunika na kurejesha udongo.
Picha hiyo ikaweka kwenye maeneo ya makumbusho na ipo hadi leo hii.
Tangu alipoona mwili wa mwanaye kwa mara nyingine, akaamua kubaki Chicago hadi naye alipofariki mwaka 1945.