Mwikwabe anashauri waziri Masha achunguzwe kuhusu EPA na Deep Green | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwikwabe anashauri waziri Masha achunguzwe kuhusu EPA na Deep Green

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Dec 20, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Na Ashauri Waziri Masha achunguzwe EPA

  Kada machachari wa CCM aliyehamia Chadema hivi karibuni, Mwita Mwikabe, amevishauri vyombo vya dola kuanza kumchunguza Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha endapo alihusika na wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  Amesema kwa kuwa Masha alikuwa mmoja wa Wakurugenzi kwenye kampuni ya Deep Green iliyochota Sh. bilioni 10 kwenye akaunti ya EPA, lazima ahojiwe na ikibainika alihusika afikishwe mahakamani kuungana na wenzake 20.

  Akizungumza na Nipashe jana, Mwikabe alisema Masha ameanza kutoa vitisho vya wanaoandika habari za ufisadi.

  ``Kabla ya kuanza kutishia watu wanaopiga vita ufisadi, lazima tujue uhusuika wake Deep Green, kampuni iliyoko kwenye kundi la mafisadi...Masha anaanza kujihami ili mambo yake yasianikwe kwa kutishia watu,`` alisema Mwikabe ambaye hivi karibuni alikuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga.

  Aidha, alisema watu wote waliohusika katika wizi wa fedha za umma, wamekuwa maadui wakubwa wa vyombo vya habari kutokana na kufichua uovu wao.

  Wakati huo huo, Mwikabe alimshangaa Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba kwa kudai kuwa mjadala wa EPA umefungwa.

  Alisema Makamba hastahili kutoa kauli kama hiyo kwani chama chake ndicho kinatuhumiwa kwa makosa yaliyotokea na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni.

  Alisema mtuhumiwa hawezi kuwa hakimu kwenye kesi yake mwenyewe.

  ``Walengwa kama Kagoda Agriculture Ltd hawajakamatwa halafu unasema mjadala umefungwa? yeye ni nani mpaka afunge mjadala,`` alisema Mwikabe.

  Hivi karibuni, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, amemtuhumu Waziri mmoja wa Serikali ya Awamu ya nne kuwa ameagiza abambikiwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa ili hatimaye afilisiwe.

  Alisema Waziri huyo ameahidi kunyamanzisha kabisa kutokana na kupigia kelele ufisadi.

  Mengi alisema Waziri huyo amekuwa akijigamba kuwa atanyamanzisha kwa kuhakikisha anafilisiwa kama alivyofilisiwa tajiri mmoja huko Urusi.

  Mengi alisema Waziri huyo anadai kuwa vyombo vyake vya habari vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri na linawanyanyasa baadhi ya watu.

  ``Nilitarajia Waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanyakazi...anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na si mmiliki,``.alisema.

  Alisema ingawa tayari amemsamehe Waziri huyo lakini anapaswa kujua kuwa asiyekemea maovu katika jamii anakuwa sehemu ya maovu hayo.

  Alisema Waziri huyo na wale ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa vitisho lazima wakumbuke kuwa hata wakifanikiwa kunyamanzisha yeye (Mengi), moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za watanzania hauwezi kuzimika kamwe.
  SOURCE: Nipashe
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mwikwabe wewe sema maana unaijua siri ya CCM ulikuwa ndani kabisa kwenye chungu .Tueleze nasi tutakaa nyuma yako kukulinda ama njoo hapa JF mwaga sie tutasambaza.
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndugu Mwikwabe,
  Kwanza nakupa pongezi kwa kujitoa kutoka CCM. Umeonesha ni jinsi gani unaipenda nchi yako kwani CCM iko pale kuimaliza nchi na wala si kuilinda na kuijenga nchi.
  Tutakuhitaji sana hapa JF katika kujua undani wa CCM na serikali yake chafu ili tuweze kuibamiza toka kila upande. KARIBU SANA
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Inaonekana huyu Mwikabe ni kichwa huyu, maana hachanganyi maneno na kurusha hukumu bila facts.
   
 5. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ha, ha, ha, Mwita Mwikwabe.

  Siamini kama huyu jamaa anamaanisha kwa kuyasema haya kwa Bosi wake na ndio maana natilia mashaka hata kuhamia kwake CHADEMA naona kama ni mtu aliyetumwa kuja kuiboma CHADEMA.

  Ila acha yangu yawe macho tuone.
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwita kasema vyema sana .

  Hii ndio huyu aliyekataa kuwa mfagizi ktk ofisi ya Nchimbi ?Walimfanyia fitna kutoa ofisi ya Tanga kuja kuwa secretary wa Nchimbi akagoma akidai yeye graduate hawezi kufanya kazi hiyo.
  Wanaomjua naomba wanihakikishe kama ndio huyu maana huyu jamaa kama ndio yeye namjua akiwa sekondary pale Azania na nafikiri alishakuwa rais wa wanafunzi UDSM.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mutu he is the man .The very guy unaye muongelea.Wanao toa wasi wasi kwamba kaenda kwa kutumwa lazima waangalie pia mazungira ya yeye kutoka CCM.Hawezi kutoka wakati muhimu sana kama ule kwa CCM kisa katumwa .Waacheni wenye kujaribu kuikoa Tanzania wajaribu na wengine chongeni kwenye forum kuonyesha uchungu ambao hamnao .Mazingira ya kufanya siasa Tanzania nakuishi hapa ni magumu sana .Usione urahisi wa kuchonga hapa na unalala kwenye majumba ya wazungu huko Ulaya na US .Waacheni watu wenye nia ya dhati .
   
 8. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Natusubiri tuone.Namfahamu Mwikwabe ila kwakuwa mtu sio jiwe...kuna kubadilika...lets wait and see
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Baba J una maana kwamba Mwikwabe ni kanjanja na opportunisty na atawaacha Chadema hoi ? Sasa who os to be trusted kwamba ni pure opposition maana kila mmoja lazima utasikia huyu katumwa mara analipwa na CCM nk .
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wakuu tusiwe naive na wanasiasa, wote huwa ni ma-opportunists lakini give this kid a credit kwa sababu ni moja ya sababu kubwa ya kushindwa kwa CCM Tarime, sasa kama kweli CCM walimtuma ili aisadie Chadema kuwashinda Tarime, then kuna something hatujui kuhusu CCM.

  - Binafsi I respect this kid kwa sababu ya kutoka at the right time na siku zote huongea the right words, na siamini kwamba Chadema walimnunua kama ambavyo huwa tunaambiwa hapa kiongozi wa upinzani anapohamia CCM huwa wamenunuliwa tu na njaa inawasumbua, siamini kuwa that is the case na this kid.

  Wanasiasa wote huwa ni ma-oppurtunists.
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mara zote ambazo nimekaa na Mwikwabe kuanzia Kampeni kule Tarime , Mikutano Musoma , Kuapishwa Mbunge wao watu wa Tarime pale Dodoma nimetumia muda sana kumsoma ili kujua jambo lakini the boy ni makini tuache utani .Kama ni mapungufu wote tunayo lakini kwa national issues tumpe nafasi akiboronga pia hatutacha kusema .
   
 12. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2016
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Siasa za siasa...
   
 13. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2016
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa Masha ni kamanda na kashafutiwa dhambi ya ufisadi pamoja na Lowassa.
   
 14. M

  Mwanachama Sahihi JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2016
  Joined: Apr 3, 2015
  Messages: 523
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Baada ya miaka saba una la kuongeza mkuu?
   
Loading...