Mwigulu sasa kufanywa ajenda kuu CHADEMA

Mwigulu sasa kufanywa ajenda kuu CHADEMA

Wewe ni nani ndani ya chadema?

Kwani kakwambia yuko ndani ya CHADEMA!?? huyo ní mtanzania kama watanzania wengind wengi wasiopenda upuuzi kama huu wako.. you poor thing..
 
WanaJF!

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kina tazamiwa kuwa na ajenda ambazo ni mbadala wa zile za chama tawala ambazo zingeweza kufanya mabadiliko ya hali ukilinganisha na hali ilivyo sasa, badala yake chama hichi kimekuwa 'vuvuzela' kwa kulitaja jina Mwigulu kwenye vikao vyake na mikutano ya chama.

Katika hali hiyo ya CHADEMA kujadili jina la mtu (Mwigulu) na kulifanya jina hilo kuziteka ajenda nyingine za chama ambazo wenda zingekuwa na umuhmu kwa mustakabali wa taifa, ina dhihirisha chama hichi kufirisika kisiasa na kimawazo na hata hadhi yake ya kuwa chama kikuu cha upinzani imezorota.

Aidha, juzi kwenye mkutano aliofanya Dr Slaa hapa Iramba na ule aliofanya Tanga, karibu 90% ya ajenda zake zilikuwa zimemlenga mhe Mwigulu, badala ya kuongelea mambo yanayohusu katiba mpya kama ambavyo imekusudiwa, hii ni hatari sana katika siasa za ushindani.

Lakini vilevile hata ukitazama mijadala mbalimbali ya makamanda wa CHADEMA ambayo ilikuwa na lengo la kujadili mambo yanayohusu utaifa na mambo mengine ya aina hiyo, badala ya kujikita kwenye mada iliyo mbele yao, wao wanaishia kumtaja Mwigulu, sasa wananchi wa kawaida tuwaeleweje CHADEMA?

Siku zote watu makini huwa hawana muda wa kujadili wanaume wenzao kama wewe unavyoatack person badala ya kujadili issues,siku zote ww ni Slaa,Mbowe na Cdm ndio issue zako za kujadili wakati kuna issues kibao za kujadili unless otherwise unampenda Slaa

Kwa watu wenye akili pia Mwigulu hawezi kuwa agenda ya kujadili,umjadili kwa lipi? Ugaidi au kwa lipi la maana? Huyo ni role model wenu kwa ugaidi,ujambazi,kumwagia watu tindikali kama Ponda kwa hilo atakuwa agenda vinginevyo si malikitu kabisa sawa we
 
Well, CHADEMA is not like your dearest party, why can't you join Nape's department because always you bring stories of CHADEMA Dr. Slaa only. Why can't you tell us about Drug trafficking, Corruption scandals, mismanagement of our natural resources, the Mtwara situation than focussing on CHADEMA. As far as I understand it is CCM' role to mention CHADEMA through out, and the civic education they CHADEMA are providing is done to the open and not indoors.

We do enjoy reading your substandard observations and comments, but all the same it is your constitutional rights to say whatever you feel like,

WOW!!!!

Hichi Kiswahili kilichoandikwa kwa Kiengereza kinafurahisha kidogo! Majuzi nilikuwa napita Moshi nikawa nasikiliza Kili FM wakijadili "Why Tanzanians like to buy quantity and not quality". Caller mmoja alimaliza mazungumzo kwa kusema "thank you" na mtangazaji akamjibu "thank you too". Haya ndiyo yale ya mtu anaku-wish "happy birthday" unaishia kujibu "happy birthday too"! Nataka kuuliza hivi kuna ubaya gani bandiko lililoandikwa kwa lugha ya Kiswahili likajibiwa kwa Kiswahili?
 
Hamy-D Unaota ndoto ya mchana. Chadema in a agenda za kutosha za kuwakomboa Watanzania. Ndo maana Kama uko makini, katika mkutano wa Baraza la Kitaasisi la Chadema kilichofanyika Igunga hatukuwa na muda wa kupoteza na jina la Mwigulu. Kumbuka Watanzania WANs kero nyingi, Mwigulu can no longer be an agenda, kashindwa kusimamia Jimbo lake Lina kero kibao, wananchi wake walimwaga hadharani. Pamoja na aibu ya kupeleka Timu ya Simba, alivuna alichopata, Mkutano wa Chadema ulidunda Kama ulivyopangwa.

Dr pole sana, kwanza Mwigulu sio mbunge wa Igunga. Huko igunga aliongoza kampen tu. Ndio uzee nini babu? Mwigulu ni mbungr wa Iramba. Pili utakuwa umedanganywa na umejidanganya mwenyewe ukidhani mwigulu hakupata watu. Ukweli ni kwamba watu ulikuwa nao hawakuwa hata Robo ya watu waliokuwa uwanjani na Mwigulu. Mwigulu alipokelewa kifalme sana. Kama ilikuwa mbinu basi mwigulu alifanikiwa over 100% maana wewe ulihutubia viongoz wako tu. Wanakudanganya kama wanakwambia mwigulu aliambulia aibu
 
Habari Dr., samahani mimi sio mbunge wa Igunga na mkutano wako haukufanyikia Igunga bali ni IRAMBA, UMEJIBU HARAKA AU NDIO UMRI TENA? MIMI SIKUILETA SIMBA KWA AJILI YA MKUTANO WAKO, NI mwendelezo wa program yangu kwenye upande wa michezo. Mwaka juzi niliileta Toto Africa, mwaka jana niliileta Mtibwa Sugar. Mpira na siasa ni vitu viwili tofauti. Mkutano wako hauna madhara kwangu cos Iramba ni nyumbani kwangu. Kama unadhani wewe una madhara kwangu Iramba hamishia makao makuu ya chadema kiomboi hapa iramba na zunguka mtaa kwa mtaa halafu tugombee wote Iramba hapo hapo. Ukipata hata nusu tu ya kura zangu dr slaa mimi naandika barua kule tume wakutangaze uwe mbunge wa Iramba. I repeat again and again dr, you are neither my competitor nor my threat in politics. Am 38 yrs old and you are around 70. You are automatically phasing out of politics while am just starting ( other things remain constant) where were you at 38th my age? Where will I be 10 yrs from now? And you? You are comparing your politics by chance and my politics by tallent.
 
Well said. Huyu babu anadanganywa na watu wake na gazeti lake la tanzania daima. Siku hiyo iramba yote ilikuwa mpiran. Alihutubia viongozi wake. Mpk sasa gumzo iramba ni kuhusu simba. Watu wanasema slaa hawezi rudi iramba kwa aibu aliyoipata. Slaa anajiona mwigulu hakufanikiwa, hivi slaa unakwenda kinyumenyume?
 
Huyu Mwigulu asiwape tabu, ndivyo alivyo. Pale Mazengo miaka ya 2000 alikuwa form 6 na akawa akitembea hupungia watu vidole vitatu akimaanisha atapata div 1 ya point 3. Matokeo yake alipata div 3 ya mwisho...na kuwaacha vichwa kama akina Fighton wakipiga div 1 za nguvu... Pamoja na kukariri Mzumbe Project lote haikusaidia...aje hapa abishe...halafu mh. Mwigulu una miaka 34 ama 38? Ama yule mwigulu orijino ndo ana 34 na wewe successor ukiwa na 38 ama ni typo tu mkuu???
 
Dr pole sana, kwanza Mwigulu sio mbunge wa Igunga. Huko igunga aliongoza kampen tu. Ndio uzee nini babu? Mwigulu ni mbungr wa Iramba. Pili utakuwa umedanganywa na umejidanganya mwenyewe ukidhani mwigulu hakupata watu. Ukweli ni kwamba watu ulikuwa nao hawakuwa hata Robo ya watu waliokuwa uwanjani na Mwigulu. Mwigulu alipokelewa kifalme sana. Kama ilikuwa mbinu basi mwigulu alifanikiwa over 100% maana wewe ulihutubia viongoz wako tu. Wanakudanganya kama wanakwambia mwigulu aliambulia aibu

Nyumba ndogo ya Mwigulu Nchemba naona upo hapo au wewe ndio wale green guard aliowatuma kumwagia Tesha tindikali? Gaidi lililogundua matumizi ya kumwagiana Tindikali Tanzania na kulipuana mabomu
 
Habari Dr., samahani mimi sio mbunge wa Igunga na mkutano wako haukufanyikia Igunga bali ni IRAMBA, UMEJIBU HARAKA AU NDIO UMRI TENA? MIMI SIKUILETA SIMBA KWA AJILI YA MKUTANO WAKO, NI mwendelezo wa program yangu kwenye upande wa michezo. Mwaka juzi niliileta Toto Africa, mwaka jana niliileta Mtibwa Sugar. Mpira na siasa ni vitu viwili tofauti. Mkutano wako hauna madhara kwangu cos Iramba ni nyumbani kwangu. Kama unadhani wewe una madhara kwangu Iramba hamishia makao makuu ya chadema kiomboi hapa iramba na zunguka mtaa kwa mtaa halafu tugombee wote Iramba hapo hapo. Ukipata hata nusu tu ya kura zangu dr slaa mimi naandika barua kule tume wakutangaze uwe mbunge wa Iramba. I repeat again and again dr, you are neither my competitor nor my threat in politics. Am 38 yrs old and you are around 70. You are automatically phasing out of politics while am just starting ( other things remain constant) where were you at 38th my age? Where will I be 10 yrs from now? And you? You are comparing your politics by chance and my politics by tallent.

Mwigulu
Lazima ukiri kwamba ulikurupuka au wakati unaamua kuileta Simba haukutumia akili zilizokupa huo uchumi first class,kwa sababu zifuatazo
-Katiba sio suala la Cdm,ccm,Slaa wala Mwigulu ni suala la Watanzania wote,kitendo cha wewe kugonganisha mechi na mkutano kwa kisingizio kwamba Iramba ni nyumbani kwako,ni akili ndogo ambazo hazifai hayo maelezo kutolewa na mchumi anayejidai ni first class,umeonyesha bado akili zako sio timamu,kwani umewakosesha nafasi wanairamba kuchangia mawazo yao katika kuandika katiba,kwa kutumia ushamba wao kuja kuishangaa Simba badala ya kutoa maoni yao,yatatolewa maamuzi na waliojitokeza kwa upuuzi wako na wao watadai wao hawakuchangia kuundwa kwa katiba hiyo,sababu kwa kutokujua kwako au kwa makusudi kwa kutumia ujinga wao uliwadivert kutoka kwenye mambo ya maana na kuwadirect kwenye upuuzi wa dakika 90 utawacost maisha yao yote wengine,watakulaani Mwigulu sio ujanja ulioufanya kwamba unamkomoa Dr Slaa bali ni uliwakosesha nafasi wao kutoa mawazo yao kwa siasa zako za kitoto

Halafu unaqeka post na picha humu jf ambapo wengine hawajafikia elimu yako hiyo lakini wamekuona bonge la nguruwe kwa ulichokifanya,eti SONGELA SAANA kwa kiongozi kama wewe kupost upuuzi ni upuuzi wa kutisha

Elewa katiba ni ya Watanzania sio ya Cdm wala ccm watanzania wasichaguliwe cha kuongea kwa kuwachagulia vibaraza vya katiba vya watu wa ccm kuteka mjadala wa katiba kuweka watu wao kwa kutumia wingi wao ili wapitishe mapendekezo ya ccm ili waendelee kutawala,mjadala wa wazi kama wa Chadema ndio wa wananchi wote,sasa wewe unawazuia watu wa nyumbani kwako ulivyowaita unawarishisha akili mbovu ulizonazo

Hebu jiheshimu acha kupost thread zinazokuaibisha na kuonyesha upeo wako wa kufikiria unapofikia,THINK BIG MAN unaongoza zaidi ya wanaccm milioni4
 
Babu piga hela msimu wa mavuno ndio huu teketeza hela za ruzuku na za wahisani wenu. Usirudi nyuma umri unakupita huu Babu sasa una miaka 79 na toto la kihaya ndio mbichi saka noti babu.

Kwa kweli babu hadi mchakato huu wa katiba ukipita sio Haba utakuwa umetunisha acc yako kwa kiasi kikubwa. Si unajua mtoto mdogo anahitaji misingi thabiti ya kumfanya akue vyema. Siasa inalipa si umeona ni tofauti sana na kusubiri matoleo ya kila jumapili Huku kwenye siasa siku zote jumapili.
 
Dr pole sana, kwanza Mwigulu sio mbunge wa Igunga. Huko igunga aliongoza kampen tu. Ndio uzee nini babu? Mwigulu ni mbungr wa Iramba. Pili utakuwa umedanganywa na umejidanganya mwenyewe ukidhani mwigulu hakupata watu. Ukweli ni kwamba watu ulikuwa nao hawakuwa hata Robo ya watu waliokuwa uwanjani na Mwigulu. Mwigulu alipokelewa kifalme sana. Kama ilikuwa mbinu basi mwigulu alifanikiwa over 100% maana wewe ulihutubia viongoz wako tu. Wanakudanganya kama wanakwambia mwigulu aliambulia aibu
Babu siku hizi umezeeka kweli yaani unashindwa kutofautisha Igunga na Iramba? Pole sana nguvu unayo lakini akili ishachoka sana na upo around 70 sasa. Babu CDM sio mwisho wa maisha sasa inabidi upumzike umlee huyo mtoto wako mdogo.

Mwigulu hamuwezi yeye ni kijana na ni msomi Mzuri wee umri haupo nawe tena na kwa hakika umeshaanza kukopa umri kwa mujibu ya biblia.
 
Imenibidi nichangie huu uzi kutokana na majibu yaliotolewa na wanajamvi wengine wenye akili achilia mbali kichwa wazi anayejiita hamy D. Mimi niliamua kutosoma kabisa post za amy D kwa sababu kila akija humu jamvini yeye na dr Slaa tuu kila siku na kujadili personalities badala ya issues tene critical zinazowahusu watanzania wasikini wa kutupwa kwenye nchi yao tajiri
 
Nyumba ndogo ya Mwigulu Nchemba naona upo hapo au wewe ndio wale green guard aliowatuma kumwagia Tesha tindikali? Gaidi lililogundua matumizi ya kumwagiana Tindikali Tanzania na kulipuana mabomu

Tukana tu lakini tushindane kwa hoja ndio uungwana nyie vijana wa mtaa wa ufipa mbona jazba kila jambo? Ukizidiwa kwa hoja unajenga hoja juu ya hoja. Kama matusi tunaweza sana lakini kuna usemi usemao ukigombana na mjinga utakuwa mjinga pia.

Jifunze kuwa mstaaarabu bwana mdogo au muda wako wa kwenda shule ndio umefika? Soma dogo achana na siasa hizi hazitakusaidia na kukujenga katika umri mdogo Kama huu
 
Imenibidi nichangie huu uzi kutokana na majibu yaliotolewa na wanajamvi wengine wenye akili achilia mbali kichwa wazi anayejiita hamy D. Mimi niliamua kutosoma kabisa post za amy D kwa sababu kila akija humu jamvini yeye na dr Slaa tuu kila siku na kujadili personalities badala ya issues tene critical zinazowahusu watanzania wasikini wa kutupwa kwenye nchi yao tajiri

Wee unafikiri humu JF kuna mtu mwenye hoja nzito zenye ukweli na weledi zaidi na HAMY-D? Usiposoma sie twasoma yaani ukisusa sie twala
 
ZeMarcopolo,
Ni maskini wa moyo na roho ndo daima wanaofikiria "posho". Wenzako wanawaza mbinu ya kukomboa Taifa wewe unawaza posho! Ndo maana watanzania wamewapuuza! Zungumza kwenye mtandao, nenda hadharani uone Kama utakuwa na ujasiri wa kutamka hayo mbele ya watanzania waliopigika kwa miaka hamsini. Saa hizi chadema inapeleka elimu muhimu mpaka kijijini, na hii ndiyo itakayoing'oa CCM. Endelea na Ngonjera yako utaitazama nchi inayoyoma, kana kukusanya Buku zako sasa, vinginevyo utasaga meno!

Acha kuwalaghai wenzako wapuuzie posho wakati wewe akaunti innona tu. Ungekuwa hujali posho usingeweka masharti ya kulipwa mshahara wa kibunge kwa kuzurura na wala usingeidhinisha Josephine alipwe mamilioni ya Chadema kwa kazi za kimagumashi.

Age mates wako kina Kingunge na Mzee Samwel Malecela sasa hivi wanakula pensheni zao halali.
 
[h=3]Nchemba, hata shetani hutajwa mara nyingi[/h]
​
Na Prudence Karugendo

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba, kaandika kwenye mtandao wa kijamii, kwa njia ya kutamba, akionesha kuwa kutajwatajwa kwake mara nyingi, hasa kwenye vyombo vya habari, kunadhihirisha mafanikio yake aliyoyapata mpaka sasa katika umri wake mdogo alio nao.

Mwigulu anazidi kutamba, huku akijilinganisha na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kwamba katika umri wake wa miaka 34 anatajwatajwa kiasi hicho, je, akija kufikia umri kama alio nao Dk. Slaa kwa sasa hali itakuwaje?

Kwa upande wangu, katika watu ambao nilikuwa najizuia kujadili mienendo yao ni pamoja na Mwigulu Nchemba. Sikutaka kujadili mwenendo wa Nchemba kwa vile unaonekana kuwa na utata mwingi ambao kuujadili pengine inabidi mtu apate kilevi kwanza.

Niwe muwazi, nimuonavyo mimi, Nchemba ni mtu ambaye hafai uongozi wa aina yoyote katika jamii, lakini ajabu wengine wanaona kinyume chake! Mtu ninayemuo hafai wengine wakamchagua awe mbunge wao. Mtu huyohuyo akapata nyadhifa mbalimbali katika chama chake, chama tawala, huku mwenyekiti wa chama hicho kitaifa akimuona anafaa zaidi kiasi cha kumpandisha chati kwa kumteua awe Naibu Katibu Mkuu!

Hayo ndiyo mambo yanayoifanya Tanzania ionekane nchi ya ajabu, nchi ambayo mtu anaweza kufanya ovu lolote na bado akashangiliwa na walewale aliowafanyia uovu. Tanzania ya maajabu.

Huko tupaache, inawezekana anapafaa kulingana na halihalisi ilivyo kwa upande wao. Maana Waswahili wanasema kwamba kila shetani na mbuyu wake. Cha kuangalia ni vituko na majigambo ya kijana huyo kada wa CCM ndani ya jamii yetu.

Kijamii, Mwigulu anaonekana kutumia nafasi aliyo nayo kuigawa jamii yetu katika makundi hasimu kwa kisingizio cha itikadi za kisiasa na kisha kuchochea uhasama kati ya kundi moja na lingine kusudi makundi hayo yachukiane. Jambo hilo analifanya bila kujali kwamba anahatarisha mustakabali wa nchi yetu ambayo yeye ni kiongozi.
​

Kauli na matendo yake ambavyo amekwishavionesha, kuanzia Bungeni mpaka kwenye mikutano ya hadhara, hususan kwenye kampeni mbalimbali za kuwashawishi wananchi wakichague chama chake dhidi ya vyama vya upinzani, ni ushahidi tosha wa haya ninayoyasema hapa.

Mfano, Nchemba katengeneza kitu anachokiita ugaidi na kukivisha kwa wengine hasa anaowachukulia kama mahasimu wake kimaslahi. Katika mojawapowapo ya vituko vyake, kaapa kuanzia Bungeni kuwa anao ushahidi wa duniani na mbinguni juu ya ugaidi wa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare. Lakini mpaka Lwakatare anafutiwa mashitaka hayo ya kuchonga ya ugaidi na Mahakama Kuu hatukuuona wala kuusikia ushahidi wa Mwigulu.Wengine tukajiridhisha kuwa pengine ushahidi huo umekwamia kwenye masjala ya mbinguni alikokusema.Sasa kilichobaki kikijionesha wazi ni vita kati ya mahakama na uzushi wa Nchemba. Mahakama inaonekana kuukomalia uzushi wa Nchemba, ambapo tunajionea jinsi mahakama inavyoyatupilia mbali kila madai ya ugaidi yanayopelekwa kwake ikidaiwa kuna ushahidi uliohifadhiwa mbinguni ila mahakama inapouhitaji hauletwi.

Vihoja vingine vya Nchemba ni kama vile vya kuvaa bendera ya taifa shingoni karibu kila wakati, au kuvaa mavazi yaliyo katika mfumo wa mavazi ya kijeshi. Haieleweki kama hiyo ndiyo inayomaanisha au kuonyesha uzalendo uliotukuka. Kwamba yeye ni mzalendo kuliko wengine wote kwa kuvaa bendera ya taifa shingoni. Au kwamba yeye ni mtu anayefanya mambo kijeshi kwa kuvaa mavazi yaliyo katika mfumo wa mavazi ya makamanda wa jeshi.

Hivi hayo ndiyo mafanikio ya Nchemba anayodai yanamfanya atajwetajwe sana na kutamba kuwa kamwe hakuna atakayetokea na kuyasimamisha? Mafanikio yaliyopatikana katika umri mdogo!

Ningetaka kumkumbusha Nchemba kwa kutumia tu uzoefu wa maisha. Kama kusemwasemwa sana katika umri mdogo ndicho kinachomfanya mtu ang’are basi Samwel Doe wa Liberia aliyeupata urais katika umri wa miaka 25 angeng’ara zaidi ya Nelson Mandela aliyeupata urais katika umri wa miaka 76. Lakini je, ndivyo halihalisi ilivyo? Kuna uwezekano wowote wa kumlinganisha Samwel Doe na Mandela katika mafanikio ya kisiasa?

Sasa kwa kulizingatia hilo inawezekanaje Nchemba ajilinganishe kwa Dk. Slaa kisa kaanza kusemwasemwa katika siasa kwa umri mdogo wakati Slaa kaingia kwenye siasa ukubwani? Hapo najaribu kutegua kitendawili cha Nchemba kwamba katika umri wa miaka 34 anasemwa hivi, je, katika umri kama alio nao Slaa itakuwaje.

Naweza kubashiri kwamba si ajabu katika kufikia umri kama alio nao Dk. Slaa, Nchemba akawa hajulikani tena kwenye siasa za nchi yetu kutokana na usemi wa kwamba ivumayo haidumu. Maana maisha yana kanuni zake ambazo si rahisi kuzibadilisha, ndiyo maana wahenga wakapata semi mbalimbali za uhakika zinazotabiri maisha kulingana na matukio yaliyopo.

Wahenga walikuwa na hekima nyingi, walisema chema chajiuza kibaya chajitembeza. Ni kweli kabisa. Ni nadra sana chema kusemwa mara kwa mara. Ila kiovu husemwa sana mara kwa mara. Nahisi kusemwa sana kwa kilicho kiovu ni katika kukumbushana namna ya kukiepuka. Chema hakina tatizo lolote.

Shetani ni muovu, swali la kujiuliza ni yupi kati yake na malaika aliye mwema anayetajwa zaidi? Kwa walio waamini kwa uwepo wa Mungu watakuwa wanaelewa kwamba ibada inaweza kuendeshwa mpaka ikaisha bila kutaja neno malaika, lakini ibada haiwezi kuendeshwa mpaka kumalizika bila kumtaja shetani. Hivi kweli shetani anaweza kuvimba kichwa na kumtambia malaika kutokana na kutajwa kwake sana hata ndani ya nyumba za ibada?

Tumeshuhudia kauli mbalimbali za hatari zinazotolewa na kada huyo wa CCM akiwa hajari zinaweza zikaiathiri kiasi gani jamii yetu. Tukiacha zile za kuwabambikia wenzake sifa mbaya ya ugaidi, tumesikia kama zile za kwamba mkiwachagua Chadema mtakufa. Kauli hiyo imetolewa katika kampeni za udiwani, Arusha. Na kweli muda mfupi baada ya kauli hiyo kukatokea vifo katika mkutano wa Chadema. Na mpaka sasa mtu huyo hajachukuliwa hatua yoyote, walau kuulizwa tu kwamba kauli yake hiyo ilikuwa na maana gani.

Zipo kauli nyingi za hatari zilizotolewa na Nchemba huku wakubwa wake wakimuangalia tu na kufurahia wakidhani anawakomoa wapinzani, hivyo wakamuachia tu bila kumkemea. Lakini inabidi ieleweke kuwa mtoto mtukutu anayechezea moto ndani ya chumba kilichohifadhi petroli ni wa kukanya kwa ukali bila kuangalia kama anacheza na ndugu wa kambo, maana lolote la kutokea linaweza kuwaangamiza watoto wote pasipo kujali ni nani asiyekuwa mtoto wa kambo.

Mtu wa aina hiyo atatoweka vipi vinywani mwa watu? Na anaposemwa ni kweli anasemwa kutokana na mafanikio yake aliyoyapata katika umri wake mdogo? Kama kweli hayo ni mafanikio yanayopaswa kutambiwa basi shetani ana kila sababu ya kumtambia malaika maana anasemwa sana zaidi yake.

prudencekarugendo@yahoo.com
0784 989 51
BUKOBA WADAU BLOG
 
Back
Top Bottom