Mwigulu Nchemba: TRA inatimiza wajibu wake vizuri, wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi ipasavyo!

Waziri wa katiba na sheria Dr Mwigullu Nchemba amewajibu wabunge wa CCM wanaoilalamikia TRA kwamba taasisi hiyo inatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Mwigullu Nchemba amesema katika serikali iliyopita wakati akiwa Naibu waziri wa fedha uchumi wetu uliendeshwa kwa kodi za watumishi wa umma kwani wafanyabiashara hasa wakubwa walikuwa hawalipi kodi kabisa. Wafanyabiashara walikuwa wanakimbilia bodi ya rufani za kodi kujificha lakini awamu hii mambo ya konakona hayapo tena, amesema Mwigullu.

Ikumbukwe kuwa wabunge wa CCM wakiongozwa na Nape Nnauye na Joseph Musukuma walidai kuwa TRA inawaonea wafanyabiashara kwa kutumia task force badala ya wataalamu wa kodi.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
Sasa naelewa maneno ya biblia KWANINI watu waliwachukia watoza ushuru na KWANINI walikuwa wakwasi Sana kumbe Ni GENETIC.
 
Huyu mzee ni boya sana kama walikuwa hawalipi mbona JK alikuwa anaajiri kila mara, kupandisha mishahara, kusomesha watumishi, fidia kwa majanga mbalimbali, ujenzi wa miundo mbinu, kununua mazao ya wakulima n.k? hawa ndiyo wanamdanganya dikteta kuwa anafanya vizuri kumbe anaua biashara za watu matokeo yake sisi sekta binafsi hatuna pakupumulia.
 
Ni kweli wanafanya Kazi nzuri Sana ya kuuwa biashara na kuwafanya waishi kishetani
 
Makodi mengi. Mfanyabiashara ana mlundikano wa kodi nyingi. Kiasi kwamba kuna zingine na hali ya kibiashara inakuwa ngumu kuzilipa. Viwango vya kodi, viendane na uharisia wa mtoa kodi. Mtu unafungua biashara umejikopea huko, wanjemba hao.. hawakopeshi
 
Mimi naamini ipo siku moja Watanzania wote kwa kauli moja tutaafikiana kuna mahali tumekosea, TRA indeleeni kufanya munayofanya ila naamini nanyi pia mupo kwenye hii boti.
Hao wanatii maagizo ya mtu mmoja msumbufu.
 
Waziri wa katiba na sheria Dr Mwigullu Nchemba amewajibu wabunge wa CCM wanaoilalamikia TRA kwamba taasisi hiyo inatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Mwigullu Nchemba amesema katika serikali iliyopita wakati akiwa Naibu waziri wa fedha uchumi wetu uliendeshwa kwa kodi za watumishi wa umma kwani wafanyabiashara hasa wakubwa walikuwa hawalipi kodi kabisa. Wafanyabiashara walikuwa wanakimbilia bodi ya rufani za kodi kujificha lakini awamu hii mambo ya konakona hayapo tena, amesema Mwigullu.

Ikumbukwe kuwa wabunge wa CCM wakiongozwa na Nape Nnauye na Joseph Musukuma walidai kuwa TRA inawaonea wafanyabiashara kwa kutumia task force badala ya wataalamu wa kodi.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
Mungu ibariki JF
 
Huyu mwizi ataendelea kuua uchumi.

Watu wanatokea mbali sana!.jpg

Halafu Bashiru anataka apewe vyeo uzeeni ! Thubutu !
 
Back
Top Bottom