Mwigulu Nchemba: TRA inatimiza wajibu wake vizuri, wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi ipasavyo!

Waziri wa katiba na sheria Dr Mwigullu Nchemba amewajibu wabunge wa CCM wanaoilalamikia TRA kwamba taasisi hiyo inatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Mwigullu Nchemba amesema katika serikali iliyopita wakati akiwa Naibu waziri wa fedha uchumi wetu uliendeshwa kwa kodi za watumishi wa umma kwani wafanyabiashara hasa wakubwa walikuwa hawalipi kodi kabisa. Wafanyabiashara walikuwa wanakimbilia bodi ya rufani za kodi kujificha lakini awamu hii mambo ya konakona hayapo tena, amesema Mwigullu.

Ikumbukwe kuwa wabunge wa CCM wakiongozwa na Nape Nnauye na Joseph Musukuma walidai kuwa TRA inawaonea wafanyabiashara kwa kutumia task force badala ya wataalamu wa kodi.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!

Hopefully na Yeye yale Mabasi yake ya Esther anayalipia Kodi vizuri na Kisheria kabisa bila Kukwepa.
 
Back
Top Bottom