Mwigulu Nchemba ni tatizo-Balile

Mwigulu Nchemba ni tatizo-Balile

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mhariri wa gazeti la JAMHURI Deodatus Balile amedai kushangazwa na hatua ya Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba kushambulia vyombo vya habari bungeni kwa madai kuwa vyombo hivyo kazi yake ni kufanya uchochezi.

Akizungumza katika kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star TV asubuhi hii Balile amewapongeza wabunge Peter Serukamba na Jenister Mhagama wa CCM walioungana na wale wa upinzani kulaani mswada wa serikali wa kuzidi kukandamiza wanahabari.

Mwigulu Nchemba akichangia Mswada huo bungeni kwa kutumia lugha kali na ya kuudhi alivishambulia vikali vyombo vyote vya habari na hasa magazeti kwa madai kuwa lengo lao kubwa ni kutaka nchi isitawalike.Pia alilaani Chadema kwa kutoa hotuba ya upinzani iliyokuwa inatetea wanahabari.

Mwigulu alifika mbali kusema kwamba serikali ifanye haraka kuchunguza pasi za kusafiria wale wote wanaopinga mswada huo wa kukandamiza waandishi wa habari.Kwani alidai yeyote anayepinga mswada huo sio mzalendo!

Hata hivyo bunge liliukataa mswada huo kwa kauli moja hali iliyomsononesha sana Mwigulu Nchemba.
 
Mwegulu ni gaidi anajua ipo siku vyombo vya habari vitampeleka ICCriminals
 
Mwigulu inamaana bado hajajua kuwa aina ya siasa zake zimeshindwa, anahitaji kubadilika.?
 
Mwigulu ni janga la Taifa. Nimefuatilia mjadala huu na kuona ni jinsi gani waandishi wa habari walivyokereka na muswada ule uliokataliwa na wabunge wengi pasipo kuangalia itikadi za vyama vyao na kutetea maslahi ya umma zaidi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hivi bado yupo? Naona baada ya Nape kuikataa ile tour yake ya US na UK kuwa hazikuwa za chama bali zake (ingawa alituaaga hapa JF kuwa ametumwa na waTanzania) alinywea kwa muda.
 
msimlaumu mwigulu, sio makosa yake.....
 
Mwigulu inamaana bado hajajua kuwa aina ya siasa zake zimeshindwa, anahitaji kubadilika.?
Hajajaaliwa kiwango hicho cha ung'amuzi. Kwani we unamuonaje?
 
mwigulu ni gaidi ,nami ninaushahidi hapa duniani na mbinguni pia
 
Tatizo la watu kama akina Balile ni wabinafsi sana! Wakati watu karibia wote ukiacha ile Misukule ya buku 7 ya Lumumba, wanamlalamikia huyu gaidi yeye aliziba masikio aliona hayamuhusu, leo hii, gaidi, Taswira kapiga kwenye maslahi yake ndio anajifanya kumfahamu. Nyambaff! Tulia akunyoe mpaka nywele za kikalio.
 
Nimepita mahali wazee wanamjadili Mwigulu. Mzee mmoja tena mwenye hekima akasema huwa akimwona Mwigulu anazungumza kwenye tv anazima tv
 
huyu balile ndiye aliyehusishwa ishu ya kibanda au ni mwingine?
 
Mhariri wa gazeti la JAMHURI Deodatus Balile amedai kushangazwa na hatua ya Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba kushambulia vyombo vya habari bungeni kwa madai kuwa vyombo hivyo kazi yake ni kufanya uchochezi.

Akizungumza katika kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star TV asubuhi hii Balile amewapongeza wabunge Peter Serukamba na Jenister Mhagama wa CCM walioungana na wale wa upinzani kulaani mswada wa serikali wa kuzidi kukandamiza wanahabari.

Mwigulu Nchemba akichangia Mswada huo bungeni kwa kutumia lugha kali na ya kuudhi alivishambulia vikali vyombo vyote vya habari na hasa magazeti kwa madai kuwa lengo lao kubwa ni kutaka nchi isitawalike.Pia alilaani Chadema kwa kutoa hotuba ya upinzani iliyokuwa inatetea wanahabari.

Hata hivyo bunge liliukataa mswada huo kwa kauli moja hali iliyomsononesha sana Mwigulu Nchemba.

mwigulu ndo nani vile?kwetu mwigulu maana yake ni maka.......o!
 
Siasa za mwigulu zimeshindwa na zimepitwa na wakati, nchi ilishatoka kwenye siasa za zidumu fikra za mweneyekiti zamani sana yeye hasipobadilika upepo wa mabadiliko utamzoa
 
Back
Top Bottom