Mwigulu Nchemba na mkandarasi, China Civil Engineering construction corporation biashara yenu ina harufu mbaya

Mbona Lot 6 ipo kwenye manunuzi bado kwa mujibu wa Masanja Kadogosa wewe unavyosema mwigulu kaipa tenda CCEC lini,au umeamua kumchafua tuu waziri? Maana wakati wa uwekaji jiwe la msingi kipande cha Makutupola to Tabora vilizungumziwa vipande vilivyobaki hasa cha Tabora to Isaka.Hautajisikia mahali popote kuwa CCEC imepewa kazi ya kujenga Tabora to Kigoma mkuu.
Mkuu isijekuwa tunajilisha upepo humu kumbe sukuma gang kaleta uzushi..

Huyo mtoa mada ana malengo Gani ikiwa Mkandarasi wa lot 6 hajapatikana ila amekuja kumchafua Mwigulu humu?

Nadhani hapa bila shaka kuna msuguano huko ndani.
 
Huu ni upumbavu wa watanzania wengi na wewe ukiwemo,

Hoja ni ufujaji wa matrioni ya fedha kwa ujenze wa reli, halafu umaleta umalaya wa kikekike hapa!
Hasira ya nini km ripoti hujaisoma kalisha makalio hapo haijatajwa Reli ya Isaka tu, ingia Google Ukaguzi utakuta na mwaka 2020/2021 usitukane Wakaguzi, hii ya Reli Kampuni hiyo hiyo CCECC ndio inajenga Daraja la Busisi na huko wamepiga riba tu licha ya malipo
Kwa kuzingatia masharti ya malipo na ucheleweshaji halisi, mwajiri alitakiwa kulipa riba kwa mkandarasi ya Sh. 1,647,512,028.19. Hata hivyo, katika kupitia nyaraka za malipo kwa Mhandisi Mshauri msimamizi na Mkandarasi, nilibaini kuwa Mwajiri alilipa riba ya Sh. 1,553,097,096.80 kwa ucheleweshaji wa malipo ya wakandarasi kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 10-3 hapa chini
Mapitio ya barua yenye kumbukumbu namba CCECC/TANROADS/20190805/002 ya tarehe 5 Agosti 2019, yalionesha kuwa, kuchelewa kumpata mshauri mwelekezi kulisababisha Mkandarasi kushindwa kuanza kazi kwa vile Mhandisi Mshauri angekuwa hayupo kwa ajili ya kutoa mwongozo wa kazi

fungua uk 179 yapo mambo ya Kampuni ya CCECC inayolalamikiwa kwenye reli hapa wapo pia kwenye Daraja
[ICODE][/SIZE][/I] [SIZE=2]SURA YA KUMI UKAGUZI WA KIUFUNDI WA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGOBUSISI 10.1 Utangulizi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Barabara Tanzania inatekeleza mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigongo Busisi lenye urefu wa Kilomita 3.2[/SIZE][I][SIZE=2][/ICODE]
 

Attachments

  • RIPOTI_YA_UKAGUZI_WA_MIRADI_YA_MAENDELEO__MWAKA_2020_21 (5).pdf
    3.3 MB · Views: 4
Mgunga piri,hebu nisaidie,katiba mpya bira uadilifu inazuiaje wizi?
Mkuu uadilifu ni neno mtambuka
ie.uzalendo ambalo tunaimba kila siku lakini implementation ni zero kabisa
Udilifu huanzia kwenye family ties likikosekana hili taifa lina angamia
Kuna philosophical questions ya social contract baina ya mtawala na mtawaliwa hii ndio mwarobaini wa matatizo yetu
Katiba itaweka road map nni tufanye
Lakini currently unaona sarakasi zinavyo fanyika
 
Mchina ndiye anagharamia mradi huo, hawezi kubali hela iende kwa nchi nyingine.

Chadema mmemaliza kuomba omba Hela mitaani?

Umeshafanya retirement za mamia ya mamilioni ya Chadema uliyolipwa kwa kigezo Cha kukaa Dsm kuripoti kesi ya Mbowe ?
Mada imekuzidi uwezo ndo maana badala ujadili mada umekuja na ujinga.
 
CCM Especially ndugu Kinana Tunaomba uchukur hii hoja Sisi huku mbuzuzu hatujui kama ni kweli au ni uongo
 


Kwa ivyo mchina huyu huyu anaejenga miradi luluki ya Nigeria railway network na infrastructure project nyingine kubwa duniani; akija Tanzania awezi kazi.

Serikali ya bi tozo ni ya ovyo aijawahi tokea hilo halina ubishi, lakini ebu wakosolewe kwa yale wanayo haribu kweli, na yapo mengi.

Kabla ya kukosoa ungetuambia mchina alikuwa anatakiwa kuwa keshafanya tasks gani ndani ya miezi 16 kwa mujibu wa mkataba.

kusema tu amefanya 4.4% aina maana mradi utachelewa kuna task zingine zinachukua muda mrefu than others.

Kwa haraka haraka tu, kabla ya kuanza kazi inabidi ajenge karakana, feasibility ya njia, alete vitendea kazi, atafute subcontractors, atoe training ya wafanyakazi; na mipango mingine luluki ambayo ujatueleza ilitakiwa ichukue muda gani.
 
tuliona watu walitumbulkwa na wengine kufilisiwa majumba akina masamaki huyu mkuu wa inchi hawezi kuwa na uamuzi muzito kama huo
Huto Masamaki aliachiwa na mahakama kuwa hana hatia na hajafilisiwa..uwe unafanya tafiti kabla hujaandika hoja.
 
PUMBU mkubwa huu mradi kauanzisha Mwigulu, Riport ya CAG imetoa ripoti ya JPM miezi 9 Sasa Reli ya Isaka na mradi wa Busisi no wa lini? km hujui kufungua PDF ya Ukaguzi ninyi ndio mlitoroka shule kueimda Ndege na ushabiki wa taputapu, usibishe usilolijua

Hebu soma tena ulichokiandika hapa wewe KILAZA ,hata kuandika tu hujui ndio utaweza kusoma report ya CAG na kuilewa wewe ZUZU?
 
Mwigulu Nchemba, mmeingia makubaliano ya awali na kampuni ya China Civil Engineering construction corporation kwa utaratibu wa single source (bila ushindani) yenye thamani ya Shs. 6,698,935,255,040.00 kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ bila ushindani.

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 16. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni mzaha.

Utaratibu wa ‘single source’ ni LAZIMA mkandarasi awe amekidhi vigezo na uwezo. Huyu mkandarasi wa Mwigulu hana sifa hizo. Miezi 16 ameshindwa kupeleka hata ambulance, hakuna usala kwa wafanyakazi, na amefanya kazi kwa 4.4%. Mkandarasi huyu hajakidhi vigezo vya single source.

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation tena kapewa ujenzi wa lot Na. 6 ya kutoka Tabora - Kigoma (411km). Na gharama za ujenzi wake ni US$4.8M (Sh.11.1bn) kwa kila 1km. Hivyo kwa 411km mkandarasi atatumia Shs. 4.6 trilioni. Kapewa tender bila ushindani.

Phase 1 Dar es Salaam – Morogoro (300 km) kandarasi ni Yapi Merkezi na Mota Engil Africa. Phase 2 Morogoro- Makutupora (422 km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Phase 3 Makutupora–Tabora (294 km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Kumbuka, phase 3 imegharimu US$1.9 billion (TZS 4.4 trillion)

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) ndugu Mwigulu, ametokea wapi hadi kupewa kandarasi ya trilioni 4.6 wakati kwa miezi 16 amejenga lot Na. 5 kwa 4.4% pekee? Dar Es Salaam - Mwanza ujenzi wake jumla ni Shs. 14.7 trillion (US$6.4 billion).

China Civil Engineering construction corporation (CCECC) Tabora - Kigoma (411km) amechukua Shs. 6.7 trilioni. Zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimetengwa kwa ujenzi wa Dar Es Salaam - Mwanza ujenzi wake jumla ni Shs. 14.7 trillion (US$6.4 billion). Ni UJAMBAZI hakuna shaka.

Kwamba Rais (ambaye ni mwenyekiti wa mikutano yote ya Baraza la mawaziri) hajui lolote kuhusu wizara ya fedha na mipango chini ya usimamizi wa waziri Mwigulu Nchemba kutumia single source yenye BID ID 421346 ambayo ipo secured? Opening na Closing date yake ni siku moja 04/04/2022

Sheria ya Ununuzi wa Umma Na.7 ya mwaka 2011 imefutwa lini? The Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) haina mamlaka tena? Zabuni shindanishi zimefutwa lini na bunge? Kwamba waziri anaweza kutumia ‘single source’ idhini ya PPRA kutoa Shs. 6.7 trilioni bila kumueleza Rais?

Utaratibu wa ununuzi katika kazi za ujenzi, ununuzi wa huduma na bidhaa kwa njia ya “single source” unasimamiwa na Kanuni ya 159, 160 na 161 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2013 kama zilivyofanyiwa marekebisho na Tangazo la Serikali Na. 333. la mwaka 2016.

Kwa utaratibu wa ununuzi wa ‘single source’, PPRA inatakiwa kuhakikisha wanapata wazabuni wenye sifa, uzoefu na uwezo wa kutekeleza mikataba hiyo kwa haraka na ndani ya muda wa mkataba na kuhakikisha Serikali inapata thamani ya fedha kwa manunuzi yote yatakayofanyika.

Edward Lowassa akiwa waziri mkuu na Dk. Ibrahim Msabaha walipotimuliwa serikali kwa shinikizo la tume ya Harrison Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni (procurement and tendering) katika kashfa ya RICHMOND. Sheria ya manunuzi ya umma ikaongezewa meno.

Richmond; kampuni ilipewa tenda ya kuzalisha umeme huku ikiwa haina fedha, wataalam wala ofisi. Ndiyo iliondoka na Edward Lowassa. Sasa hawa China Civil Engineering construction corporation nao wamepewa tenda katika mazingira kama hayo. Mwigulu anakiri kweli hawakuwa na fedha

Richmond; kampuni ilipewa tenda ya kuzalisha umeme huku ikiwa haina fedha, wataalam wala ofisi. Ndiyo iliondoka na Edward Lowassa. Sasa hawa China Civil Engineering construction corporation nao wamepewa tenda katika mazingira kama hayo. Mwigulu anakiri kweli hawakuwa na fedha

Athari za kutumia mzabuni mmoja kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ ni kiini cha rushwa, uzembe, upendeleo, pamoja na uwezo mdogo wa mzabuni. Ndiyo sasa tunaona yanayotokea kati ya Mwigulu Nchemba na China Civil Engineering construction corporation.

Mfumo wa ushindani wa wazabuni wengi, ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi, huchukua takriban miezi mitatu au zaidi hadi kutangazwa mshindi. kutoa zabuni bila ushindani kunaleta upendeleo kwa baadhi ya wazabuni kwa gharama za watu wengine. Rushwa inaweza kutamalaki.

Katika mfumo huu, kuna uwezekano mkubwa wa kutekeleza miradi chini ya kiwango, hili ni jambo ambalo uzoefu unaonesha yapo maeneo ambayo miradi mingi haijadumu kwa sababu ya kutekelezwa chini ya kiwango, lakini gharama za mradi zikiwa za chini. Mashaka ni makubwa sana.

Gharama za mradi zinaweza zisiwe halisi. Kwamba zinaweza kuwa gharama kubwa zaidi, maana makubaliano ndio yanasimamia gharama za mradi. SASA hili la Mwigulu kupigania kandarasi ya CCECC bila uwepo wa zabuni shindani ni jambo lenye mashaka mengi ya dhahiri na lazima tuhoji.

Ahsante pia Aeshi Hilaly, mbunge wa Sumbawanga Mjini, nimeona bungeni ukimueleza Mwigulu Nchemba kwamba wewe na kamati yako ya miundombinu mmefika hadi kwenye ujenzi, hamridhiki na ujenzi wa lot Na. 5 na kuna ufisadi mkubwa katika zabuni ya ujenzi wa lot Na. 6. Barikiwa

MMM, Martin Maranja Masese
unafikiri SAMIA hajui? no question, she is part and parcel.
 
Hebu soma tena ulichokiandika hapa wewe KILAZA ,hata kuandika tu hujui ndio utaweza kusoma report ya CAG na kuilewa wewe ZUZU?
Hujui ninachokielezea, umeng'ang'ania point moja tu ya upigaji wa pesa ya Mwigulu ktk Reli ya Isaka na Kampuni ya CCECC, huko tumetoka tunazungumzia upigaji wa Mwendazake kiujumla kapeleka mihela huko wakati haikupitia Bunge.
ripoti 2020/2021 imesema nalo Daraja la Busisi limo na miradi kibao
YALIYOMO

ORODHA YA MAJEDWALI....................................................................iv

MUHTASARI .................................................................................. xv

SURA YA KWANZA............................................................................ 1

HALI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA UKAGUZI ........... 11

UTENDAJI WA KIFEDHA NA USIMAMIZI WA MATUMIZI............. 20

UNUNUZI NA USIMAMIZI WA MIKATABA...................................... 57

HALI HALISI YA UTENDAJI WA MIRADI ......................................... 69

UKAGUZI MAALUM WA UJENZI, VIWANJA VYA NDEGE …..107

BARABARA ZA JIJI LA DODOMA ......................................................130

USAMBAZAJI WA MAJI...............................................................150

UKAGUZI UMWAGILIAJI NCHINI.................................................168

SURA YA KUMI .................................................................................179

UKAGUZI WA KIUFUNDI WA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI...179

SURA YA KUMI NA MOJA .................................................................192

UKAGUZI UJENZI WA HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA NA

KANDA .......................................................................................192
 
Hujui ninachokielezea, umeng'ang'ania point moja tu ya upigaji wa pesa ya Mwigulu ktk Reli ya Isaka na Kampuni ya CCECC, huko tumetoka tunazungumzia upigaji wa Mwendazake kiujumla kapeleka mihela huko wakati haikupitia Bunge.
Zitto Kabwe kasema ripoti 2020/2021 imesema hela imepelekwa nyingi ya kifisadi.
Kwa hiyo humu jukwaani unataka tusijadili mengine ya wizi? Mobutu alikua na Mji Globetore hata hapa utapotea, nacho huamini
YOTE NANI KASABABISHA
Awamu zote zimeoza
 
Kuna hii tabia ya vijana wa ccm kuunga mkono kila kitu, na hii wataunga mkono lakini siku akikamatwa kwa ufisadi anaofanya vijana hawahwa wa ccm nao wataunga mkono kikamatwa kwake! Hawa ndio vijana wa ccm wasiotaka kufikiri au kutumia akili zao
 
Of course Katiba mpya haiwezi kuleta Suluhu ya ufisadi ila itaweka nafuu ya udhibiti..

Tanzania hii wizi ni hulka ya jamii yetu na ni tatizo la kijamii labda tuanze kuweka mkazo kwenye shule za watoto kuanzia wakiwa chekechea.
Asikwambie Mtu anayesema katiba mpya sio dawa ya ufisadi basi ni fisadi.

Ukishakuwa na mahakama huru, Rais Huru, Bunge Huru? Polis na Jeshi Huru huyo fisadi hana pa kupumulia
 
Nakazia
kuna kipindi mnavyolalamika na haya malalamiko yenu ndio maana wengine tunasema yule Mwamba JPM alikuwa anafaa sana...

nchi hii ili mambo yaende yanahitaji, ubabe, ukatili na unyama wa hali ya juu...kifupi kuna watu wanapaswa kufa na makaburi yao yasionekane kabisa, wengine wanapaswa kukaa kwenye jela zenye mateso makali...

Mwisho kabisa, HAKUNA DEMOKRASIA KWA MPUMBAVU, vinginevyo mtalalamika sana..
 
Back
Top Bottom