Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Tamko la jana la mahakama limewafanya baadhi ya watu kuona kama CHADEMA ni chama chepesi sana na ni kama kinaanguka kesho,hili si sahihi!!
Kinachoipa nguvu CDM ni kuwa kuna watu wanaotaka mabadiliko na wengine wamo hata ndani ya serikali na chama tawala.
Hawajionyeshi wazi lakini kama umeme ulsivyoonekana lakini nguvu yake iko wazi.
Tujikumbushe imekuwaje kesi za ugaidi zimetokomea?
Kwa nini serikali inakatalia vitu vya wazi kabisa kama kuunda tume ya kimahakama ya kuchunguza vifo vya utata?
Ni suala la muda tu!!
 
Wana JF

Napenda tu kuwatayarisha wenzetu wa CHADEMA kuwa mwaka huu jiandaeni hamna rangi ambayo hamtaiona. Niliwahi kuandika humu ndani juu ya fedha chafu zilizoandaliwa kuimaliza CHADEMA kupitia vyombo vya habari nadhaini watu wengi hawakuelewa. Ukitaka kulifahamu hilo kwa mtu mwenye uelewa wa kupambanua mambo tazama magazeti ya leo. Angalia vichwa vya habari vya magazeti ya leo na habari zilivyoandikwa kwa mtizomo na mtiririko fulani kwa malengo fulani, hupati shida kujua zimeandikwa kwa malengo gani,tazama picha zilivyowekwa kwa aina fulani kudanganya watu wa mikoani. Mimi nimeshaona na natabiri mwaka huu utakuwa mgumu kwa CHADEMA ni vizuri viongozi wa juu CHADEMA hasa Slaa, Mbowe,Lisu, Mnyika kujiandaa kisaikolojia kwa kuwa nawaambia wakishangaa haya ya zzk wanaweza kuona ya Ulimboka au ya Mwangosi achiliambali kesi watakazofunguliwa, Mungu apishilie mbali.


Mganga njaa tu huna lolote! Chadema inajimaliza yenyewe haiwezekani chama kiwe chini ya viongozi ambao wazinifu; waongo na wezi ambao wanajali maslahi yao zaidi kuliko ya chama halafu eti utegemee chama kiwe imara!
 
Amina, hata Yesu ambaye alikuwa mkombozi walimdhihaki na kumpinga. Huu ni mpango wa Mungu na katika safari lazima kuwe na changamoto nyingi ili ufike Kanaani. Tunakabiliana na changamoto na Kanaani inatuhusu. ZZK ni sawa na kijinga cha moto ambacho kinajaribu kupasha moto maji ya bahari. Maji yametulia unataka kuyapima nguvu kwa miguu, mtoto amelilia wembe sasa ameshaona madhara yake.
 
Hahahahahaaaaa, eti magazeti yote yamehongwa! Au wewe ndo unachukia ukweli ulioandikwa kwenye magazeti hayo?
 
mbona na nyie hamtaki kujibu hoja za wazi kama matumizi mabaya ya fedha za ruzuku, kupokea fedha kutoka kwa mafisadi, kuhongwa ili msifanye kampeni kwenye baadhi ya majimbo kama la mkono, kupokea misaada kutoka nje na kwenda kuanzisha gazeti binafsi la tanzania daima,
kutumia hela za uma kwenda kutalii na kimada dubai.... Nk.

Msihangaike kujisafisha, tumesha wagundua.
 
Mganga njaa tu huna lolote! Chadema inajimaliza yenyewe haiwezekani chama kiwe chini ya viongozi ambao wazinifu; waongo na wezi ambao wanajali maslahi yao zaidi kuliko ya chama halafu eti utegemee chama kiwe imara!
Mkuu, akili za huyu hazina tofauti na akili za mwenyekiti wake ambaye amesema kuwa kupata fedha na ccm si tatizo bali unapewa kwa malengo gani namunazitumiaje
 
Mtu akikaribia kukata roho hata kama ni kwa ugonjwa unaofahamika sharti mtu ashikwe uchawi. Kwetu kuna jamaa mmoja alijinyonga lakini watu kadhaa walishikwa uchawi. Ni sawa na hii misukule ya CHADEMA
 
Kama za Ugaidi tulishinda why this tushindwe!!! Wako wapi waliokuwa na ushahidi hadi Mbinguni? wako wapi waliotukana kumbe wao ndio walikuwa wanawasiliana na hao waliowaita magaidi tena kwa kuwatumia pesa kwa njia ya simu na kuwaita Dodoma? Ni Mpuuzi tu atakyeona kuwa Chadema inakufa..........ni msaliti na mroho wa madaraka tu atakyeona unyonge na udhaifu wa Chadema kuwa ndio mwisho hahahaaaa, ni mwanzo tu wa ushindi zaidi
 
Hahahahahaaaaa, eti magazeti yote yamehongwa! Au wewe ndo unachukia ukweli ulioandikwa kwenye magazeti hayo?

CDM haiwezi kufa kwa kutumia magazeti,njooni field muone muziki wake! huyo savimbi alivyo mwehu anasema eti haitapata hata mgombea wa udiwani wakati chama cha mizigo kipo taabani BUNDA kwa kukosa mgombea hadi kulazimisha watu wachukue fomu tena bure huku CDM watu wakigombania fomu! ni mwendawazimu tu anayeweza kuwa na akili za kuku na kujifariji hivyo.
 
Kama naibu katibu mkuu anaiwazia chadema hivi,je wananchi waonakiunga mkono chama hiki nao atawamaliza wote baada ya 2015? Maana mtu mzima kuwa na maona ya vifo mara kwa mara ni wendawazimu kabisa,huyu ni mgumba wa akili,tasa wa hekima 100%.
Badala ya kuhakikisha wanadumisha huduma za jamii ili wananchi walio chadema warudi ccm wao wanawaza vifo tu,tutauwana mpk leo Mh mwigulu nchemba????
 
Mtu akikaribia kukata roho hata kama ni kwa ugonjwa unaofahamika sharti mtu ashikwe uchawi. Kwetu kuna jamaa mmoja alijinyonga lakini watu kadhaa walishikwa uchawi. Ni sawa na hii misukule ya CHADEMA

Mwambieni savimbai aende na SOMBETINI akavune aibu! teh teh teh teh teh teh...mimi ntakuwepo BUNDA kuwashikisha adabu magamba! mtaendelea kufarijiana kuwa inakufa huku CDM ikivuna kata zenu mlizoshinda 2010 kwa kwenda mbele,february si mbali!
 
Mkuu, akili za huyu hazina tofauti na akili za mwenyekiti wake ambaye amesema kuwa kupata fedha na ccm si tatizo bali unapewa kwa malengo gani namunazitumiaje

Siasa zenu zimebaki mitandaoni tu! field bila maroli/mafuso hata chekechea hawajitokezi.kama kweli mnakubalika na chama chenu chakavu achaneni na mafuso tuone!
 
Mwigulu,

Poleni sana, kwani mbinu mlizotumia kukiua CDM imagundulika. Kila siku matamko, CCM itagawanyika vipande vipande kabla ya 2015, take from me.

Kama umeangalia hiyo move iliyogundulika CDM, ilianzia DUCE. Wote waliofukuzwa CDM walipitia/wapo DUCE, na waliletwa CDM kukivuruga ama kukiua kabisa, ila kwa vile tupo na Mungu uchafu wote umegundulika. Mwampamba, Machange, Yona, Dr. Kitila......wote hao ni product ya DUCE, na DUCE ni mali ya serikali na Kitila ameajiriwa na Serikali.

Kila uchafu fanyie Upinzani ila YATAWARUDI muda si mrefu...
 
Mtu akikaribia kukata roho hata kama ni kwa ugonjwa unaofahamika sharti mtu ashikwe uchawi. Kwetu kuna jamaa mmoja alijinyonga lakini watu kadhaa walishikwa uchawi. Ni sawa na hii misukule ya CHADEMA
Aaah cdm ife sababu kumtimua zitt? Sahau kabisa hii sio ccm ambayo mwenykt wake alisema wajivue magamba baadae akaanza kulalama eti wenzake wamemgeuka...hawez hata kucmamia maamuz yake....
 
Haya yanayotokea ndani ya CDM ni muhimu ili kujenga CDM imara zaidi tutaingia kwenye chaguzi huku tukijua adui wa ndani hana nguvu tena.

Hujuma alizozifanya 2010 hataweza tena.
 
Si chama cha wa chaga ni chama cha watanzania jamani. Ama kweli ukiamua kumchukia mtu. Siamini kama anayesema hivi ana dini kwa sababu kwa sisi Roman ni sawa na kufungiwa dhambi na kufa nayo. Sijui kwa wenzetu wengine lakini haipendezi kujitoa ufahamu na kuendelea kuongea ukabila wakati wote ni watanzania. Na ningelipenda tufahamu kwamba kila kitu kina mwanzo wake. Sitegemei kama chama kianzishwe kilimanjaro halafu kikose wafuasi wengi huko wakati misingi na kanuni zake zinaeleweka. Ndugu yangu naomba usije ukafa na dhambi hiyo bule haina sababu ijapokuwa mimi si mchaga ila sipendi hiyo kauli mbiu.
aka mkosa chama tatizo la Watz tunashabikia tusilolijua kwani hamjua vita iliyopo cdm? kama hamjui hicho chama cha wachaga mtadanganyika mpaka lini fuatilieni mtaona au ni chama cha mzee Mtei
 
aka mkosa chama tatizo la Watz tunashabikia tusilolijua kwani hamjua vita iliyopo cdm? kama hamjui hicho chama cha wachaga mtadanganyika mpaka lini fuatilieni mtaona au ni chama cha mzee Mtei
hiyo sio hoja ya kuwa chadema ni chama cha wachaga..! ila unaonekana hujui nini maana ya vyama vingi.
 
Back
Top Bottom